Wakoma wageuka Mashujaa na kuiokoa Nchi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,551
(2 Wafalme 7:1-20).

Nasummarize Kwa uchache,

Washami wakaizingira Nchi nzima ya Israel, Israeli ikapata habari na kufunga malango yote ya nchi!!

WAKOMA 4 nao wakafungiwa nje ya mji. Kufungwa malango ya mji kukazuia supply yote ya vyakula, bidhaa nk.

Njaa ikawa kuu sana nchini, waisraeli wakafikia hatua ya kula MAVI ya njiwa kupunguza makali ya njaa!!!

WAKOMA wanne wakasemezana, mbona tunakaa hapa hata tufe? Tukisema tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo!! Nasi twende tukaliendee Jeshi la Washami, wakituhifadhi hai, TUTAISHI; WAKITUUA TUTAKUFA TU!

Walipoondoka, BWANA akawasikilizisha Washami kichindo Cha miendo ya magari, na kishindo Cha farasi, kama kishindo Cha JESHI kubwa.

Washami wakakimbia na kuacha silaha, fedha, vyakula, nguo, farasi, na magari ya farasi, WAKOMA WANNE,kufika kambi ya Washami, hakuna mtu, ilikuwa usiku!!!

Wakala na kunywa na kufurahi, baadae likawajia wazo, Wakasemezana, Si vyema kunyamaza na habari hii njema, twende tukawaarifu waisraeli wenzetu na mfalme!!

Nchi ilipata habari, watu walitoka nje na kwenda kujipatia chakula na mahitaji Kutoka ktk vitu walivyoacha Washami!!

Tangu siku Ile hawakuitwa WAKOMA tena, waliitwa MASHUJAA na WAZALENDO!!!!


UJUMBE;
1. Mungu hufanya KAZI na Wachache wenye Imani na ujasiri!!!

2. Inakuja njaa kali juu ya nchi, na asili ya njaa Haina Baunsa!!!

Njaa imewafanya mabinti wadogo kukodisha miili Yao Kwa chakula ingawa NJAA imezidi Badala ya kupungua wakiwa ndani.

Njaa imewapeleka vijana betting na wengine Viwanjani kujifariji stress lakini NJAA ikaongezeka wakiwa ndani.

Njaa imesababisha matching guys kuvamia hifadhi za barabara zetu na nje ya maduka ya wenye kulipa Kodi Ili kupata unafuu wa matumbo Yao, lakini NJAA haikuisha,

Njaa imewafanya vijana wakimbilie bodaboda kama ajira wakiamini njaa itaisha, matokeo yake wengi hawana tena miguu Kwa Ajali, njaa imezidi pasi kuondoka.

Njaa imewaamsha PANYA road Kutoka kwenda kuwadhuru dada na mama zao, kupora simu ya laki 7 na kuiuza Elfu ishirini Ili kupoza njaa lakini NJAA haikwisha, Badala yake imezidi.

Njaa imewafanya wamama wauze walivyonavyo Ili kwenda kununua maji na mafuta ya upako Kwa manabii feki Ili wapate utajiri na kupona magonjwa Yao, lakini NJAA na magonjwa havikuisha imeongezeka wakiwa ndani.

Njaa imewafanya wamama kuuza vitanda na magodoro na samani za ndani Ili kupata pesa ya matibabu ya watoto wao wasio na bima, pamoja na kupeleka pesa hizo, Bado hazikutosha Kwa chakula na matibabu wakiwa ndani!!!

Wakati hayo yakiendelea ndani kwa maskini, upande wa pili Wana maisha Bora, chakula tele, pesa wanazo nyingi hazina idadi, matibabu Bure, usafiri Bure,hawalipi Kodi, wanapokea Kodi,wanakula wakitakacho, hawalipi bill yoyote, Kila kitu ni Bure, hawana habari juu ya nini kinaendelea upande wa pili wa maskini.

4. WAKOMA 4, walipochungulia nje kwenye kambi ya Washami waliona vyakula tele, maji ,fedha, pesa na Dhahabu na Kila aina ya utajiri!!! Ingawa waliona pia hatari ya KIFO mbele Yao ila hawakuogopa!!

Wakasema twende tukadai chakula, tukifa na tufe, kusipokufa ni Bahati kwetu.

Je wawajua WAKOMA wanne ni akina nani?

Nawasilisha.
 
Wakoma walipofika kule kambini Washaam( Jordan na Yemeni) wakadhani kuna wahaini wanakuja kutupindua.

Biblia inasema walidhani wamekodi majeshi ya Wahiti na Wafilisti( mabeberu) wakala nduki.
 
Eti wanatutishiwa kifo sie WAKOMA 4, tuliotengwa, tumepigika, no food,hamna Kila kitu!!!

Mkoma got nothing to loose!!!

Tukijificha tutakufa, tukienda Ili tukafe, Mungu ataenda nasi Ili kuiponya Nchi.

Neno la Mungu ni Kweli na AMIN!!
 
Back
Top Bottom