Wako wapi wafuasi kindakindaki wa Magufuli?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Wote tulitegemea baada ya kifo cha ghafla cha Rais Magufuli, tungeona kundi fulani likijipambanua kuwa ni wafuasi kindakindaki wa Magufuli na siasa zake.

Hii tulitegemea ingeleta siasa kali za ushindani mkubwa ndani ya CCM, zile siasa tulizokuwa tunazisema za CCM-Asilia na CCM-Magufuli. Najua Magufuli alijaribu sana, ingawa nadhani kwa mafanikio madogo, kujijengea wafuasi wake wa kisiasa. Wengi aliwapa vyeo, wengine wengi akawaingiza Bungeni.

Cha ajabu, toka kifo chake kumekuwa na ukimya wa ajabu kutoka kwa watu hawa. Wengine wamepata hata ujasiri wa kupinga waziwazi baadhi ya sera zake. Na mwenendo unavyokwenda, inaonyesha mbinu anayoenda kutumia Rais Samia ni kuwatumia hawa hawa watu waende kufichua madudu yoyote yaliyokuwa yanafanyika. Anaenda kulivunja hili kundi kwa kutumia mikono yao wenyewe. Wengi wasipokuwa makini wanaenda kupotea kabisa kisiasa.

Inamaanisha, katika miaka mitano ya utawala wake, Magufuli hakufanikiwa kushawishi viongozi wa kutosha wa kusimama kidete na kutetea kile alichokuwa anakisimamia?

Mbona baadhi ya wananchi wa chini waliamini sana katika 'Maono ya Magufuli'? Ina maana hakuna mtu hata mmoja ndani ya CCM aliye na utashi, matamanio na ujasiri wa kisiasa wa kuwa mobilize hawa watu, ili kufaidika na mtaji wa kisiasa alioacha Magufuli?
 
Magufuli hakuwa na wafuasi Ila wachumia matumbo na watu waliojaa njaa, wanafiki na waoga, watu wenye kujipendekeza kulikopitiliza, waimba myimbo za mapambio na sifa za kukufuru.

Hawa watu ndo hasa lile kundi hatari Sana lililokuwa pembeni mwa Bwana Mtukufu wa Chato sie twawaita (chawa) ama kupe, maana kupe ataishi kwa kukunyonya damu maisha yake yote. Ili kupe aishi na akue lazima asilete bughudha kwa mnyonywa.

Watu Hawa hawakuwa na upendo na taswira ya kweli kwa Magufuli kwani Mara baada tu ya Magufuli kufariki, tayari upepo umewapeperusha na Sasa wamehamia kwa SSH kufanya Kama kile walichokuwa wanakifanya kwa Magufuli.

Mfano Kuna Zwazwa moja tapeli la Kidini linajiita Masanja Mkandamizaji, hili lijamaaa lilisifu weee na kugalagala kwenye madaraja lakini Magufuli hakuliona linafaa kuwa hata katibu kata, Sasa Magufuli kafariki limeibuka Tena Kwa Samia, linasifu ujinga tu lengo 'Uteuzi'.

Watu Kama akina Kigwangala ndo walikuwa begakwabega na Mtukufu huyo lakini hapa juzi tu ajipambanua kwa kukosoa kile Mtukufu wa Chato alichokuwa anaamini. Kaongea meengi lakini lengo lake likiwa kuikosoa serikali Iliyopita juu ya kuipuuzia Corona kwa kuruhusu utumiwaji wa njia za jadi ikiwa nipamoja na utumiaji wa nyungu (kujifukiza) na mambo Kama hayo.


Ametoa ushauri wa kidaktari na kupendekeza Chanjo nzuri ambayo italifaa Taifa, ameishauri serikali ya SSH iagize chanjo ya Corona.
Sasa watu Hawa ndo walikuwa wapambe wa Mtukufu wa Chato lakini leo hii wamegeuka wapinzani kuliko hata wapinzani wenyewe .

Mtukufu wa Chato Hana chake na ajiandae kusahaulika kwa muda mchache tu. Waswahili husema, “atupae tope humrukia yeye mwenyewe”.
 
Ushawishi ni bora kuliko shuruti, Magu hakutengeneza wafuasi wengi kwa sababu alipenda kutumia shuruti na ukitumia mabavu watu watakusikiliza lakini hawatakuamini!
 
Ushawishi ni bora kuliko shuruti, Magu hakutengeneza wafuasi wengi kwa sababu alipenda kutumia shuruti na ukitumia mabavu watu watakusikiliza lakini hawatakuamini!
Labda Magufuli alikuwa anafuata mafundisho ya Machiaveli aliyesema, ni vizuri kujaribu kupendwa na kuogopwa ila kama ikishindikana kupata vyote viwili, basi ni afadhali kuogopwa.
 
MJG.jpg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom