Wako wapi Salum Mwalim, John Mnyika?

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,012
Wanaukumbi.

Kwa muda sasa sijawasikia hawa makamanda Salum Mwalim, John Mnyika, Tundu Lissu, hata ukipita Makao Makuu ya Chadema pale Ufipa ni ngumu kuwapata.

Tulizoe kusikia na kuona matamko yao kila baada ya muda kupitia kwa Tumaini Makene ambaye naye hajulikani alipo.

Kwa habari za ndani kabisa kama tulivyoambiwa na mfuasi mmoja wa Chadema pale Ufipa anajulikana kwa jina moja tu Kabwela, kuwa sasa hivi shughuli za chama zinafanyika Masaki kwa Lowassa, siyo Ufipa tena na huko ni vigumu kufika wao.

Anasema hata huyu Katibu Mkuu mpya naye uwa anakuwa Masaki pia, Ufipa tupo siye tu alisema Kabwela.
 
Mafisadi ndani ya CHADEMA wamewanyima pumzi, na hawana pa kutokea!

Ikumbukwe kuwa alipoingia Lowassa tu, Slaa akajiengua kupinga mafisadi kuchukua chama.

Kina Myika na vijana wa ukweli nao kiuhalali wangeondoka, lakini waende wapi?
 
Wanaukumbi.

Kwa muda sasa sijawasikia hawa makamanda Salum Mwalim, John Mnyika, Tundu Lissu, hata ukipita Makao Makuu ya Chadema pale Ufipa ni ngumu kuwapata.

Tulizoe kusikia na kuona matamko yao kila baada ya muda kupitia kwa Tumaini Makene ambaye naye hajulikani alipo.

Kwa habari za ndani kabisa kama tulivyoambiwa na mfuasi mmoja wa Chadema pale Ufipa anajulikana kwa jina moja tu Kabwela, kuwa sasa hivi shughuli za chama zinafanyika Masaki siyo Ufipa tena na huko ni vigumu kufika wao.

Anasema hata huyu Katibu Mkuu mpya naye uwa anakuwa Masaki pia, Ufipa tupo siye tu alisema Kabwela.
Yuko wapi Kinana?
 
~~~>>Ukimya wa Mnyika unaleta maswali mengi yasiyo na Majibu..... Ukimya huu umeanza mwaka jana.

~~~>>Hata baada ya kuwa na Katibu bado naona chama hakisikiki tena..... Hapa kuna Changamoto.
 
~~~>>Ukimya wa Mnyika unaleta maswali mengi yasiyo na Majibu..... Ukimya huu umeanza mwaka jana.

~~~>>Hata baada ya kuwa na Katibu bado naona chama hakisikiki tena..... Hapa kuna Changamoto.

Viongozi na Wabunge wengi nguli wa CHADEMA ninaointeract nao wanakiri "nje ya kiapo" kuwa Katibu Mkuu mpya ni mzigo mzito. Hii project ya Mbowe inaweza kuishusha CHADEMA.
 
~~~>>Mimi nipo Kilimanjaro, Kabla ya Uchaguzi mwaka jana lilikuwa jambo la ajabu kujitangaza kama MwanaCCM

~~>>Leo hii ktk Magari na vijiweni habari ni Magufuli.... Jarbu kumpinga Magufuli uone shughuli yake wanaweza hata kukupiga.

Najiuliza kama Kilimanjaro imemkubali Magufuli je Dodoma na mikoa mingine ngome ya CCM itakuwa ktk hali gani???

Wapinzani tumebanwa!
 
Viongozi na Wabunge wengi nguli wa Chadema ninaointeract nao wanakiri "nje ya kiapo" kuwa Katibu Mkuu mpya ni mzigo mzito. Hii project ya Mbowe inaweza kuishusha Chadema.

~~~>Inawezekana amekosa Support ya Salum & Mnyika...... Ameachwa na Mwenyekiti tu.
 
Toka uchaguzi uishe wapo kimya sijui kwa nini.
Siyo tangu uchaguzi uishe sema tangu wampokee Lowassa.
Kamanda wa kweli hawezi kupigana vita katika kikosi kinachoongozwa na Lowassa. Mnyika kisha rudisha silaha armory, Salum Mwalimu kajiuguza.
 
Back
Top Bottom