Kuna wanamme wasafi hadi anakutoa mwanamke knockout
Ila kuna wanamme wachafu pia
Ila kama wako, mfunze kuwa msafi
Siku bajeti inaruhusu mnunulie vitu vizuri vizuri
Mnunulie deodorant, mist
Na akirudi home, nguo alovaa ziweke kwenye kapu la nguo chafu kabisa au loweka ili kesho asirudie
Nguo ambazo huzipendi, zigawe kwa shamba boi au mlinzi
Weka mikakati unamnunulia ya shati moja kila mwezi au unabadilisha mwezi huu shati unafuata suruali
SInglend na pichu tenga kulingana bajeti nenda kariakoo, utapata tu za cotton kwa bei nafuu
Ukienda na elf 70 mbona utaepusha aibu.
Mshurutishe kuwa msafi kwa kumsimamia aoge, aswaki, anyoe nywele, inawezekana kabisa.