Hay wanajamvi wenzangu
Mnaendeleaje na pilika pilika za maandalizi ya sikukuu ya Pasaka, na mambo mengine kiujumla, mwenzenu niko fiti naendelea vyema na shughuli zangu za kunipatia kipato cha kula.
Awali ya yote nimeonelea leo niongee au nizungumzie tabia chafu ya baadhi ya WANAUME ambao wamekuwa kero kila kona. Kitu ambacho nataka nikisema leo jamani wandugu tena naomba marafiki zangu wanaume wa humu jf mmu msinielewe vibaya kwa hoja hii. Ni kuhusu UCHAFU WA BAADHI YA WANAUME ambao umekuwa kero kwetu hasa jamii nzima, lakini sio wote ambao ni wachafu au wananuka, bali wako baadhi ambao wanajiendekeza kwa unukaji, na wengine
wanadiriki kuvaa nguo wiki nzima, wao hawaoni kuwa ni chafu bali ule UVIVU uliowatawala ndani yao wanashindwa hata kufua jamani. na wengine inapita siku tatu hawaogi, ukisema wanasema kuwa wao ni wanatashati, heee! jamani utanashati gani huo?
Sasa mtu kama huyo anayejifanya eyeye ni mtanashati hebu mfanye naye kazi sehemu moja kwenye meza moja huku Airconditioner iwe imewashwa utakimbia mahali hapo kwani huo uharufu unaotoka hapo utasema kuwa PANYA AMEFIA WAPI TUMTAFUTE, kumbe sio panya ni yeye ananuka vibaya, mbaya zaidi wengine wanashindwa hata kunyoa sehemu zile ............................... (sizitaji kwa usalama zaidi) kwani harufu ya huko si mchezo wengine ukipishana nao wananuka vinywa utafikiri wajapiga mswaki mwaka mzima jamani we acha, mm Lady sitaki kuongeza chumvi hapo ila nasema vijana, makaka zetu na mababa zetu jamani acheni tabia hiyo ya uchafu ni hatari kwa afya zenu na afya za familia zenu jamani. Labda niwashauri wanawake wenzangu kama mkiona wanaume zenu ni wachafu wasemeni msiwaogope kwani hao wamekuwa simba mpaka muwaogope, sema nao kwa nguvu zote, na kama hawajirekebishi basi chukua uamuzi wa kuwakimbia maana ni hatari kwa afya zenu.
Onyo: Akina makaka, mababa, vijana wetu acheni tabia ya uchafu kwa uvivu wenu wa kutokujipenda ninyi ni viongozi wa familia mnataka watoto wajifunze wapi huo uchafu wenu?
NASEMA JAMANI ACHENI TABIA YA UCHAFU NADHANI MESSAGE SEND