Wakili Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ili arejee nchini. Lakini, nani hasa amhakikishie usalama wake ili arejee nchini?

Raia wanapokuwa na hofu juu ya usalama wao ndani ya Taifa lao huru....kaa chini tafakari kwa kina.
 
Petro E. Mselewa , Wewe siyo wakili msomi kwa bandiko lako kuhusu rais kukosolewa ; mtizamo wako haukuwa wa kisomi hata chuo chako wanajuta kukuruhusu kuhitimu ili hali hukustahili kabisa.

Lissu, kwa sasa hajielewi kabisa. Mtu timamu huwezi ukategemea viongozi wako wa chama cha siasa tena kisichokuwa kwenye madaraka kuhakikisha usalama wako unaporudi nchini.

Ningemuona Lissu anajitambua kama angesema yaani angalau familia yake na serikali kwa sababu kuu mbili:
1. Familia imekuwa naye muda wote na ndiyo tegemeo lake kubwa
2. Serikali ; kwa vile ni jukumu la serikali kulinda watu wake; tena kauli ya kuomba ulinzi wake kutoka serikalini ungeiweka serikali katika mazingira ya kumlinda sana kuogopa kupata doa .

Sasa hapo bado hatujui aliyefanya yale kwake; je; kama ni viongozi wake wa chama chake walitaka kumtoa roho ili kuichafua serikali au kulinda madaraka ya baadhi ya watu katika chama chake?

Any way, Lissu baki tu huko , ule hela huko duniani huko singinda achana nako.
Utumbo kwa ndizi huwa ni muzuri sana,lakini ukivunda ni wa kufukiwa ndani ya shimo reefu,kwani hata mbwa hawautaki mwe!!
 
Hakuna zaidi ya mzee Meko hata hao askari yeye ni amri jeshi mkuu wa Tz
Siku za nyuma Lissu alikuwa chief whip kutoka chama kikuu cha siasa, alikuwa mbunge wa Singida ma..., alikuwa Raisi wa chama cha wanasharia Tanganyika nk. Sasa Lissu hana cheo chochote! Hivyo ni kama Mtanzania yeyote. Na kila Mtanzania amehakikishiwa usalama wake na serikali kupitia majeshi yetu yote. Hivyo, individual Mtanzania (Lissu) asianze kulazimisha special attention - he is not special. Kunawatu waliumizwa kwenye matatizo ya MKIRU, kwa hiyo hao watu wagome wasiende mabaweni, mashambani nk. Eti kwanza wadai usalama wao? Kuwapo kwa serikali inayo wajibika hii ya awamu ya tano ndiyo hakikisho la usalama wetu - Lissu included.
 
Da mambo mengine magumu sana kujadili,nimewaza sana hili jambo mpaka nikasinzia,kustuka nasikia abiria wanalalamika mbona dereva siondoi gari,nikawasha gari tukaondoka
 
eti nawewe una shahada ya sheria!!! so sadness

Makamanda mbona hampendi uhuru wa maoni? Sasa atalindwa na nani ikiwa anasema serikali ndio ina husika na shambulio lake? Hivi nani atamlinda?
 
Serikali ndiyo yenye wajibu wa kulinda raia wake,ikitokea serikali hiyo hiyo ikawa ndiye muuaji wa raia wake basi imekuwa jinamizi kubwa.

Mkuu wa serikali hiyo ni ni lazima ajiulize mara mbili mbili kama anatosha kuwa mkuu wa serikali huru,ama ni mkuu wa serikali dhalimu?
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
Unajua mara nyingi huwa tunasema huyu ndugu yetu Tundu Lisu akili zake haziko sawa. Akili yake imekuwa ikiamini kuwa serikali ndiyo iliyomtandika hizo risasi. Amekuwa akiituhumu serikali ndani na nje ya nchi kwa kitendo hicho. Serikali imekuwa ikikanusha na kumtaka yeye na dreva wake warudi nyumbani ili washirikiane na jeshi la polisi kukamilisha uchunguzi wa shambulio hilo ili hatimaye waliomshambulia watiwe nguvuni.

Sasa yeye kwa akili yake anataka serikali imuhakikishie kuwa haitamtandika tena risasi zingine atakaporudi nchini! Yaani anataka serikali iseme kuwa haitamshambulia tena! Hivi kwa mtu mwenye akili za kawaida utaomba kweli ulindwe na mtu ambaye unaamini ndiyo mbaya wako?

Sehemu ambayo iko 100% kwa usalama wa maisha ya mtu ni lockup (selo) ya polisi au ya magereza. Kupewa walinzi/ body guards hakuwezi kukuhakikishia usalama wako hasa kama wewe unaishi vibaya na wenzako. Kama wewe unaishi kila kukicha ni kutukana na kudharau wenzako unajijengea mazingira hatarishi na huwezi kuwa salama. Kwa hiyo Lisu anaomba serikali imuweke lockup atakaporudi maana kule ndiko kwenye uhakika wa usalama wa maisha yake.

Yaani huyu ndugu yetu akili yake inashindwa kung'amua kuwa huyo dreva wake kwa namna moja au nyingine huenda alihusika katika shambulio hilo. Kwa maneno yake mwenyewe huyo dreva alisema alijua hao waliokuwa wanawafuatilia walikuwa na nia mbaya. Sasa yeye dreva badala ya kurudisha gari bungeni au polisi stesheni kwenye usalama, kalipeleka sehemu ile ambayo alijua usalama wake ni mdogo hasa muda huo wa saa 7 mchana.

Yeye akili yake inashindwa kujua kuwa serikali wala chama chake cha chadema haiwezi kusema kuwa itamuhakikishia usalama wake. Kwanza wala hasemi wamuhakikishie usalama wake kwa kufanya mambo gani? How?

Anyamaze aendelee kuwa mkimbizi wa siasa huko aliko na afuate sheria za kimataifa zinavyowataka namna ya kuishi huko kama political asylums. Vinginevyo mawakili zetu wamfungulie mashitaka kwenye mahakama ya nchi hizo.
 
Petro kwa wewe kuwa mwanasheria, sikutarajia hoja yako ikae kwa namna ulivyoiweka!!

Ni kweli kuwa serikali ina wajibu wa kumhakikishis kila raia usalama wake na mali zake LAKINI namna ya kulitekeleza jukumu hilo kwa raia au makundi ya raia hutofautiana kwa kutegemea hatari iliyopo kwa mhusika.

Hatari ikishapimwa, ndipo hujulikana nguvu na umakini kiasi gani uwekwe kwa yule ambaye yupo hatarini.

Petro, hujawahi kuona gari lililobeba pesa likisindikizwa na polisi wakati lorry lililobeba pamba likiwa na dereva na utingo tu, wakati malori yote yana mali zinazostahili kupewa ulinzi wa serikali?

Au Petro hujawahi kuona Rais akilindwa wakati wewe Mayala unahanja mitaani bila ulinzi wowote? Lakini ni sahihi kabisa kama kuna hatari iliyo dhahiri dhidi ya usalama wako, una haki ya kulindwa masaa 24. Jambo hili ni la kawaida sana kwa nchi kama Marekani. Ukiona maisha yako yapo hatarini, unatoa taarifa polisi halafu polisi wanakuoa ulinzi mara moja na kisha wanaanzisha uchunguzi ili kujiridhisha kama kweli kuna hatari iliyoripotiwa.
 
Raia wanapokuwa na hofu juu ya usalama wao ndani ya Taifa lao huru....kaa chini tafakari kwa kina.
Kati ya raia 55m, hao wenye hofu ya usalama wao ni % ngapi?! Wakati Lisu anatumiana sms za kuhujumu nchi na kina Mwanyika alikuwa anawakilisha % ngapi ya watanzania?!

Think twice brother!
 
Unajua mara nyingi huwa tunasema huyu ndugu yetu Tundu Lisu akili zake haziko sawa. Akili yake imekuwa ikiamini kuwa serikali ndiyo iliyomtandika hizo risasi. Amekuwa akiituhumu serikali ndani na nje ya nchi kwa kitendo hicho. Serikali imekuwa ikikanusha na kumtaka yeye na dreva wake warudi nyumbani ili washirikiane na jeshi la polisi kukamilisha uchunguzi wa shambulio hilo ili hatimaye waliomshambulia watiwe nguvuni.

Sasa yeye kwa akili yake anataka serikali imuhakikishie kuwa haitamtandika tena risasi zingine atakaporudi nchini! Yaani anataka serikali iseme kuwa haitamshambulia tena! Hivi kwa mtu mwenye akili za kawaida utaomba kweli ulindwe na mtu ambaye unaamini ndiyo mbaya wako?

Sehemu ambayo iko 100% kwa usalama wa maisha ya mtu ni lockup (selo) ya polisi au ya magereza. Kupewa walinzi/ body guards hakuwezi kukuhakikishia usalama wako hasa kama wewe unaishi vibaya na wenzako. Kama wewe unaishi kila kukicha ni kutukana na kudharau wenzako unajijengea mazingira hatarishi na huwezi kuwa salama. Kwa hiyo Lisu anaomba serikali imuweke lockup atakaporudi maana kule ndiko kwenye uhakika wa usalama wa maisha yake.

Yaani huyu ndugu yetu akili yake inashindwa kung'amua kuwa huyo dreva wake kwa namna moja au nyingine huenda alihusika katika shambulio hilo. Kwa maneno yake mwenyewe huyo dreva alisema alijua hao waliokuwa wanawafuatilia walikuwa na nia mbaya. Sasa yeye dreva badala ya kurudisha gari bungeni au polisi stesheni kwenye usalama, kalipeleka sehemu ile ambayo alijua usalama wake ni mdogo hasa muda huo wa saa 7 mchana.

Yeye akili yake inashindwa kujua kuwa serikali wala chama chake cha chadema haiwezi kusema kuwa itamuhakikishia usalama wake. Kwanza wala hasemi wamuhakikishie usalama wake kwa kufanya mambo gani? How?

Anyamaze aendelee kuwa mkimbizi wa siasa huko aliko na afuate sheria za kimataifa zinavyowataka namna ya kuishi huko kama political asylums. Vinginevyo mawakili zetu wamfungulie mashitaka kwenye mahakama ya nchi hizo.
Huyu tapeli aliwahi kuulizwa kuhusu maslahi ya wabunge kuwa juu sana kuliko hata wanataaluma tukuka kama hawa madaktari waliookoa maisha ya Ruwaichi. Jibu alilotoa ni kuwa ni haki kwa kuwa kabla ya ubunge alikuwa anatengeneza pesa ndefu kuliko anayopata akiwa bungeni.

Huyu mtu ana matatizo makubwa sana kichwani. Fukua aliyoandika kuhalalisha Lowasa kugombea urais kupiptia chadema.
 
Kati ya raia 55m, hao wenye hofu ya usalama wao ni % ngapi?! Wakati Lisu anatumiana sms za kuhujumu nchi na kina Mwanyika alikuwa anawakilisha % ngapi ya watanzania?!

Think twice brother!

..hivi katika suala la kulinda na kutetea rasilimali za nchi hii TL ndiye Mtanzania aliyestahili hukumu ya kifo, tena cha kikatili?

..hata tukikubaliana na tuhuma kuwa he exchanged txt message na watendaji wa Accacia, mbona serikali yenyewe ilikaa na kufanya nao mazungumzo? Mbona wamiliki wa Accacia ambao ni Barrick walikwenda mpaka Ikulu?

Gagnija dont be insensitive kiasi hicho. Kama TL alifanya makosa basi alipaswa kushtakiwa ktk mahakama zetu.

..It is totally unfair jinsi alivyoumizwa na serikali haichukui hatua zozote za maana. Hivi tunajenga jamii ya aina gani?
 
list ya wakimbizi wa hiari inaongezeka
~Mange Kimambi
~Evarist Chahali
~na sasa Tundu Lissu
 
..hivi katika suala la kulinda na kutetea rasilimali za nchi hii TL ndiye Mtanzania aliyestahili hukumu ya kifo, tena cha kikatili?

..hata tukikubaliana na tuhuma kuwa he exchanged txt message na watendaji wa Accacia, mbona serikali yenyewe ilikaa na kufanya nao mazungumzo? Mbona wamiliki wa Accacia ambao ni Barrick walikwenda mpaka Ikulu?

Gagnija dont be insensitive kiasi hicho. Kama TL alifanya makosa basi alipaswa kushtakiwa ktk mahakama zetu.

..It is totally unfair jinsi alivyoumizwa na serikali haichukui hatua zozote za maana. Hivi tunajenga jamii ya aina gani?
OK, Lisu alikaa nao na serikali nayo alikaa nao. Sasa tueleza seikali ilikaa nao kwa maslahi ya nani, na Lisu alikaa nao kwa maslahi ya nani.

JK, Una maslahi kwenye tope hili?!
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
Ni sahihi mkuu. Kwa ujumla wetu serikali inatulinda watanzania wote. Sijawahi kusikia Duniani kote mtu m1 m1 akithibitiwa na serikali kuwa atalindwa yy binafsi. Labda hii ianzie Tanzania na kwa.TUNDU
 
Sikujua kama Lissu ni mbinafsi na muongo kiasi hiki,yeye anaogopa kauli za Musiba halafu anataka ahakikishiwe ulinzi yeye ni nani ,wangapi wanapata matatizo na hawana hata pa kusemea?halafu alivyotangaza kuwa anarudi ,je alihakikishiwa ulinzi na nani,awe mkweli aseme tu ameudhika baada ya kuchomolewa ubunge,Lissu bila ubunge ni sawa na samaki kutoswa nchi kavu.Sasa hana kinga ya kubwatuka tena na hao wazungu wake sasa hawatamuona wa maana tena kwani hana hadhi yoyote ya kusema jambo likawa na uzito,wazungu wamemtumia kama ko....
 
Gagnija,

..madai ya txt messages hayajathibitishwa popote pale.

..vilevile kuna watu wanadai aliyekuwa akiwasiliana kwa txt na Deo Mwanyika ni mtu mwingine siyo TL.

..Je, txt hizo zimehujumu nchi yetu kuliko sheria mbovu zilizopitishwa na wabunge, pamoja na mikataba ya kinyonyaji iliyosainiwa na watendaji wa serikali?

..Alichotendewa TL siyo haki. Na sote tunapaswa kukemea, na kuwakataa waliotenda unyama ule.
 
No no no... Kwa wastaarabu kama China alichostahili Lisu ni kitanzi. Haiwezekani watu wanafanya juhudi za kuitoa nchi ilipokwama wewe unafanya juhudi isitoke.

Siku zote nimekuwa naamini kwamba Mungu alimponyesha Lisu ili apate fursa ya kutubu hujuma alizowafanyia watanzania. The ball is on his side.
 
..waliopitisha sheria mbaya za madini na gesi na waliosaini mikataba mibovu mbona wao hawajashambuliwa?

..how come mabeberu wenyewe wamiliki wa barrick walitinga mpaka ikulu na hakuna walichofanywa?

..lakini zaidi tuna sheria na mahakama na huko ndiko wanakopelekwa wakosaji wote.

NB.

..TL ndiye mtetezi wa rasilimali za nchi hii. Alianzia kutetea watu wa Rufiji delta, machimbo ya Bulyankulu, na maeneo mengine.
 
Back
Top Bottom