Wakili Mwale Anyimwa Dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakili Mwale Anyimwa Dhamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Aug 9, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hatimaye yule wakili maarufu jijini Arusha leo amepelekwa mahakani na kusomewa mashtaka kwa ilie kesi ya kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha ambacho mpaka sasa hivi upelelezi unaendelea ili kujua chanzo cha yeye kukutwa na fedha nyingi kwenye account yake binafsi. Akiwa mahakamani hapo alionekana kutokwa na machozi baada ya kunyimwa dhamana na pia mawakili wenzake walikua wanahangaika huku na huku ili kumsaidia lakini sheria ilichukua mkondo wake kwa kumnyima dhamana. Hatimaye naondoka kwenye viwanja vya mahakama kuu jijini Arusha alikua anasubiri usafiri wa kumpeka magereza.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lakini dhamana ni haki ya mtuhumiwa labda kuwe na pingamizi lenye hoja nzito kama sio kukomoana.
   
 3. N

  Ndoano Senior Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkubwa tufahamishane huyo wakili kapandishwa kizimbani kwa mashtaka gani?
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma mabandiko vizuri...
   
 5. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hakuna kitu kama hicho, huwezi kusomewa mashitaka ya kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha!
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu hata mimi nashangaa kwanini akose dhamana hii kesi naendelea kuifuatilia.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mkuu! Kweli la kuvunda halina ubani. Ojare hakuwepo? Kweli sheria ni msumeno na Mganga hajigangi.
   
 8. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanamtuhumu kufanya money laundering "Money laundering is the act of hiding the source and/or destination of illegally obtained funds".
   
 9. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  pole yake,.........
   
 10. S

  Sanchez Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama ni money Laundering, ni kesi kubwa sana.wanaweza wamhusisha na vikundi vya ugaidi.itabidi mawakili wake waumize vichwa sana kumchomoa.
  On matters of style swim with the current, On matters of principles stand like a rock" Thomas Jefferson
   
 11. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Kithuku
  10th October 2007 01:50 AM
  #1 [​IMG]  [​IMG] Mawakili Medium Mwale na Loom Ojare ni majambazi?

  Wanabodi, Naomba tujadili hii mada. Mawakili mabwana Medium Mwale na Loom Ojare ni maarufu sana mjini Arusha hasa katika kutetea majambazi mahakamani, tena wana ujasiri wa kutosha sana wa kuwatetea majambazi wanaokamatwa kwenye tukio. Hawa ndio waliosimamia rufaa ya Bw Nyari hadi akafutiwa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kufuatia kupatikana na hatia ya ujambazi wa kutumia silaha.

  Hawa hawa Ojare na Mwale ndio wanaowatetea wale majambazi wawili waliopambana na polisi kwa masaa 6 katika nyumba ya Bw Chonjo kule Njiro walikokuwa wamejificha baada ya kupora na kuua kwenye benki ya NMB Mwanga. Hawa pia wamewatetea majambazi waliopora sh bil 4 NBC Moshi mwaka 2004. Na katika tukio moja mtuhumiwa mmoja wa ujambazi sugu aliyekuwa anatafutwa na polisi aliwahi kukamatwa akiwa nyumbani kwa mmoja wa mawakili hawa, wakili alipobanwa na polisi akadai ni mpangaji wake.

  Na zipo kesi nyingine nyingi tu za watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha katika mahakama kuu kanda ya Moshi na katika mahakama za hakimu Mkazi Moshi na Arusha ambazo mawakili hawa wanasimamia. Ukisikia kuna tukio la ujambazi wa kutumia silaha na majambazi wamekamatwa Moshi au Arusha, kama ni majambazi sugu wale wanaofahamika hata na wenyeji, fuatilia utasikia pia kuwa mawakili wao ni Loom Ojare na Medium Mwale.

  Ukisikia benki imevamiwa Moshi na kuporwa mabilioni, fuatilia nani wakili wa watuhumiwa mara wakamatwapo; Loom Ojare na Medium Mwale. Sijui kama wana kesi nyingine za wasiotuhumiwa ujambazi. Je kuna uhusiano wowote (zaidi ya umahiri katika sheria) kati ya mawakili hawa na majambazi wauaji? Je hawa jamaa nao pia ni majambazi au washirika wao?

  Hebu naomba tujadili hii mada maana kuna watu wameshaanza kupoteza imani si tu na mawakili hawa, bali pia na mfumo wetu wa sheria kwa ujumla. Naelewa katika nchi zilizoendelea kuna mawakili ambao wamejikita katika aina fulani za kesi na kuwa mahiri na wa kutumainiwa kwa mfano katika kesi za murder, fraud, divorce, blasphemy, n.k, ambapo yeyote mwenye kesi ya namna hiyo huwafuata mawakili hao. Je ni hivyo kwa hawa Mwale na Ojare au kuna zaidi?

  Nafahamu pia huu usemi: "A bright lawyer knows the law (might be LL.B Hons first class) but a smart lawyer knows the judge" (might have passed his law degree very poorly and by sheer luck, but wins cases by all means!) Hawa jamaa wako upande upi hapa?

  Naomba tujadili, mwenye ushahidi wowote hata wa kimazingira atuwekee hapa. Asanteni.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/6108-mawakili-medium-mwale-na-loom-ojare-ni-majambazi.html
   
 12. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Wakili "maarufu" Medium Mwalle asomewa mashitaka

  09/08/2011
  Wakili Maarufu jijini Arusha Medium Mwalle amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashitaka 13 yanayodaiwa kumkabili likiwamo la kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye kaunti zake zisizo na maelezo sahihi (Money Laundering).

  Mwale alisomewa mashitaka hayo 13 jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magessa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali aliyejulikana kwa jina moja la Mallya.

  Mara baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo Hakimu Magessa alitupilia mbali hoja za upande wa Mashitaka akidai maelezo katika hati hiyo hayakueleza wazi. Akisoma uamuzi mdogo baada ya kuahirisha kwa muda kesi hiyo, Magessa alidai, hundi zinazodaiwa kutumika kutoa na kuingiza fedha kwenye akaunti za mtuhumiwa hazikuelezwa zimetoka wapi na kwa nani, "Hati ya Mashitaka inatakiwa ieleze au itoe maelezo mafupi kulingana na mashitaka na vipengele husika. Kama haitafanyika hivyo ni wazi mwisho wa siku nguvu ya Mahakama hupotea bure," alidai Magessa na kuongeza, "Lakini sheria inasema lazima hati ya mashitaka iwataje au imtaje mtu ili ajulikane ni nani. Hatua hii inasaidia mlalamikaji kujua nani anayemlalamikia."

  Alidai kutokana na hatua hiyo Hakimu Magessa alidai, kwamba Mahakama yake haitayapokea mashitaka hayo kuanzia la tatu hadi la 11 kutokana na makosa yalijitokeza, "Mashitaka haya kuwa ni makubwa, hivyo napendekeza yarudishwe yaandaliwe upya ili kusiwapo na mashaka kwenye hatui mpya itakayoletwa siku yoyote skutoka upande wa Serikali. "Sasa basi haitakuwa busara kuendelea na mashitaka ya haya hivyo naamuru mashitaka ya kwanza hadi la pili nayo yarudishwe yaje pamoja. Mtuhumiwa arudishwe mikononi mwa polisi kwani wao ndio wanataratibu za kumshikilia," alidai Magessa.

  Mwalle moja ya Mawakili waliojijengea umaarufu mkubwa anadaiwa kukamatwa Agosti 2, 2011 na polisi wa kimataifa wa Interpol, ambapo hadi jana tayari alikuwa amefikisha wiki moja akiwa anashikiliwa na polisi.

  Aidha, hati ya mashitaka haikuweza kupatika kwa ajili ya kuandika kwa usahihi mashitaka hayo 13 kutokana na madai kwamba kulihitajika marekebisho.

  Nje ya Mahakama

  Hali ya hewa ilionekana kuwa nzito zaidi kwa baadhi ya mawakili waliokuwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kujua hatima ya wakili mwenzao. Baada ya kutoka nje ya jengo la mahakama, wakili huyo alishindwa kuficha sura yake baada ya kukutana na kamera ya televisheni moja hapa nchini. Hatua hiyo ilimfanya Mwalle kuomba mpiga picha asiendelee kupiga picha kwa madai kuwa "atamharibia". Alilazimika kusimama kwa kuipa mgongo camera huku akiwa amezungukwa na maofisa wa polisi na usalama wa Taifa. Mara baada ya kuona wanacheleweshwa maofisa hao walimwamuru kuanza kutembea licha ya kamera hiyo kummulika.
  source: Wavuti - Habari
   
Loading...