Wakili Maneno Mbunda atoweka siku ya 7 sasa

Wakili Maneno Mbunda atoweka siku ya 7 sasa

Username yake humu jf ni ipi?
!
!
!

Tuanzie hapo kwanza
 
Amekamatwa na maaskari,alafu vituo vya polisi hayupo!
Hapa tulipofikia ni pabaya sana,tunautengeneza ugaidi ambao baadaye tutashindwa kuudhibiti.Mungu tunusuru.
 
Wakili akiwa na tamaa, unamtetea mteja wako, wanakuja waliomshitaki wanakupa kitu kidogo unaanza kumpoteza mteja wako, anakushtukia, wakati huo tayari ameshakueleza kila kitu, anapatwa na shaka na wewe, hapo ndio shida inapoanza.


Conflict of interest, very unethical
 
Ni mkakati wa kutengeneza Taifa la watu waoga, wasio hoji jambo lolote kwa maandalizi ya utawala wa kifalme.
 
nimeona mwananchi online wanasema DPP anaseama wanamshikilia kwa kosa la uhujumu uchumi na wenzake....swali ni je kwanini wamkamate kwenye mazingira ya utekaji tekaji?
 
"Atakuwa ameenda kutafuta maisha" Alisikika Nchemba akisema.
 
3 May 2019
UTATA' WAKILI MWINGINE ATOWEKA, MDOGO WAKE AMWAGA CHOZI
Matandao wa THRDC waomba serikali kufuatilia watu wanaopotea
Wakili Maneno Mbuda ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Arusha National Park,taarifa za kutoweka zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na 2/5/2019 ndipo mdogo wake kwa jina la Upendo Mbunda alitoa taarifa za kutoweka kwa kaka yake kwenye ofisi za Mtandao(THRDC)kwa ajili ya usaidizi wao .

THRDC wakinukuu Takwimu alizotoa Kangi Lugola waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi Tanzania zinasema zaidi ya watu 100 wameripotiwa kupotea kati hali ya utata. Mtandao wa Haki za Binadamu unaomba serikali izidishe juhudi ili watu waliopotea wapatikane .

Source : Muungwana TV
 
View attachment 1087588

Taarifa za kutoweka kwa Mbunda, ambaye pia ni Mwanasheria wa Hifadhi ya Wanyama Arusha, zilitolewa Aprili 28 mwaka huu zinashangaza wengi na kuomba suala hilo lichukuliwe kwa uzito ili wakili huyo apatikane.

Olengurumwa amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Wakili huyo, magari yaliyotumika kumkamatia hayakuwa na namba za gari na alikamatwa eneo la USA River jijini Arusha, na hajulikani alipo hadi sasa.

“Matukio ya kupotea kwa watu na mawakili na watetezi wengine wa haki za binadamu yamekuwa yakiongezeka hapa nchini na hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa na hata kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Ikumbukwe kwamba ni takribani miaka minne sasa tangu wakili wa kujitegemea, Philibert Gwagilo, alipopotea na hadi sasa hajulikani alipo, matukio haya ya kupotea kwa watu yanapojitokeza ni lazima hatua za haraka za kiuchunguzi zichukuliwe ili kusaidia upatikanaji wake,” amesema.

Naye dada wa Wakili Mbunda, aliyejitambulisha kwa jina la Upendo, huku akibubujikwa na machozi amesema kaka yake alipotea tangu Aprili 28 mwaka huu, ma kwa mujibu wa maelezo ya rafiki yake aliyekuja kutoa taarifa nyumbani kwao alidai kuwa alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maaskari.

Upendo amesema tangu tarehe hiyo mpaka leo kaka yake hajaonekana wala hawajafanikiwa kumpata katika kituo chochote cha polisi hapa nchini jambo ambalo anadai limewashtua na linaendelea kuwatia hofu kwakuwa hawana baba wala mama na walikuwa wakimtegemea yeye katika familia yao.

Hata hivyo namba ya Kamanda Polisi, Mkoa wa Arusha, ilipopigwa ili kuelezea tukio hilo kama wanalifahamu simu ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake na kusema atamuelezea mkuu wake kuhusu suala hilo.
Tutapotea sana awamu hii na wakuu wenyewe wanasema kupotea ni hiyari😭😭
 
Back
Top Bottom