Nadhani ni ule msemo wa waswahili kuwa "Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa".Hivi hao Wazungu mnojifanya hamna ushirika nao na mnawatukana,si ndio wanaofadhili mfuko wa "Benjamin Mkapa Foundation" na juzi huko Chato walizindua nyumba za wahudumu wa afya?
Si ndio hao mmewaomba toka Instanbul wawajengee reli ya SG toka Dsm mpaka Moro,mkawakopa hadharani kwenye TV huku mkionekana?Ndio hao nyie mnawaita "Washirika wa Maendeleo" ili kupoza maana ya neno "Wafadhili?"
Hao ndio wanachangia 60% ya bajeti ya viwanda ya 2017/2018...Kama mmethibitisha "anatumika" na wazungu,kwanini msimshtaki haraka iwezekanavyo!?
Mwenzenu kila sentensi anayotamka anajua ina madhara gani kisheria.Mtaishia kumuweka mahabusu kwa amri kutoka juu,lakini hamuwezi kumfunga kwa kutumia vifungu vya sheria.
Mnampa umaarufu wa bure...Mpaka mtaani watoto wakiwa wanashindana kwenye michezo,mmoja akisema "Mi Magufuli" mwingine anasema "Mimi Tundu Lissu"...Aliyesema Magufuli,anasema basi mi sichezi.