Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Wakili ataka Mtendaji wa Kobil kufungwa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th December 2010 @ 23:50
WAKILI Jerome Msemwa amefungua hati ya dharura Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kobil Tanzania Ltd, Fabrice Ezaovi akiomba atupwe jela kwa kuidharau mahakama.
Kwa mujibu wa hati hiyo, Msemwa ambaye ni wakili wa mashtaka anayemwakilisha Samuel Michael ambaye ni muuza mafuta aina ya dizeli na petroli katika kituo hicho cha Kobil kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam, imeeleza kwamba Michael anazo taarifa zilizo sahihi
kuwa Ezaovi ana mpango wa kuondoka nchini kabla kesi ya msingi haijamalizika.
Katika kesi hiyo ya msingi Michael analalamika kuvunjwa kwa mkataba walioingia kwa pamoja unaomruhusu Michael kufanya biashara katika kituo hicho.
Kutokana na hilo, aliomba mahakama hiyo iliyokuwa imeketi chini ya Jaji Alice Chingwile kusikiliza hati hiyo ya dharura mapema iwezekanavyo ili mteja wake kupata haki yake kabla mlalamikiwa hajaondoka nchini.
Hati hiyo, ameeleza kuwa kwa nyakati tofauti ambazo kesi hiyo ilikuja kusikilizwa, mlalamikiwa alishindwa kufika mahakamani bila taarifa yoyote jambo linaloashiria kudharau mahakama na kuzuia haki kutendeka.
Katika kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo, Michael aliingia kwenye mkataba na Mkurugenzi huyo akimruhusu kuuza mafuta katika kituo hicho cha Kobil.
Hata hivyo, bila sababu ya msingi kabla muda wa mkataba haujamalizika, mlalamikiwa alivunja mkataba huo isivyo halali na kuingilia biashara ya malalamikaji kinyume cha matakwa ya mkataba wao.
Kesi ya msingi itasikilizwa tena Machi 7, mwakani