Freedom tommorrow
JF-Expert Member
- Jan 31, 2015
- 1,795
- 1,132
Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa Wakenya zaidi ya 280 wameingia Loliondo pamoja na Serengeti na kuishi kinyume na sheria.
Baadhi yao wamediriki hata kupewa uanachama wa CCM na kupewa uongozi mbalimbali wa chama hicho. Mkuu wa Wilaya amekiri kuwepo kwa wahamiaji haramu hao.
Mpaka sasa ni 17 tu ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Majina yote jamhuri wameyaweka ili kuvisaidia vyombo vya usalama kuwashughulikia.
Maoni yangu ni kuwa hili suala ni nyeti sana hasa wakenya sio majirani wazuri kama tunavyowafikiri.
Kwao hawawezi kukuruhusu hata kupata eneo la biashara kirahisirahisi, waulize Watanzania wanaoishi mipakani watawapa majibu.
Hivyo viongozi husika walichukulie serious ili jambo waache virushwarushwa. waanze kuwashughulikia kama ile operation kimbunga.