Wakenya walitupora lugha yetu kwenye mtandao..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakenya walitupora lugha yetu kwenye mtandao..!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Leonard Robert, Apr 13, 2012.

 1. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Yamesemwa ndani ya kongamano linalofanyika chuo kikuu cha Dar es salaam..
  Mtoa mada mzee abdulatiful abdala kutoka kenya..alisema eti Kenya sasa imefika mbali kuliko Tanzania katika nyanja za lugha ya kiswahili..
  Akikanusha hoja hiyo kutoka meza kuu,alisema eti kenya bado hawajatufikia katika kukiendeleza kiswahili bali wao wamejitangaza kuliko sisi..
  Amesema kujitangaza kenya ni tabia yao,katoa mfano kenya imewai kujitangaza kwamba mlima kilimanjaro huko kwao wakati si kweli..amesema wao kusema mlima huko kwao haimanishi hauko Tanzania..

  Amesema hata kiswahili kinachotumika kwenye internet/mtandao..kimetungwa Tanzania lakini wakenya walipata tenda na kukitumia hicho kiswahili chetu..

  {lakini hakutueleza nivipi au ilikuaje wakenya wakapata tenda na kuchukua kiswahili hicho kutoka Tanzania}
  naomba mtu mwenye uelewa mzuri wa haya maswala atuleze tuelewe kama wakenye wametuweza kuanzia mlima kilimanjaro hadi lugha ya kiswahili..nawasilisha.
   
 2. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Mwenye uelewa atu dadavulie..karibuni wadau..
   
 3. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,841
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nchi hii itaibiwa kila rasilimali yake iliyojaaliwa na Mwenyeezi Mungu hadi siku mtakapoacha kuwachagua mafisadi wala nchi.
   
 4. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  inawezekana, lakini ni n gumu kuthibitisha kwa 7bu hata hicho kiswahili chenyewe cha kwenye mtandao sio fanisi, sidhani kama kimetungwa tanzania
   
 5. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  kwakweli hili la kutuibia lugha limenistua kidogo..
   
 6. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  kama si fanisi,mbona hawa jamaa wa kiswahili wanaking'ang'ani eti ni chao kilitungwa Tanzania..
   
 7. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Wazee wa lugha hii ya kiswahili mko wapi,mtuambie kilichotokea hadi wakenya wakatuibia lugha yetu..
  Na kwanini tulikubali kuwapa wao wakauze sisi tusifaidike na chochote..
   
 8. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  ^^^Lugha haina hati miliki ndio maana hatujafaidi. Anyway big up mzee wa sauti ya dhiki.
   
 9. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  sasa kama hakuna hati miliki waliwezaje kuiuza lugha kwenye mtandao kwa tenda mkuu?
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Eti ni Tanzania pekee yenye kamusi ya kiswahili online,hii ni kweli? Maana tumeshindwa mambo madogo tutaweza hilo kweli..
   
 11. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Wakenya hawakutuibia Kiswahili kwani kimekuwa kikizungumzwa huko tangu awali. Tofauti na Tanzania, Wakenya wengi walikuwa hawajui kuongea Kiswahili vizuri au walikuwa hawakijui kabisa. Hata hivyo, kumekuwa na mwamko mkubwa sana nchini humo wa kuongea Kiswahili siku hizi za karibuni. Lwa mawazo yangu, nadhani bidii za makusudi zimefanywa kukuza Kiswahili ili kuleta umoja wa kitaifa baada ya zile vurumai za kikabila zilizosababisha mauaji ya watu wengi.

  Tukirudi hapa kwetu Tanzania, Kiswahili kinaendelea kulegalega. Wakati kuna wakati tulikuwa tunajivuia kwa matumizi bora ya Kiswahili na kuonekana kama 'wadhamini' wa lugha hiyo, haki hiyo hatuna tena. Kwa maoni yangu ninaweza kueleza sababu mbalimbali mabazo zimefanya matumizi na ubora wa lugha ya Kiswahili kuporomoka Tanzania.

  Kwanza kabisa, Watanzania wengi wana dhana kuwa ukiongea Kiswahli bila kuchanganya na Kiingereza kidogo, unaonekana hukusoma, au wewe sio mtu wa 'ki-leo'. Dhana hii haipo tu kwa vijana bali hata kwa watu wazima. Ninashangazwa sana kuona hata wanasiasa wakubwa, ambao wangepaswa kuwa mifano ya kuigwa, wanafanya hivyo wakati wanapotoa hotuba mbalimbali. Jambo hili lipo kila mahali, pia hata katika bunge letu. Cha kusikitisha zaidi hapa ni kwamba wengi wa hao wanaochanganya lugha hizi hawazijui zote vizuri. Ukimwambia mtu aongee Kiingereza kitupu ataongea Kiingereza kilichojaa makosa mengi mbalimbali, vilevile kwa lugha ya Kiswahili.

  Mfano wangu wa mwisho hapo juu utanifanya niongelee sababu ya pili ya kushuka kwa Kiswahili Tanzania. Kushuka kwa ubora wa elimu kumefanya hata lugha ya Kiswahili kutofundishwa vizuri mashuleni na vyuoni. Nashangazwa sana na makosa mengi ya kisarufi yanayofanyika katika uandishi (hasa humu jamvini) na magazetini. Uandishi mbovu wa Kiswahili katika magazeti yetu unaonyesha hali ya kutoijua vizuri lugha au/na uzembe wa wahariri katka kuhariri kazi zinazoandikwa na waandishi kabla ya kuchapishwa.

  Serikali haina nia ya kukuza Kiswahili. Nahisi labda ni katika utandawazi ambapo kila kitu kimeachwa holela. Siku zilizopita juhudu makusudi ziliwekwa kukuza Kiswahili katika jamii. Nakumbuka kulikuwa na kipindi cha radio ambapo misemo tata mbalimbali ya Kiswahili ilikuwa inajadiliwa na wataalam kama Mzee Kibao, Mayoka n.k.

  Lugha ya Kiswahili kilitupa Watanzania utambulisho wa kufahamika duniani nzima. Siku hizi sio hivyo, kweli jirani zetu Kenya wanatupita kwa Kiswahili, na wanafanya hivyo kwa vile wanajua wanafanya nini. Watanzania tuamke, tutambue kile kilichokuwa kinatufanya 'taifa kubwa' na tukichukue tena kwa sababu ni chetu!
   
 12. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135  Entrepreneurship of adversity!

  Nadhani Kiswahili chake ni "biashara za ujanja-ujanja" hivi.
  Zina mwisho wake, lakini kabla ya huo mwisho tapeli atapata!
  Unakwenda kwa Mhindi, unaulizia spea. Spea hiyo mhindi huyo hana.
  Anasema ngoja niangalie stoo. Anaenda uani.
  Kule uani anamtuma Juma akachukue duka jirani. Juma analeta hiyo spea
  ikiwa imeongezewa "cha juu."

  Ukirudi kununua palepale mara ya pili kwa bei ile ya mwanzo, stori hii inakuwa na wajinga wawili:
  Mjinga wa kwanza mnunuzi asiyetembea kuangalia bei zimekaaje kwenye maduka mengine.
  Mjinga wa pili anakuwa huyu tajiri mwenye spea nyingi ambaye hajitangazi ajulikane yupo na bei zake poa.

  Now the moral of the story: Tujitangaze badala ya kulalamika-lalamika kila wakati: hooo, mara wameiba wimbo
  wetu wa malaika, hoo mara wameiba kilimanjaro; hooo mara wametuibia kiswahili chetu.
  Jamaa ee, hivi kuna siku Mwingereza alishawahi kulalamika Mwamerika kaimba kiingereza chake?

  Mi naona kama hii hoja ina mtego wa kutufanya Watanzania tuonekane wajinga.
  Wizi wa lugha? Mi naona ujanja-ujanja tu hapa. Sioni wizi.
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hii ni CNN...Nairobi!!!
   
 14. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Naomba link ya lugha ya kiswahili online
   
 15. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kama ni wizi, basi sisi ndiyo wezi wa kiswahili. Historia inasema wazi kiswahili kilianza kuzungumzwa kwa mara ya kwanza Kenya (maeneo ya Lamu).
   
 16. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  1-TUPE USHAHIDI WA KAULI YAKO
  2- AU NDO HISTORIA WANAYOTUFUNDISHA WAZUNGU ?
  KISWAHILI KILIZALIWA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI NA BAADAE KUTAPAKAA BARA.
  KUANZIA BARAWA -SOMALIA MPAKA SOFALA - MSUMBIJI.HAYA NDIO MAENEO YA AWALI .
  Wajuzi tujuzeni.
   
 17. K

  KIOCH New Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni upumbavu ulotujaa. wakati vyuoni kila mtu anataka azungumze lugha za kigeni ili atambulike msoni. hiyo tovuti ya kiswahili ndo ipi mbona tunadanganyana hapa. wakenya wanafanya sisi tunatunga sera. kwa ninavyojuwa wakenya ndo walimu wakiswahili katika vyuo vingi duniani ukilinganisha na watanzania na wana tovuti nyingi mfano paneli ya kiswahili ambayo hata walimu wakitanzania wanaitumia kujifunza na kufundishia. aibuuuuu
   
Loading...