mkuu unajua gharama ya kudesign kifaa kimoja? ni mabilioni ya hela,
ndio vifaa vya ndani wananunua toka makampuni mengine lakini usifikiri ukiwa na vifaa hapo hapo unakuwa designer mzuri wa laptop, inahitaji ma engineeer wenye uwezo mkubwa kudeliver product nzuri.
mfano tuchukulie laptop zinazoaminika an makampuni mengi duniani yaani thinkpad za lenovo (zamani ibm)
ukiwa na thinkpad ukifanya benchmark ya cpu utaona upo above average, siku zote yako itazidi kidogo perfomance sababu ya cooling nzuri na design ya uhakika, kwa kutumia same battery laptop yako itakaa na chaji kuliko laptop nyengine yenye same specs etc
kampuni ndogo kama hizo Taifa, chuwi, honda, Tecno na wengine wanaotengeneza vifaa vya windows kama hao wanatumia ready made design, kina intel wamehangaika wakatumia mabilioni ya research na kutoa design fulani kwa ajili ya vikampuni vidogo kutumia, sifahamu Taifa katumia design ipi ila najua design kadhaa za namna hii
mfano angalia hii design ya baytrail/braswell/apollo lake
unapewa motherboard ambayo ina cpu imeshagandishwa, nyengine ram zimegandishwa au unaeka mwenyewe, nyengine storage za kugandishwa au unaeka mwenyewe. hapo unavisha kasha na kueka tu power supply, na sababu hizo low powered cpu unaweza tumia chaja ya simu au tablet yenye amps kubwa.
lakini leo kanunue desktop au laptop ya dell ndani utakuta katumia motherboard yake mwenyewe, muulize mtu anaeunda desktop yake mwenyewe akupe story ya motherboard za hp na dell na ugumu wa power supply na vitu kama hivyo. wangekuwa hawajadesign wao tungevipata kirahisi ila sababu wamedesign wao ndio maana ni kazi ngumu kuvipata.
kuhitimisha mkuu
-kina dell, hp, lenovo etc wapo level yao vifaa vyao wanadesign wenyewe na ni vizuri (kwenye laptop na compact device nyengine)
-haya makampuni madogo hawadesign wao wanategemea kununua design ambazo zimetengenezwa na kupachika tu na quality zao hazilingani na wa juu
-kila.mtu hata mimi na wewe tunaweza tengeneza pc zetu sio sanaa ngumu