PreGE2025 Wakenya (Martha Karua na wenzake) waliokuja Tanzania kushuhudia kesi ya Lissu warudishwa wakiwa uwanja wa ndege Dar

PreGE2025 Wakenya (Martha Karua na wenzake) waliokuja Tanzania kushuhudia kesi ya Lissu warudishwa wakiwa uwanja wa ndege Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tukisema CCM ni tatizo kuna wakina tatalila na lucas wanakuja kusema tanzania kuba uhuru wa makalio yao kupulimiwa nyuma
Tatizo liko wapi sasa?

Sisi tungeweza kwenda wakati ruto anaua Gen Zee wao?

Nadhani tutakua wapuuzi sana if we want Martha karua to come to the rescue while we have our own champions

We don’t need failures wa Kenya kuja kwetu

Angola did the same Kwa hata watanzania waliokwenda for similar purposes

International laws ziko clear, immigration wana rights za kukunyima entry

Je walikua wanakuja kikazi? Kutalii au kwenye harakati?
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
CCM hawajielewi wamebambika kesi hawataki watu wake wasikilize.
 
Nchini kwao kwenyewe hali sio nzuri , WAKATOE BORITI KWANZA KWENYE JICHO LAO , ndio waje kufatilia kibanzi
 
nipeleke EU basi

Sijajua huko EU kama bado wanataka kuoa. Kwa USA Trump hataki watu wapelekwe kule kuolewa. Anataka wanaume wabaki kama wanaume. Sijajua kwa nini unataka upelekwe EU mbona hata CCM mpo nyie na mnapata watu wa kuwaoa?
 
Angalia CCM walivyo wajinga, Wakati wanamzuia Martha Karua wakidhan ndo Sasa Kesi haitamulikwa kimataifa.

Wanasahau kua kesho Mabalozi na Wawakilishi wa balozi mbali mbali Duniani, watakuwepo, wataona na wataitangazia Dunia vilevile.


Hivi CCM huku hamna mwenye Akili kabisa kabisa???.
Aisee kuna mambo yanatutia aibu sana sijui tumefikaje huku na sijui tutaendelea mpaka wapi na haya mambo, sio mchezo
 
Karua alieleza kushangazwa na hatua hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni raia maarufu wa Kenya na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).​
Hapa nimecheka 😂 kwahy akiwa maarufu sisi tufanyeje
 
Waziri wa zamani wa Sheria nchini Kenya, Martha Karua, ameeleza masikitiko yake baada ya kuzuiwa kuingia nchini Tanzania akiwa na watetezi wengine wa haki za binadamu na mawakili wenzake, Lynn Ngugi na Gloria Kimani.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili asubuhi, Karua alisema kuwa pasipoti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwa msimamizi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na alizuiliwa kwa zaidi ya saa moja bila maelezo yoyote.

Karua alieleza kushangazwa na hatua hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni raia maarufu wa Kenya na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

"Nilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tatu asubuhi, ambapo maafisa wa uhamiaji walikabidhi pasipoti yangu kwa msimamizi. Tangu wakati huo nimekuwa nikisubiri kwa zaidi ya saa moja huku wakishauriana na wakuu wao. Ninasikitishwa na hali hii, kwani kama mwanachama wa EAC, haipaswi kuwepo vizuizi visivyoeleweka kuingia katika nchi mwanachama," alisema.

Karua pia alifafanua kuwa wenzake, Gloria Kimani na Lynn Ngugi, nao wanazuiliwa. Alisema wote walialikwa na Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki, kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Kenya, Faith Odhiambo, pamoja na Chama cha Wanasheria wa Uganda.

View attachment 3337923
KATIKA DIPLOMASIA SAFI, WANGEACHIWA TU. (WAVINJARI)
 
Tena ilotakiwa wazuiewe na kupata viboko 12

hivi ni kwa nini watanzagiza wanapenda sana kupiga? je, ulikuwa abused as child labda na wazazi au mlezi kwa kupigwa na sasa unaona ni kawaida kupiga wengine?
 
Kama Wana wa nchi wanatekwa na kupotezwa, kumzuia jirani kitu gani?
 
Back
Top Bottom