PreGE2025 Wakenya (Martha Karua na wenzake) waliokuja Tanzania kushuhudia kesi ya Lissu warudishwa wakiwa uwanja wa ndege Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
980
Reaction score
3,646

Waziri wa zamani wa Sheria nchini Kenya, Martha Karua, ameeleza masikitiko yake baada ya kuzuiwa kuingia nchini Tanzania akiwa na watetezi wengine wa haki za binadamu na mawakili wenzake, Lynn Ngugi na Gloria Kimani.
Ndio mana tunahitaji elimu sana.
Kasome kwamba mojawapo ya malengo ya uanzishwaji wa jumuiya za kikanda ikiwemo EAC au East African Community ni
Free movement of people and goods across the region,. Sasa kama haya mambo shuleni ulikariri tu Kwa ajili ya kujibia mtihani na ukaja kusimamiwa na darasa la Saba au form four wa uvccm ambaye AMEAMUA kuingiza siasa kwenye professionalism na ambaye hajui mikataba na makubaliano ya mikataifa na kikanda ambayo Tanzania ni signatory lazima utajibu hivi au utafanya kama walivyofanya!
The EAC Common Market Protocol

Signed: 20th November 2009
Came into force: 1st July 2010

This is a legally binding agreement between member states that aims to create a single market among the EAC countries.

Article 10: Free Movement of Persons

.”

Article 13: Free Movement of Workers

.”

Kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili asubuhi, Karua alisema kuwa pasipoti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwa msimamizi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na alizuiliwa kwa zaidi ya saa moja bila maelezo yoyote.

Karua alieleza kushangazwa na hatua hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni raia maarufu wa Kenya na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

"Nilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tatu asubuhi, ambapo maafisa wa uhamiaji walikabidhi pasipoti yangu kwa msimamizi. Tangu wakati huo nimekuwa nikisubiri kwa zaidi ya saa moja huku wakishauriana na wakuu wao. Ninasikitishwa na hali hii, kwani kama mwanachama wa EAC, haipaswi kuwepo vizuizi visivyoeleweka kuingia katika nchi mwanachama," alisema.

Karua pia alifafanua kuwa wenzake, Gloria Kimani na Lynn Ngugi, nao wanazuiliwa. Alisema wote walialikwa na Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki, kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Kenya, Faith Odhiambo, pamoja na Chama cha Wanasheria wa Uganda.

Karua.jpg

b8dbf21f-d13c-467e-9594-95f918c672d2.jpeg

3b31c396-42e3-4795-887a-eaf41f125bee.jpeg
IMG_4090.jpeg
 
Wakili Martha Karua na wenzake wamezuiwa kuingia Tanzania wakiwa uwanja wa ndege Dar bila kuwepo kwa sababu zozote.

Jambo hili siyo zuri kwani huenda kesho akawa kiongozi wa Kenya, je tutakuwa tunajenga jumuiya au kuibomoa?
 
Waziri wa zamani wa Sheria nchini Kenya, Martha Karua, ameeleza masikitiko yake baada ya kuzuiwa kuingia nchini Tanzania akiwa na watetezi wengine wa haki za binadamu na mawakili wenzake, Lynn Ngugi na Gloria Kimani.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili asubuhi, Karua alisema kuwa pasipoti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwa msimamizi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na alizuiliwa kwa zaidi ya saa moja bila maelezo yoyote.

Karua alieleza kushangazwa na hatua hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni raia maarufu wa Kenya na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

"Nilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tatu asubuhi, ambapo maafisa wa uhamiaji walikabidhi pasipoti yangu kwa msimamizi. Tangu wakati huo nimekuwa nikisubiri kwa zaidi ya saa moja huku wakishauriana na wakuu wao. Ninasikitishwa na hali hii, kwani kama mwanachama wa EAC, haipaswi kuwepo vizuizi visivyoeleweka kuingia katika nchi mwanachama," alisema.

Karua pia alifafanua kuwa wenzake, Gloria Kimani na Lynn Ngugi, nao wanazuiliwa. Alisema wote walialikwa na Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki, kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Kenya, Faith Odhiambo, pamoja na Chama cha Wanasheria wa Uganda.

Hili lilikuwa liko wazi sana, however kuna wengine tayari wako nchini, hawawezi zuia hao
 
Angalia CCM walivyo wajinga, Wakati wanamzuia Martha Karua wakidhan ndo Sasa Kesi haitamulikwa kimataifa.

Wanasahau kua kesho Mabalozi na Wawakilishi wa balozi mbali mbali Duniani, watakuwepo, wataona na wataitangazia Dunia vilevile.

Hivi CCM huku hamna mwenye Akili kabisa kabisa???.
 
Back
Top Bottom