wake kule visiwani wanaongoza kwa kudai talaka tatu!

Wanaume wa zanzibar wengi wao wavivu sana..ndio maana wanataka hata kijitenga ili waje watawaliwe tena wawe wanapata kila kitu bure...wanawake ndio wanajishughulisha mara kwa mara....

Sasa mwanaume hutimizi majukumu yako bado unaleta kisauti...bora mtu ajiombee talaka yake..ni haki yao wacha waitumie.

Buswelu, haki inapendwa lakini wajibu wa kugema na kugemwa huo naona huongelei kwa nini?
 
Last edited by a moderator:
hahaha RUTA najua ulipoona habari hii kama kweli la kwanza ulinifikiria mm leo nitampata wahida ..ata kama siishi zanzibar kwa muda huu ila let me tell u RUTA wewe ni EDUCATED MAN unadhani kitu kitatokeaje bila ya reason? kuna sababu ya wanawake kuchoka kuishi na wanaume zao ,s sababu ya umaskin no ,ila behaviour za wanaume ,znz kuwa na mabadiliko ya economic n ndoto ,ila wanawake wao ndio wana huge responsibility ya familia zao. utamkuta mama ana watoto 6 au zaid yy ndie anahangaika kwa kila kitu na hana kazi ya maana so unaona ndoa zitakuwaje apo kama si migogoro?

wahida.........ninafurahi kuwa umkweli nilikuwa nina wasiwasi utajaribu kutetea uozo wa hizi familia kubw na zisizo na mpangilio kwa kudai wanalinda mila na dini.............
 
Last edited by a moderator:
kwa zanzibar au kaskazini?
[MENTION]
Edward Teller[/MENTION] Zenji yote inanikumbusha na ule msemo usemao amaki mmoja akioza basi ujue wote wameoza....................hakuna cha north versus south hapo...................tatizo hili lipo kila mahali............
 
Mungi..............kama wanaumme anashindwa kuihudumia familia yake unafikliri hata mke mdogo atapenda kubakia khapo. Kama anaongeza wake na huku hata kipato hana na kufnaykazi hataki unatarajia mwisho wake utakuwaje vile?

Maana yake kuuliza ni kutaka kujua wanawake wanaoomba talaka kama ni wake wadogo nihamie zanzibar. nitakuwa nawabanjua wakiwa kwa waume zao ili kupunguza kasi ya kuomba talaka.
naamini wanaume walaku tupo kibao tunaweza kwenda kuishi kule kuokoa ndoa za wenzetu!
 
ruta unayoyasema ni kweli na kote huko mimi nimeshapita Mwera na Mwanakwerekwe, wanaojazana pale ni wakina mama.tatizo kubwa linalosababisha kuwepo kwa hayo madai ya talaka ni hali ya kimaisha kua duni na unakuta mwanamume ana watoto 6 halafu kima cha chini cha mshahara ni 90,000.. hapo lazima mwanamke hali lazima imshinde na ukizingatia wanawake wa kizenji ni wavivu hua hawataki hata kupika...
 
Last edited by a moderator:
Maana yake kuuliza ni kutaka kujua wanawake wanaoomba talaka kama ni wake wadogo nihamie zanzibar. nitakuwa nawabanjua wakiwa kwa waume zao ili kupunguza kasi ya kuomba talaka.
naamini wanaume walaku tupo kibao tunaweza kwenda kuishi kule kuokoa ndoa za wenzetu!

Mkuu, wanawake wa kizenji ni wavivu sna na hua wanaboa tabia za umbea na majungu na ni wachache sana kuwakuta wanapika wanapenda kununua vyakula magengeni. utaweza? hiyo hali?
 
Mkuu, wanawake wa kizenji ni wavivu sna na hua wanaboa tabia za umbea na majungu na ni wachache sana kuwakuta wanapika wanapenda kununua vyakula magengeni. utaweza? hiyo hali?

Mkuu kazi yangu siyo kununua nini wala nini. nitakuwa na shughuli moja tu ya kubanjua ili ndoa yake iwe salama!
 
huku bara pia ktk mahakama za mwanzo baraza la usuluhishi 80%ya kesi ni za kuomba talaka.Fanya utafiti utalijua hilo
 
mm ni born muslim .ila dini yangu ,inahimiza utuzwaji wa wanawake na heshima ya ndoa ,ila s unaajua binaadamu sisi tumeumbwa hatuwezi tukawa parfect ,
 
Nimeshangazwa na taarifa ya Kadhi Mkuu kule Zenji kuwa zaidi ya asilimia 70 ya kesi za talaka ni wake wakidai walimwe talaka tatu na waume zao baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanywasaji, kutelekezwa na kudhalilishwa na waume zao................katika makala hii ya habari leo isomekayo kama.............Utoaji talaka wakithiri Zanzibar inathibitisha ya kuwa ndoa zimeparanganyika sana kule visiwani kama huku bara kutokana na waume kushindwa kubeba majukumu yao........................hatujui kwa kiasi gani na hao wake wameshindwa kubeba majukumu yao hususani la utii kwa waumme zao hata kusababisha kujikuta wanapata mateso makubwa kwa kisa "wameolewa"....................

Labda kwa vile waume zao wanaruhusiwa kuwa na wake wengh wanashindwa kuhudumia pande nyingine!
 
sawabho...........hiyo ilkuwa zamani sana......siku hizi akikaa ndani atakula nini na wakumletea mapochopocho yuko wapi.........na ndiyo maana wanaona hawajaolewa kama walivyotegemea na ndiyo maana wanataka kuishia...........

Hapo nimekuelewa Mkuu, kumbe wanaingia kwenye ndoa wakiwa na matumaini ya kufanyiwa kila kitu kama walivyoona Mama zao wakifanyiwa enzi za nyuma, bila kufahamu kuwa maisha sasa hivi yamebadilika. Kama mume ni mfanyakazi, mshahara ni kidogo; na kama ni mvuvi mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha upungufu wa samaki; na idadi ya wavuvi imeongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
 
Maana yake kuuliza ni kutaka kujua wanawake wanaoomba talaka kama ni wake wadogo nihamie zanzibar. nitakuwa nawabanjua wakiwa kwa waume zao ili kupunguza kasi ya kuomba talaka.
naamini wanaume walaku tupo kibao tunaweza kwenda kuishi kule kuokoa ndoa za wenzetu!

Mungi.........................ninaimani unatania kwa sababu idadi yao unaijua? Na magonjwa je umeyaweka wapi kwenye hizo hesabu na wewe huna shughuli ya maana ya kuifanya?
 
Last edited by a moderator:
Hapo nimekuelewa Mkuu, kumbe wanaingia kwenye ndoa wakiwa na matumaini ya kufanyiwa kila kitu kama walivyoona Mama zao wakifanyiwa enzi za nyuma, bila kufahamu kuwa maisha sasa hivi yamebadilika. Kama mume ni mfanyakazi, mshahara ni kidogo; na kama ni mvuvi mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha upungufu wa samaki; na idadi ya wavuvi imeongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

sawabho uko sahihi kabisa na wanaumme pia walikuwa na matarajio kama hayo sasa wanapokwama kuwatimizia wake zao na malalamiko yakashamiri basi vipigo huwa vinawaandama na jitihada ya kutafuta mke mwingine au mabwana wengineo hujitokeza na mwishowe huw talaka tatu..............
 
Last edited by a moderator:
Mungi.........................ninaimani unatania kwa sababu idadi yao unaijua? Na magonjwa je umeyaweka wapi kwenye hizo hesabu na wewe huna shughuli ya maana ya kuifanya?

Mkuu mbona magonjwa yamesha expire siku nyingi? hakuna ugonjwa tena unatembea peku kama huna kichwa vile!
Idadi yao si sababu kwa sababu timu ya walaku ni kubwa. hapa nawakilisha tu!
 
sio avatar ni picha yangu

Duu!! Smile sina la kusema kwa kweli, ngoja niishie kutazama tuu, najuuta kujua kwamba hiyo ni picha yako harisi. Ni kama mpita njia kuona vinywaji baridi kwenye friji madukani huku jua kali likimpiga na hana pesa mifukoni.
 
Last edited by a moderator:
kwan ndoa azabu jaman? Kwann ulazmishwe kuish na mtu usiemtaka? Kwan ndoa si mkataba?
 
Edward Teller Zenji yote inanikumbusha na ule msemo usemao amaki mmoja akioza basi ujue wote wameoza....................hakuna cha north versus south hapo...................tatizo hili lipo kila mahali............
me naona hawa wazenj wamezidi-wanajitwisha mzigo wasioweza kuubeba
 
Lizzy haki yao kama ni kuachika na wajibu wao ni upi?..........................hakuna haki bila ya wajibu, you know that.......
Tunapozungumza HAKI NA WAJIBU tuliangalie suala hili katika hali ya mlalo (horizontally) na sio ya wima (vertically) kwa maana ya kuwa mmoja anatakiwa apewe haki mwengie hataki kutimiza wajibu.

Binafsi sipendelei sana NDoa za Mkeka, japo mimi Ni Muislamu, lakini watoto wa siku hizi wamezidi kufanya mambo yasiyofaa, mzazi anaona labda akimfanya vile huenda Binti atatulia, na pia ni katika kuondoa DHIMMA ya Mzazi kuepusha Zinaa. mkumbuke kuwa Zanzibar ni nchi ambayo wakaazi wake ni 95% waislamu na ni wazazi ambao wanaishi kwa misingi ya Dini yao! hivo wanaepusha Zinaa. tatizo kubwa linakuja kwa watoto wa kiume nia yao nadhani ni kufanya Zinaa akimshamchezea Binti akimbie. sasa Mzazi hakubali hili anaona bora amuozeshe! anaepuka Zinaa na pia huenda binti akatulia.
Kwa kiasi kikubwa ndoa za mkeka ni sababu ya talaka. Bila ya kufanya utafiti, nahisi asilimia kubwa ya ndoa za mkeka hazidumu (mawazo binafsi).

kule unakuta mtu ana wake 3,kazi anayofanya ni kuvua samaki-at local and primitive way,hawezi kukidhi mahitaji ya familia,na anatumia sheria za dini kuforce submission kutoka kwa wake zake-regardless huyo mr yupo right or wrong-so kwa wanawake wasiopenda kuonewa,lazima wakimbie kwa mtu kama huyu wakajilimie mwani
Uko sahihi Bro kwa kuzingatia hayo nilyoweka red isipokuwa hilo la mwisho "wanawake wasiopenda kuonewa" ambalo nahisi HAKUNA binadamu anayependa kuonewa. Lakini si suala la kipato kidogo tu linalovunja ndoa bali suala la unyanyasaji vileviel. Wengine hutumia kipato chao kama silaha ya kunyanyasa wake zao; na bado kuna wengine pamoja na kipato kikubwa, hawatimizi wajibu wao katika ndoa - hawaheshimu ndoa zao kwa uasherati na hawatoi dozi inayostahiki. Usishangae kuona ke wa tajiri anatembea na mtunza bustani.

Yaani kweli wanawake wa Zenj hawana shukrani !!!! Huko si ndio nasikia kuwa mwanamke kazi yake kukaa ndani tu na kujichora na hina; mwanaume aleta kila kitu ikiwa ni pamoja na kwanda marikiti ?
Haya mambo ya kusikia haya.....!!!

wake wakidai walimwe talaka tatu na waume zao baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanywasaji, kutelekezwa na kudhalilishwa na waume zao................katika makala hii ya habari leo isomekayo kama.............Utoaji talaka wakithiri Zanzibar inathibitisha ya kuwa ndoa zimeparanganyika sana kule visiwani kama huku bara kutokana na waume kushindwa kubeba majukumu yao........................hatujui kwa kiasi gani na hao wake wameshindwa kubeba majukumu yao hususani la utii kwa waumme zao hata kusababisha kujikuta wanapata mateso makubwa kwa kisa "wameolewa"....................
Ikiwa taarifa hii umeiwasilisha kama ilivyoandikwa, nahisi inajitosheleza wala haihitaji kutafuta mchawi wa pili. Taarifa inasema na kusisitiza..."wake wanadai talaka baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanywasaji, kutelekezwa na kudhalilishwa na waume zao.....ndoa zimeparanganyika sana kule visiwani kutokana na waume kushindwa kubeba majukumu yao....."
Sasa Ruta Mkuu, ikiwa mume ni mnyanyasaji, mtelekezaji, mdhalilishaji, anayeshindwa kubeba majukumu yake (kwa mujibu wa taarifa ya kadhi na kusisitizwa na maelezo yako), bado unahisi kuna haja ya kudai mke atakeleze majukumu yake? Tuseme hayo matendo ya mwanamme yanatokana na mwanamke kutotimiza wajibu wake?

Kama nlivyodokeza kule juu kuhusu haki na wajibu, hivi vitu vinakwenda sambamba kwa wakati mmoja, mwenye wajibu atekeleze kabla ya kudai haki, na kwa kadhia hii tunaona kuwa mwanamme ndiye kwa kupitia matendo kadhaa anakiuka wajibu wake. Bahati mbaya suala la ndoa linaangukia sana kwenye dini, utamaduni na mfumo ambapo yote matatu kwa bahati mbaya mwanamke/mke anakuwa "raia wa pili", wa kwanza akiwa mwanamme/mume.
 
Back
Top Bottom