Wakazi wa Mahenge neema imewashukia

Wakazi wa Mahenge neema imewashukia

Mwaka Jana nilitaka kwenda huko,Kuna jamaa wanaeneo huko Karibu na machimbo ya hao wafanyabiashara alikuwa wanataka partner awekeze vifaa vya kisasa. Mtu niliyemuunganisha nae akaogopa cost deal likafa.
Ukitaka kuwekeza kwenye mradi mkubwa ambao unajua utakuingizia faida usiogope gharama
 
Unachokisema huenda kina ukweli, niliwahi kwenda Mererani, Manyara wanakochimba Tanzanite, maisha ya pale wachimbaji wadogo na wamiliki wa migodi wanapotoka machimboni nje ya ukuta kwenye barabara kuu iendayo KIA hadi Arusha kuna eneo linaitwa getini hapo ni starehe mwanzo mwisho ni bia,nyama choma na biashara ya ukahaba unakuta magari ya gharama yakiwa yameegeshwa pub na grocery zilizopo eneo hilo watu ni kula bata. Nilionyeshwa wachimbaji waliowahi kushika pesa kiasi cha milioni mia nane lakini sasa hivi ni choka mbaya hawana hata mia wanaishi kwa kugongea mpaka sigara.Ukiuliza pesa yote wamefanyia nini jibu unalopata ni kula na starehe, wakiamini siku inayofuata wakienda mgodini watapata pesa zingine kumbe siku hazifanani.
Hawa ni maapolo huwa hawana malengo ya maisha pia uchimba kwa kubahatisha.
Ukiyajua madini ni rahisi kutoka.Siku hizi technology za kisasa za uchimbaji zipo tele uhitaji ramli kujua madini yalipo wala kificho kwenye uuzaji KILA kitu kipo wazi.
 
Hivi unajua kipindi cha awamu ya 4 kuna kesi ya mauwaji w madini kutoka mahenge,sasa madini mahenge yapo na yamegundulika toka kitaaaaaambo , na wanachimba toka kitaaaaambo, hakuna jipya hapo
Tangu enzi ya mkoloni yapo hadi kesho sio ya kuisha leo.
Mtoa mada leo ndo kaona mwezi.
 
Hawa ni maapolo huwa hawana malengo ya maisha pia uchimba kwa kubahatisha.
Ukiyajua madini ni rahisi kutoka.Siku hizi technology za kisasa za uchimbaji zipo tele uhitaji ramli kujua madini yalipo wala kificho kwenye uuzaji KILA kitu kipo wazi.
Naaam!
 
Ni mwishoni mwa mwaka jana nilipata mawasiliano ya jamaa yangu tuliyepotezana kwa takriban miaka mitano, nakumbuka mara ya mwisho kuonana naye ni 2016 baada ya mimi kurejea toka kwenye majukumu nje ya nchi, kiukweli kiuchumi alikuwa ameyumba nilimuuliza sasa jamaa yangu una mpango gani kujikwamua kimaisha?

Akanijibu rafiki yangu sina ramani yoyote ila ningepata kama M 1 ningejua nini cha kufanya, kwa vile nilisota nae sana mimi nikampa cash milioni moja alishukuru mara mbilimbili hakuamini. Tangu siku hiyo hatukuonana tena sababu mimi nilirudi kwenye kituo changu cha kazi na yeye aliendelea na mishe zake.

Hivi karibuni nilipata taarifa zake kutoka kwa ndugu yake kwamba ni mmiliki wa mgodi wa madini aina ya ruby huko Mahenge, baada ya kupata taarifa hizo na mawasiliano yake, nilimtafuta kwa njia ya simu alipopokea akauliza nani?

Nikamjibu mimi ni fulani loh! jamaa alifurahi sana sana, akanitamkia aisee rafiki yangu wewe ndio umenifanya niheshimike na kuonekana mtu, ile milioni moja ulionipa kwa kweli imebadilisha maisha yangu kabisa, uliponipa nikakimbilia Mahenge baada ya kusikia kuna madini ya ruby green na red.

Baada ya kufika kwenye eneo husika nilitulia kwa mwezi mzima nikisoma mazingira na kuona jinsi shughuli zinavyofanyika, baadae nilianza kwa kununua madini hayo kwa wachimbaji wadogo wadogo, na sasa hivi nimekuwa mmiliki wa mgodi na ninasafiri hadi Thailand na nchi zingine kupeka mzigo.

Namshukuru Mungu kwa kukugusa wewe na kunipa ile milioni moja ambayo imezaa mamilioni ya fedha.Tafadhali ukipata nafasi rafiki yangu nitembelee uje uone maendeleo niliyoyapata, na nakuandalia donge nono kwa sababu kama sio wewe mimi sijui ningekuwa katika hali gani. Ndio najipanga nikipata likizo nimtembelee mshkaji.
Mkuu Ile milioni moja ndio ilimfanya akae mahenge mwezi akisoma biashara na hiyo milioni ikatosha kupata mtaji wa kununua Ruby
 
Back
Top Bottom