Wakazi wa Mahenge neema imewashukia

Wakazi wa Mahenge neema imewashukia

godson njamakuya

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
170
Reaction score
193
Ni mwishoni mwa mwaka jana nilipata mawasiliano ya jamaa yangu tuliyepotezana kwa takriban miaka mitano, nakumbuka mara ya mwisho kuonana naye ni 2016 baada ya mimi kurejea toka kwenye majukumu nje ya nchi, kiukweli kiuchumi alikuwa ameyumba nilimuuliza sasa jamaa yangu una mpango gani kujikwamua kimaisha?

Akanijibu rafiki yangu sina ramani yoyote ila ningepata kama M 1 ningejua nini cha kufanya, kwa vile nilisota nae sana mimi nikampa cash milioni moja alishukuru mara mbilimbili hakuamini. Tangu siku hiyo hatukuonana tena sababu mimi nilirudi kwenye kituo changu cha kazi na yeye aliendelea na mishe zake.

Hivi karibuni nilipata taarifa zake kutoka kwa ndugu yake kwamba ni mmiliki wa mgodi wa madini aina ya ruby huko Mahenge, baada ya kupata taarifa hizo na mawasiliano yake, nilimtafuta kwa njia ya simu alipopokea akauliza nani?

Nikamjibu mimi ni fulani loh! jamaa alifurahi sana sana, akanitamkia aisee rafiki yangu wewe ndio umenifanya niheshimike na kuonekana mtu, ile milioni moja ulionipa kwa kweli imebadilisha maisha yangu kabisa, uliponipa nikakimbilia Mahenge baada ya kusikia kuna madini ya ruby green na red.

Baada ya kufika kwenye eneo husika nilitulia kwa mwezi mzima nikisoma mazingira na kuona jinsi shughuli zinavyofanyika, baadae nilianza kwa kununua madini hayo kwa wachimbaji wadogo wadogo, na sasa hivi nimekuwa mmiliki wa mgodi na ninasafiri hadi Thailand na nchi zingine kupeka mzigo.

Namshukuru Mungu kwa kukugusa wewe na kunipa ile milioni moja ambayo imezaa mamilioni ya fedha.Tafadhali ukipata nafasi rafiki yangu nitembelee uje uone maendeleo niliyoyapata, na nakuandalia donge nono kwa sababu kama sio wewe mimi sijui ningekuwa katika hali gani. Ndio najipanga nikipata likizo nimtembelee mshkaji.
 
Jamaa kama ni donge nono. Kama ile milioni imemfikisha mpaka kumiliki mgodi hapa mahenge. Mwambie akupe Nyumba, gari ya maana na fedha taslimu. Hata milioni 50 aweze kuspend kwako.
Najua wamiliki wa migodi nane hadi sasa hapa mahenge. Asilete utani.
 
Hivi unajua kipindi cha awamu ya 4 kuna kesi ya mauwaji w madini kutoka mahenge,sasa madini mahenge yapo na yamegundulika toka kitaaaaaambo , na wanachimba toka kitaaaaambo, hakuna jipya hapo
Mimi sijui chochote kuhusu huko wala sijawahi kufika, ndio nataka nikipata likizo nimtembelee jamaa yangu aliyeko huko
 
Jamaa kama ni donge nono. Kama ile milioni imemfikisha mpaka kumiliki mgodi hapa mahenge. Mwambie akupe Nyumba, gari ya maana na fedha taslimu. Hata milioni 50 aweze kuspend kwako.
Najua wamiliki wa migodi nane hadi sasa hapa mahenge. Asilete utani.
Duh! kirahisi rahisi namna hiyo, infact mimi sikumpa ili aje anirudishie. Nilimpa baada ya kuona changamoto za maisha alizokuwa anapitia.
 
Biashara ya madini ina mambo mengi bila kujiongeza kivingine utaishia kupata hela kula tu yawezekana jamaa kajiongeza.
Unachokisema huenda kina ukweli, niliwahi kwenda Mererani, Manyara wanakochimba Tanzanite, maisha ya pale wachimbaji wadogo na wamiliki wa migodi wanapotoka machimboni nje ya ukuta kwenye barabara kuu iendayo KIA hadi Arusha kuna eneo linaitwa getini hapo ni starehe mwanzo mwisho ni bia,nyama choma na biashara ya ukahaba unakuta magari ya gharama yakiwa yameegeshwa pub na grocery zilizopo eneo hilo watu ni kula bata. Nilionyeshwa wachimbaji waliowahi kushika pesa kiasi cha milioni mia nane lakini sasa hivi ni choka mbaya hawana hata mia wanaishi kwa kugongea mpaka sigara.Ukiuliza pesa yote wamefanyia nini jibu unalopata ni kula na starehe, wakiamini siku inayofuata wakienda mgodini watapata pesa zingine kumbe siku hazifanani.
 
Hivi unajua kipindi cha awamu ya 4 kuna kesi ya mauwaji w madini kutoka mahenge,sasa madini mahenge yapo na yamegundulika toka kitaaaaaambo , na wanachimba toka kitaaaaambo, hakuna jipya hapo
Wale wafanyabiashara Kuna Mmoja mwanae anaendelea Kule na uchimbaji madini na anapata mawe ya kutosha, Pia Mbunge wao Salim naye ni mfanyabiashara wa madini kitambo
 
Ok, basi inaelekea jamaa yangu alitumia opportunity vizuri.
Mwaka Jana nilitaka kwenda huko,Kuna jamaa wanaeneo huko Karibu na machimbo ya hao wafanyabiashara alikuwa wanataka partner awekeze vifaa vya kisasa. Mtu niliyemuunganisha nae akaogopa cost deal likafa.
 
Ni mwishoni mwa mwaka jana nilipata mawasiliano ya jamaa yangu tuliyepotezana kwa takriban miaka mitano, nakumbuka mara ya mwisho kuonana naye ni 2016 baada ya mimi kurejea toka kwenye majukumu nje ya nchi, kiukweli kiuchumi alikuwa ameyumba nilimuuliza sasa jamaa yangu una mpango gani kujikwamua kimaisha?

Akanijibu rafiki yangu sina ramani yoyote ila ningepata kama M 1 ningejua nini cha kufanya, kwa vile nilisota nae sana mimi nikampa cash milioni moja alishukuru mara mbilimbili hakuamini. Tangu siku hiyo hatukuonana tena sababu mimi nilirudi kwenye kituo changu cha kazi na yeye aliendelea na mishe zake.

Hivi karibuni nilipata taarifa zake kutoka kwa ndugu yake kwamba ni mmiliki wa mgodi wa madini aina ya ruby huko Mahenge, baada ya kupata taarifa hizo na mawasiliano yake, nilimtafuta kwa njia ya simu alipopokea akauliza nani?

Nikamjibu mimi ni fulani loh! jamaa alifurahi sana sana, akanitamkia aisee rafiki yangu wewe ndio umenifanya niheshimike na kuonekana mtu, ile milioni moja ulionipa kwa kweli imebadilisha maisha yangu kabisa, uliponipa nikakimbilia Mahenge baada ya kusikia kuna madini ya ruby green na red.

Baada ya kufika kwenye eneo husika nilitulia kwa mwezi mzima nikisoma mazingira na kuona jinsi shughuli zinavyofanyika, baadae nilianza kwa kununua madini hayo kwa wachimbaji wadogo wadogo, na sasa hivi nimekuwa mmiliki wa mgodi na ninasafiri hadi Thailand na nchi zingine kupeka mzigo.

Namshukuru Mungu kwa kukugusa wewe na kunipa ile milioni moja ambayo imezaa mamilioni ya fedha.Tafadhali ukipata nafasi rafiki yangu nitembelee uje uone maendeleo niliyoyapata, na nakuandalia donge nono kwa sababu kama sio wewe mimi sijui ningekuwa katika hali gani. Ndio najipanga nikipata likizo nimtembelee mshkaji.
Hongera kwa kumuinua mtz.
 
Back
Top Bottom