JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Wakazi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamelalamikia kugongwa mihuri kimiujiza katika maeneo ya mgongoni, huku wakielekeza tuhuma hizo kwa baadhi ya wazee wa kijiji cha Kilima hewa.
Wakazi hao wamelazimika kuitisha mkutano maalumu ili kujadili suala hilo ambapo wamesema, awali tatizo hilo liliripotiwa na wakazi wa kata jirani ya Lupingu wilayani humo na baada ya kupigiwa kelele, tatizo hilo lilikoma, lakini hivi sasa limehamia katika kijiji cha Kilima hewa, huku wakiwataka wazee wanaotuhumiwa kurudisha mhuri huo walipoutoa.
Bado wahusika wa matukio ya kugonga watu mihuri kimiujiza, hawajatajwa moja kwa moja, licha ya kwamba wanaohusishwa ni baadhi ya wazee waliosamehewa kufanya shughuli za maendeleo na serikali kutoka na umri wao.
Kiongozi wa wakazi wa kitongoji cha Kilima hewa, Isaya Mwailamula amemwambia Mwandishi wa Habari wa Star TV kuwa mkutano huo umeitishwa maalum kujadili malalamiko ya uwepo wa mihuri ya kimiujiza kwa wakazi wa eneo hilo, baada ya kupokea malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa watu
Chanzo: Star TV