wakati wa ujauzito,naombeni msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wakati wa ujauzito,naombeni msaada

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtende, Jan 3, 2012.

 1. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  jf dotors naombani msaada
  dada yangu alipata ijauzito lakini mimba ilipokua na wiki mbili ghafle alianza kupata period then alipoenda hospitali akaambiwa mimba imeharibika akasafishwa. baada ya muda alipata tena ujauzito pia hali kama ile ile ya mwanzo ikatokea mimba ikaharibika.baada ya kusafishwa alienda hospitali kufanya chekup na aliambiwa kwamba kizazi kipo sawa na hana tatizo lolote

  alienda kwenye hospitali nyingine akafanyiwa vipimo dokta akamwambia kwamba ana kifafa ha mimba ambacho kinasukuma mimba na kusababisha itoke

  sasa she is in onfusion haelewi afanye nini, kama kuna wataalamu humu naomba mnijuze haya mabo,au kama kuna mtu anamfahamu dokta yeyote ambaye ni bingwa wa mambo hayo please anijuze nitampataje, na je hili tatizo litatibikaje? nahitaji msaada wenu
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mh kuhusu kifafa cha mimba sijui, ila kuhusu sbb za mimba kutoka ziko nyingi sana, lbd nikuulize baada ya mimba ya kwanza kutoka alivyosafishwa alitumia dawa yoyote? Na je ilichukua mda gani kupata mimba ya 2 baada ya ile ya kwanza kutoka?
   
 3. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kifafa cha mimba mara nyingi huanza kujitokeza baada ya 1st trimester (mimba zaidi wiki 12), hivyo sidhani kama ndio sababu yake ya kutoka kwake kwa mimba. Ushauri ni kuwa aanze mapema kabisa (pale tu akikosa siku zake) antenatal clinic ambapo ataonana na madaktari bingwa wa kina mama afanyiwe uchunguzi na kupewa ushauri mapema kabisa
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Poleni kwa matatizo.

  Katika hayo uliyoelezea hapo sioni kabisa dalili yeyote ya kifafa cha mimba. Hicho si kifafa cha mimba. Pia kifafa cha mimba hakisukumi mimba na kusabibisha itoke. Huyo daktari (kama kweli aliambiwa na daktari) hajui kifafa cha mimba ni nini!

  Kama livyokuambia Futota hapo juu, Kifafa cha mimba mara nyimngi huanza baada ya miezi mi3 ya kwanza ya mimba (First Trimester), na huanza kwa presha ya damu kuwa juu (Pregnancy Induced Hypertension) ambayo inaweza kumbatana na miguu kuvimba kupita kiasi (mara nyingine mpaka uso uvimba asubuhi) na kutoa protini kwenye mkojo. Kwa kawaida kina mama wanaohudhuria kliniki ya wajawazito (ANC) huwa wanachekiwa hivi vitu vyote vitatu hivyo ni rahisi kugundua kuwa mama yuko kwenye risk ya kifafa cha mimba (Eclampsia).

  Tafadhali mwambie dada akafanyiwe uchunguzi na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake (Gynaecologist) kabla ya kupata mimba, na aanze ANC mapema pindi apatapo ujauzito.
   
 5. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  baada ya mimba ya kwanza kutoka na kusafishwa dokta alimpa ntibiotics za kuzuia infections na alipata mimba ya pili baada ya miezi mitatu
   
 6. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  asante sana kwa useful advice,hivi dikta mzuri ambaye ni bingwa wa mambo haya naweza kumpata wapi tafadhali nisaidieni maana tumezunguka kila dokta anatupa majibu tofauti so hatuelewi which is which
   
 7. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maelezo mazuri, naomba kuongezea machache, presha wakati wa ujauzito (pregnancy induced hypertension) hutokea baada ya wiki 20 na endapo mama atakuwa na presha kabla ya hapo hiyo huitwa chronic hypertension,na kuvimba miguu kwa sasa haitumiki kama kigezo cha kifafa cha mimba.
  Kama wachangiaji walivyosema ni vizuri kufanya uchunguzi kwa mabingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi kabla na baada ya kupata ujauzito.
   
 8. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  asante sana be blessed maana nilikua na wasiwasi sana
   
 9. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Damu ya Yesu ni dawa tosha! Kimbilia kwake kwan yy ndiye daktar bingwa wa mabingwa wote! Atafute wa2mish wa Mungu wamwekee mkono nae atapona au hata yy akiamin afunge na kuomba kwa ajil ya hlo.
   
 10. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe unatupeleka Samunge...Wengi wameangamia Loliondo kwa akili hizi!
   
 11. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180

  that totaly tue
   
Loading...