Wakati wa taharuki makinika na kila taarifa

Wakati wa taharuki makinika na kila taarifa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
372,753
Reaction score
863,651
Siku moja mmasai mmoja ambaye hakuwahi kuvaa chupi, alinunua moja na kuvaa huko huko mnadani alikoenda kufanya biashara yake ya kuuza ng'ombe. Baada ya hapo akala na kunywa kwa furaha na rafiki zake.

Ni wakati wa kurudi nyumbani akashikwa na haja kubwa hivyo akatafuta kichaka cha karibu na kushusha mzigo..kumaliza akaangalia mzigo wake alioshusha hauoni akatimua mbio kali sana mpaka kijijini na kusimulia watu.

Kila mtu aliongea lake kuanzia uchawi mpaka mizimu kuwa ndio walichukua kinyesi chake. Taharuki ilipomwisha akagundua kinyesi chake anacho makalioni kimemganda ndani ya chupi..kumbe wakati anajisaidia hakuvua chupi kwakuwa hayakuwa mazoea yake.

Taifa lolote linapopata taharuki ama sintofahamu yoyote ile basi kitengo huingilia kati tukio zima zima na kulichakachua ili kutoa nafasi taharuki ana sintofahamu husika kufanyiwa kazi bila bugudha.

Hapa kitengo lazima kipotoshe uhalisia, kichepushe mada, kitengeneze hadithi mpya, kitengeneze taharuki ama sintofahamu bandia ili wao wabaki njia kuu huku hadhira ikichepushwa machakani.

Hili si la kulaumu hata kidogo kwakuwa unapotokea mshindo sauti yake huenda mbali na taharuki huwa juu. Kinachoonekana ni vumbi nene na watu kukimbia huko na huko, hapo kila mtu huwaza lwake. Tathmini na kujua nini kilitokea hufanyika baada ya hali kutulia.

Ni katika kipindi hicho cha kukwepeshwa hadhira mambo huwekwa sawa
  • Magendo yaliyofanyika
  • Miamala ambayo haikupita njia kuu
  • Nyeti zilizofutikwa chini
  • Chenchi na salio kwenye kibubu
  • Wafaidikaji
  • Wapigaji
  • Wahuni
  • Madudu yaliyofanyika
Ni katika kipindi hiki hadhira ikiwa inaingizwa mikenge kwa nyepesi nyepesi za kila aina basi masahihisho na kuziba viraka vinavyowezekana kuziba hufanyika kwa haraka na kwa umakini mkubwa japo makosa hayakosekani daima.

Ni katika kipindi hicho cha taharuki na sintofahamu, kitengo huwaza na kupanga kabla ya wengine hakuna kulala ni mwendo wa kubadilishiwa santuri tu halafu tufani ikikoma wakiwa tayari wameshadhibiti mshindo. Kifuatacho ni KIMYA KIKUU SANA na sometimes cha KUOGOFYA!

Ni wakati hadhira inapozoea mshtuko wa kishindo ndio huja tangazo lililotazamiwa na wengi BABA FULANI NDIO KAZAA NA BINTI YAKE
 
"Ni wakati hadhira inapozoea mshtuko wa kishindo ndio huja tangazo lililotazamiwa na wengi BABA FULANI NDIO KAZAA NA BINTI YAKE"
 
Kwa maneno ya Mwalimu (rip) nchi huendeshwa kwa kufuata katiba. Nchi si shamba la mtu au la kikundi cha watu.

Katika katiba kila kitu ni wazi. Nini cha kufanya katika hatua zote. Kwamba baba kazaa na binti yake?

Huyo hatufai katika familia wala jamii. Kwamba labda binti ni under 18? Huyo miaka 30 inamhusu. Kwa hilo hakuna kuremba!

Halipo vumbi la kusubiri litulie wala kwa mshindo kutulia.

Tujifunze sana umuhimu wa kufuata, kuzingatia na kuheshimu katiba. Mengineyo haya ni kujilisha upepo tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
[emoji117]Nchi flani hivi ya kitofauti sana, idadi ya watu wake nayo si haba!

[emoji117]Sifa yake kuu ilikua upole, upendo na amani bila ukahaba!

[emoji117]Ghafla imekuwa nchi ya chuki, husda na kurushiana shaba

[emoji117]Mkatiko mkuu baina ya waume wake na wana

[emoji117] Na hatukujuana kwa makabila, rangu wala chama

[emoji117]tulipendana kwa kukosoana bilakutishana na kutolewa kwa dhamana

[emoji117]Miaka saba tunawindana kwa chuki na uhasama

[emoji117] Ee Mungu muumba wa hii dunia, usiliache taifa lako litie mwanga!!
 
Hakika hakuna aliye na uwezo wa kuzuia mwisho wake,hata uwe na mipesa kedekede mwisho ukifika umefika,
Cha muhimu tuache tabia za kutukuza watu bali Mungu tu

Miisho mingine hii tunaipalilia wenyewe.

Ukanunue kamba. Ukajitundike mwenyewe. Kisha tuseme mwisho umefika?

Hatimaye CAF katulazimisha kucheza mechi yao bila mashabiki. Kina Prof. Mchembe, Mgaya, Makube, Gwajima nk. Wapo tu wanaendelea kuhamasisha nyungu?

Aaah wapi!
 
Back
Top Bottom