Wakati wa mahusiano kasema ana mtoto1, baada ya kuishi pamoja kumbe ana 3

Mwambie aendelee kuchapa mzigo. Angeambiwa ana ukimwi je ? Hao ni watoto na si mbwa aacha habari hizo bana.stress nyingine za kujitakia.
 
Hili jambo my bro pia lilimtokea ilikuwa mpaka imefika wiki 2 kabla ya harusi ndio aligundua mkewe ana watoto 3 na alikuwa anaishi na mwanaume kama mumewe uko mkoani
My bro alichanganyikiwa lakini mwishowe akakubali na maisha yanaendelea na wameshazaa mtoto wao

Huyo wifi yako alifanya jambo sahihi kabisa kulingana na mazingira ,maongezi na mitazamo ya kaka yako kwa kipindi kile walichokutana mimi naona hana kosa na amsamehe tu maisha yaendelee coz inawezekana angemwambia ukweli wasingekuwa pamoja
Hii comment imenibariki sana.Asante sana Mkuu ubaraikiwe
 
Yaani kumuacha ni issue.Kila mahali anajulikana kama mke hadi church wanawauliza mbona hamfungi ndoa?
Kumuacha sio suluhisho sbb nae tayari anawatoto wanne kwa wanawake tofauti, NAE NI TATIZO hivyo amkanye awe mkweli maisha yaendelee, wote hao ni majipu hakuna mwenye nafuu, mashine kaikubali aendelee nayo BORA HUYO MWENYE WATOTO NA ANAMPENDA, ATAHANGAIKA ATAKUTANA NA MWENYE MARADHI
 
Mmoja huyo alietambulishwa anaishi nao huyo wa Primary.Ila hao wa Secondary wanaishi kwa ndugu wa baba yao.Wote wanasoma wapo boarding.
Hao watoto wa kaka yako nao wanaishi wapi?
Sbb usikute anawalea yeye alafu wa mwenzie wako mbali wanamkera, Uselfish
 
Ni ngumu sana kumessa coz mke hakuwa muwaz tangu mwanzo ila cha msingi ni kumsamehe Maisha yaende sababu ukimuacha hutojuwa hy utaempata atakuwa na janga gani... Pia akae chin amwambie kuwa km kuna mengineyo kaficha ayaweke wazi tuu coz akija kugundua hakutakuwa na msamaha tena
 
mhmhmhmh kumbe wifiyo mzuri analipa watoto wa tatu lakin bado anadai.
tatizo ukweli mchungu na alimpenda kakayo wavumiliane tu
 
Hiyo ndoa kwenye nchi zenye sheria inaweza kuvunjwa ikafanywa kama haikuwahi kuwapo (annulment).
 
Heshima kwenu wakuu,

Nina kaka yangu ana mke na huyu wifi yangu ni mke mzuri kwa kweli kila mtu wa familia anampenda ikiwemo mimi binafsi kutokana na tabia zake njema na zisizokera.Kaka yangu huyu wakati anatafuta mke alitamani apate mke mwenye mtoto anagalau mmoja kwasababu yeye ana watoto watatu tayari.

Issue hapa ni kwamba wakati anafahamiana na wifi yangu huyu.Waliulizana habari za watoto wifi akasema anae mtoto mmoja.(Na kaka aliamini kitokana na wifi alivyo decent)Walipoanza kuishi pamoja miaka 2 imepita now na wifi akajifungua mtoto mwingine wa kaka.

Sasa kupitia ndugu zake ndo kaka amegundua kuwa wifi ana watoto 3 na sio mmoja kama alivyosema awali.Kumuuliza mkewe kasema ni kweli ila alishindwa kusema mwanzo kwasababu aliogopa kuachwa.Hao watoto 2 wakubwa wa Sekondari.Na huyu anaeishi nae ni wa shule ya msingi.
Wote wanaishi Dar.

Kaka anashindwa afanyeje ameniomba nimshauri kabla hajaweka wazi kwa wanafamilia wengine.Nimemwambia hii kwangu ni mpya nikamuomba nipost JamiiForums amekubali.Yeye sio member humu ila ushauri atasoma.

Kwa wenye uzoefu hii issue imekaeje ushauri wenu ni muhimu sana.
Kosa la mwanamke ni kudanganya kuhusu idadi ya watoto. Lakini kama wewe mwenyewe umekiri kuwa huyo wifi ana tabia njema na kupendwa na familia iweje kugundulika idadi kamili ilete dosari leo? Hao watoto watatu walikuwepo kabla ya nyinyi kujua na mlimkubali sasa leo isiwe kigezo cha kumtia dosari mtu ambae wote mmempenda. Mwenye maamuzi ya mwisho ni kaka yako maana yeye ndie anaeishi na huyo mwanamke na kama hakugundua tofauti yeyote mpaka alipoambiwa basi inamaanisha hakuna sababu ya kuweka tofauti sasa.
Hao ndugu waliomwambia sio wema pia, wangekuwa na nia ya dhati wasigesubiri mpaka baada ya kupatikana mtoto ndani ya ndoa ndio wafichue siri, inamaanisha ni waharibifu tu. Baada ya yote hata kama angekuwa na watoto kumi ikumbukwe ni kabla ya kuwa na kaka yako. Mshauri ayamalize yeye na mkewe, si kila jambo lihusishwe famailia yote.
 
Back
Top Bottom