Wakati wa mahusiano kasema ana mtoto1, baada ya kuishi pamoja kumbe ana 3

Executivesister

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
514
594
Heshima kwenu wakuu,

Nina kaka yangu ana mke na huyu wifi yangu ni mke mzuri kwa kweli kila mtu wa familia anampenda ikiwemo mimi binafsi kutokana na tabia zake njema na zisizokera.Kaka yangu huyu wakati anatafuta mke alitamani apate mke mwenye mtoto anagalau mmoja kwasababu yeye ana watoto watatu tayari.

Issue hapa ni kwamba wakati anafahamiana na wifi yangu huyu.Waliulizana habari za watoto wifi akasema anae mtoto mmoja.(Na kaka aliamini kitokana na wifi alivyo decent)Walipoanza kuishi pamoja miaka 2 imepita now na wifi akajifungua mtoto mwingine wa kaka.

Sasa kupitia ndugu zake ndo kaka amegundua kuwa wifi ana watoto 3 na sio mmoja kama alivyosema awali.Kumuuliza mkewe kasema ni kweli ila alishindwa kusema mwanzo kwasababu aliogopa kuachwa.Hao watoto 2 wakubwa wa Sekondari.Na huyu anaeishi nae ni wa shule ya msingi.
Wote wanaishi Dar.

Kaka anashindwa afanyeje ameniomba nimshauri kabla hajaweka wazi kwa wanafamilia wengine.Nimemwambia hii kwangu ni mpya nikamuomba nipost JamiiForums amekubali.Yeye sio member humu ila ushauri atasoma.

Kwa wenye uzoefu hii issue imekaeje ushauri wenu ni muhimu sana.
 
Kwani hao watoto wanadhuru nini? Kama anampenda mkewe haina tabu japo tayari ameshaweka doa kwenye moyo wake kuhusu mkewe kumdanganya. Waendelee tu na maisha.
 
Back
Top Bottom