Wakati wa Lowassa ''walishitakiwa'' ICJ; Wakati wa Lissu ''wameshitakiwa'' ICC

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Mwanafizikia mwenye asili ya Kiyahudi kutoka nchi ya Ujerumani, Albert Einstein aliwahi kusema, ''Upumbavu ni kuendelea kufanya vitu vile vile kwa njia zile zile na kutegemea kupata matokeo ya tofauti''

Tulichokiona mwaka 2015, baada ya Uchaguzi Mkuu ndicho hiki tunachokiona baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Ujinga na kujipumbaza unaofanyika leo kuhusu ICC ndio huo huo uliofanyika mwaka 2015.

Ikumbukwe kuwa, baada ya Rais Magufuli kutangazwa mshindi wa Urais mwaka 2015, tuliambiwa CHADEMA imepeleka kesi kwenye Mahakama ya kimataifa (The International Court of Justice-ICJ) na tukae ''mkao wa kula'' kwa sababu baadhi ya viongozi serikalini watakamatwa na kufikishwa kwenye mahakama hiyo. Ndio, Mahakama ya Kimataifa (ICJ)!

Kwa wale ambao hamkuwahi kusoma/ kusikia hiki kichekesho cha ICJ baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, ngonga hii thread usome;
LINK>>>
Kuna baadhi ya watu wajinga waliamini huu ujinga na wakasubiri siku hiyo ifike huku wakifurahi. Hawa wajinga hawakujua hata kazi za mahakama ya kimataifa (ICJ).

Miaka mitano baadaye tumejikuta tena kwenye ujinga kama ule ule wa mwaka 2015 tukiambiwa tena ''mashitaka'' yamepelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (The International Criminal Court-ICC) na tukae ''mkao wa kula'' kwa sababu baadhi ya viongozi serikalini watakamatwa na kufikishwa kwenye mahakama hiyo.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu mwenye akili timamu akikwambia jambo la kijinga na akijua una akili timamu na usipomkatalia anakudharau sana"

Hawa watu wanaotueleza huu ujinga wanawadharau sana wafuasi wao kwa sababu wanachowaambia wanajua hakiwezekani na hakiwezi kutokea!

Kuna ''wajinga'' wanadhani Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ni kama mahakama za kawaida nchini!

Wahenga walisema, ''kama huwezi kujua udogo au ukubwa wa tatizo, huwezi hata kujua mbinu ya kulishughulikia''.

Chukua mfano, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 uliofanyika Kenya ulisababisha zaidi ya watu 1,200 kupoteza maisha na wengine 600,000 kuzikimbia nyumba zao. Moja ya sababu kubwa ilikuwa ni mapigano yaliyosababishwa na viongozi wa kisiasa ambayo yalikuwa na mlengo wa kikabila. Pamoja na ukubwa wa tatizo hili, kesi ilitupiliwa mbali kwenye mahakama ya ICC.

Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2017 nchini Kenya, zaidi ya watu 30 walipoteza maisha na mamia kujeruhiwa lakini kikubwa zaidi, Mkurugenzi wa Kitengo cha TEHAMA ambaye alionekana kuwapendelea wapinzani aliuwawa na mwili wake kuokotwa ukiwa hauna mkono. Hakuna kilichotokea kuhusu ICC. Maisha yaliendelea kama kawaida huku Mzee Odinga kwa sasa akifanya kile ambacho waingereza walisema, ''If you can't beat them, join them''.

Ukitaka kusoma kuhusu vurugu za Uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya Soma hapa:

Leo hii eti tunaambiwa viongozi wa serikali nchini watapelekwa kwenye Mahakama ya ICC kwa madai ya ACT-Wazalendo kuwa wananchi 13 wamepoteza maisha kwenye uchaguzi mkuu. Kumbuka hii ni namba ambayo imetolewa bila ushahidi kama kweli ni watu 13.

Ikumbukwe kuwa, kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2001, zaidi ya watu 35 waliuwawa Zanzibar na wengine wapatao mia sita kujeruhiwa. Wazanzibari wengine zaidi ya 2,000 walikimbilia nchini Kenya. Hakuna kilichotokea kuhusu ICC.

Kuna baadhi ya watu wanaamini huu ujinga wa sasa kuhusu ICC kama walivyoamini mwaka 2015 kuhusu ICJ.

Kwa kiwango cha chaguzi za nchi za Afrika, uchaguzi wetu wa mwaka huu ulikuwa wa amani sana. Kila mwenye uelewa wa siasa za nchi za Afrika anajua.

Kwa mktadha wa chaguzi za nchi za Afrika ukilinganisha na uchaguzi wetu ndio maana hakuna taifa ambalo limesema rasmi halitambui matokeo ya Uchaguzi (illegitimate ) badala yake wanasema uchaguzi haukufuata kanuni za kunyambulika (irregularity). ''illegitimate'' na ''irregularity'' ni maneno mawili tofauti yenye maana muhimu sana katika sheria.

Mabalozi wa nchi mbali mbali hasa Ulaya na Marekani waliohudhuria kuapishwa kwa Rais Magufuli ilikuwa ni ishara inayotosha kuonyesha hizi kelele za ICC ni ujinga mwingine kama wa 2015.

Kilichokuwa kinatafutwa ni wananchi waingie barabarani halafu polisi watumie nguvu kuwazuia ili mauwaji yatokee! Waliokuwa wametega mtego huu walijua Rais Magufuli/serikali wangetumia ''nguvu'' ambazo zingesababisha mauwaji ya wananchi wengi ili iwe ni ushahidi wa kuomba ICC waanze uchunguzi. Mtego wao haukumnasa Rais Magufuli au serikali yake!

Kwa sasa kinachofanywa na wanaotuaminisha kuhusu ICC ni kama mgonjwa kupewa kipoza uwongo (placebo) na kuanza kutumaini atapona!
 
Back
Top Bottom