Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza

Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau

sent from toyota Allex
Kwa hyo mkuu wewe n Mhujum Uchumi in Mabeberu Voice

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Aisee nilifikiri kubaki DSM baada ya chuo ni lelemama. Kumbe ni mabaki ya Boom yalikuwa yananidanganya.

Nikasambaza CV mpaka na hela ya kuprint, kula na nauli zikaisha bila kupata kazi.

Nyumbani mbali na nauli sina. Kazi ikawa ni kujitetea nisife njaa. Nikaona njia pekee ya kusurvive ni kusahau kama nina Degree.

Nikafanya kazi yoyote bora mkono uende mdomoni, lakini bado Jamaa wananitenga wanahisi naigiza Maisha eti mimi ni mpelelezi!

Nikaona isiwe tabu, nikachagua Nyumba zangu Tano kupita kuomba kuwa houseboy. Nikikosa basi nabadili plan. Ya tatu nikapata ila kwa kudanganya niliishia la saba.

Nilifanya Kazi za ovyo vya kutosha, mpaka nikatamani niendelee nimalizie kuomba kazi zile nyumba nyingine zilizobaki labda ningepata yenye nafuu.

Wazo likanijia ni bora niseme ukweli nilisoma labda kazi zitabadilika. Cha ajabu majukumu yakaongezeka. On top of all, ndio kwanza nikawa mwalimu wa tuition kwa watoto wa familia ya Boss. Wadogo wa kiume wako primary mmoja wa kike alikua chuo mwaka wa pili. Usisahau mshahara ni ule ule wa hovyo.

Kwa kazi za binafsi nilizokuwa namfanyia, ilifika mahala mke wa Boss akaanza kucatch feelings za kuhitaji niwe naye. Nilikua naelekea kukubali kwa sababu Sina namna. Ghafla Boss nadhani alihisi kitu akaona ni bora anisomeshe CPA (Wahasibu wanaelewa) ili niwe busy zaidi. Nilikua busy sijawahi ona.

Baada ya yoote, Boss aliniunganisha nikapata kazi. Kutoka kwenye familia ya Boss nilipata Mke Mwema ambaye ni mwanafunzi wangu. Japo mke wa Boss bado ananisumbua.

Ila uhauseboy sitakaa nisahau! Nilikuja kuapa sitakaa nimnyanyase msaidizi wangu wa kazi kwa vyotote iwavyo. Duh, Guys hawa watu wanapitia Magumu sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mbona umemwacha mke wa boss hv hv ebu kula aisee hyo kuku na mayai yake

Mmenikumbusha maisha ya chuo, nipo zangu chuoni na jamaa wanaotoka familia tajiri sana, wao kila mwezi wanatumiwa sio chini ya $300 kwa ajili ya matumizi ya chakula, mavazi na luxuries zingine. Mimi natoka familia ya kawaida sana, maisha ya kawaida sana, nikajisemea nisipochekecha akili nitakuwa zobaaaa. Hivi huku mbali kweli nisubiri pesa za wazee, hapana!!

Nikatoka zangu, nikaenda supermarket moja ilikuwa inabamba sana mji huo, nikaomba kazi wakasema hatuwezi kukuajiri coz huna vibali vya ajira, dadeq níkaona sasa hapa nafeli, pesa naitaka nijikimu na pia nidundulize ili nikimaliza chuo niwe na pesa za kuanzia life. Nikaacha kujichanganya na wana "weusi" manake niliona nikiwa nao nitapoteza mda wangu, nikaanza kutafuta urafiki na classmates zangu "weupe", nikapata kama jamaa wawili na dada mmoja nae hakutokea mji ule. Yule dada akawa rafiki yangu sana ila sikutaka hata kumfanya "kimasihara" coz nilijua nitaharibu. Nikamuuliza kuhusu kazi baada ya masomo, akasema ataniunganisha na jamaa zake nao wanafanya kazi part time. Kweli nikakutana na jamaa, wakaniambia the best option ni kazi za construction, wages ni kubwa kuliko huko supermarket au kusafisha barabara kutoa mabarafu. Nikasema poa nipelekeni, nikapelekwa kuna bosi wa kike na MD wa kampuni ni kidume, yule MD akasema hatuwezi kufanya kazi na "mtu wa namna hii", nikajua tu ngozi yangu inaninyima kazi, bahati nzuri yule boss wa kike alinihurumia, akabembeleza sana kwa MD mwisho nikakubaliwa.

Nikapeleka ratiba yangu ya masomo, wakanipangia kazi kutokana na ratiba zangu. Dadeq sitasahau, nilikuwa nalala mda mchache sana, nikitoka class hata sirudi maskani, naenda site napiga kazi at -25°C, kuna kipindi baridi ilifika -40°C, nimevaa gloves za baridi lakini vidole vinaungua kama napitisha kwenye moto, navaa soksi nzito na buts zenye sufi ndani, lakini miguu inakakamaa, vidole vinakufa ganzi lakini kazi lazima ifanyike, wenzangu wanachapa Smirnoff, Vodka, wanavuta sigara balaa ili kutoa baridi, dadeq sitasahau, ila nashukuru nilibaki vile, nilijaribu kidogo kuonja Smirnoff . Baadae nilikuja kuzoea na kuona ni kawaida sana, wenzangu waliniona bonge la kidume, working at -20 to 35°C nje kabisa ilikuwa ni changamoto kubwa kuwahi kutokea.

Nilivyokaribia kumaliza chuo nikapata kazi kwenye kiwanda cha samaki, life was I bit easier there. Walinipenda sana the way nilikuwa nafanya kazi kwa kujituma, hadi namaliza pale boss alinifanyia goodbye party, na kupewa zawadi. Hapa ndio nilipata kuzichakata punani bila hiana, nilihakikisha nalitendea kabila langu haki.
Punani ndo nn tena mkuu umetuacha kolomije ndani ndani hko!

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Maisha Yana Vingi Sana

Mimi Niligonga O Advance Bihawana Hapo Dodoma

Kurudi Kitaa Dah Raia Wote Wanajua Mim Naenda Chuo Muda Ulipofika Nikawa Bado Nipo Nikasingizia Mkopo Kumbe Nilipiga Bashite La PCB Yaan Pure 0 (Gs Na BAM Zote F)

Basi Nikamuomba Bro Mmoja Akawa Ananipa Boda Yake Nakula Vichwa Usiku Huwezi Amini Siku Ya Kwanza Usiku Nikagonga Mtu Nikapelekwa Sero Nikakaa Wiki.

Nipo Ndani Nikawaza Vingi Sana Ndipo Nilipotoka Nikajiunga Na Jf Nikapata Kazi Ya Lodge Humu Humu Mshaara 100k Ipo Huko Airport Lakin Shughul Yake Sio Ya Kitoto, Unafua Shuka Watu Wamelana Ndogo Yaan Mav Kabisa Na Hakuna Gloves Kabisa Yaan Unapitia Tabu Mpaka Unaona Dah Hapa Siwez Ila Ukikumbuka Msoto Wa Home Unafanya Then Unasahau, Nilikaa Pale Miez Mitano Nikamuibia Ibia Nikapata Kama 2M.

Nikarudi Kitaa Nikanunua Boda 1.2M Kwa Bro Kuja Kuchunguzwa Kumbe La Wizi Nikaenda Tena Ndan Mwezi Sema Bi Mkubwa Akaja Kunitoa.

Nikarud Mtaan Tena Nikawa Najichanganya Tu Mpaka Nikpata Nafasi Ya Chuo Diploma CO.

Kufika Chuo Ndio Nikaanza Kujifanya Fund Simu Na Laptop, Mtu Akileta Simu Naenda Choon Na Google Jins Ya Kuifungua Na Tatizo Lake, Nikawa Nafanya Hivyo Na Zinapona Na Nyingine Zinazima Kabisa But Nashukuru Mungu Hii Mishe Iliniingizia Pesa Sana Na Ndio Naifanya Mpaka Now Japo Ka Diploma Ninako Ila Sikatumii.

#Wilmer

Sent using Jamii Forums mobile app
watu wanakulana nini mkuu??

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza

Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau

sent from toyota Allex

Navipenda sana vimoro asee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu mbona umemwacha mke wa boss hv hv ebu kula aisee hyo kuku na mayai yake

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app

Mkuu mume wake ni Mtu mmoja mstaarabu sana. Na kwa wema alionitendea na anaoendelea kunitendea nafsi inanisuta sana kumfanyia mabaya.

Mpaka leo huwa ananiambia ameniruhusu kuoa mwanae lakini anaona kama amemuozesha mtoto wake kwa mwanae wa kiume wa kumzaa.
 
Mimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..

Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu

Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.

Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..

Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..

Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!

Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..

Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..

Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..

Sent using Jamii Forums mobile app
Gereji gani na mwaka gani
 
Mkuu huwa kuna baraka ambayo Mungu ameiachilia kwa wazazi,kwa kuwa Mzee alishafariki na mama inaonekana hamna mawasiliano vizuri yamkini hili linakutafuna.

If you dont mind, Jaribu kumtafuta mama then andaa zawadi ambayo inaweza kugusa moyo wa mama umpatie,kisha sema nae vizuri muombe radhi kwa kumtelekeza muombe akutamkie baraka kisha rudi kapambane. Trust me unaweza pata breakthrough kwenye maisha hadi ukashangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi naona mama ndo aliemtelekeza mtoto
 
Aisee nilifikiri kubaki DSM baada ya chuo ni lelemama. Kumbe ni mabaki ya Boom yalikuwa yananidanganya.

Nikasambaza CV mpaka na hela ya kuprint, kula na nauli zikaisha bila kupata kazi.

Nyumbani mbali na nauli sina. Kazi ikawa ni kujitetea nisife njaa. Nikaona njia pekee ya kusurvive ni kusahau kama nina Degree.

Nikafanya kazi yoyote bora mkono uende mdomoni, lakini bado Jamaa wananitenga wanahisi naigiza Maisha eti mimi ni mpelelezi!

Nikaona isiwe tabu, nikachagua Nyumba zangu Tano kupita kuomba kuwa houseboy. Nikikosa basi nabadili plan. Ya tatu nikapata ila kwa kudanganya niliishia la saba.

Nilifanya Kazi za ovyo vya kutosha, mpaka nikatamani niendelee nimalizie kuomba kazi zile nyumba nyingine zilizobaki labda ningepata yenye nafuu.

Wazo likanijia ni bora niseme ukweli nilisoma labda kazi zitabadilika. Cha ajabu majukumu yakaongezeka. On top of all, ndio kwanza nikawa mwalimu wa tuition kwa watoto wa familia ya Boss. Wadogo wa kiume wako primary mmoja wa kike alikua chuo mwaka wa pili. Usisahau mshahara ni ule ule wa hovyo.

Kwa kazi za binafsi nilizokuwa namfanyia, ilifika mahala mke wa Boss akaanza kucatch feelings za kuhitaji niwe naye. Nilikua naelekea kukubali kwa sababu Sina namna. Ghafla Boss nadhani alihisi kitu akaona ni bora anisomeshe CPA (Wahasibu wanaelewa) ili niwe busy zaidi. Nilikua busy sijawahi ona.

Baada ya yoote, Boss aliniunganisha nikapata kazi. Kutoka kwenye familia ya Boss nilipata Mke Mwema ambaye ni mwanafunzi wangu. Japo mke wa Boss bado ananisumbua.

Ila uhauseboy sitakaa nisahau! Nilikuja kuapa sitakaa nimnyanyase msaidizi wangu wa kazi kwa vyotote iwavyo. Duh, Guys hawa watu wanapitia Magumu sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hongera sana mkuu na pia pole, kwa jinsi ninavyoishi na house girl wangu ni ngumu kujua kama ni house girl hata kama ni out nikitoka natoka nae pamoja na watoto wangu,
Hata ratiba za chakula nyumbani mara nyingi ni yeye hupanga.
 
Aisee nilifikiri kubaki DSM baada ya chuo ni lelemama. Kumbe ni mabaki ya Boom yalikuwa yananidanganya.

Nikasambaza CV mpaka na hela ya kuprint, kula na nauli zikaisha bila kupata kazi.

Nyumbani mbali na nauli sina. Kazi ikawa ni kujitetea nisife njaa. Nikaona njia pekee ya kusurvive ni kusahau kama nina Degree.

Nikafanya kazi yoyote bora mkono uende mdomoni, lakini bado Jamaa wananitenga wanahisi naigiza Maisha eti mimi ni mpelelezi!

Nikaona isiwe tabu, nikachagua Nyumba zangu Tano kupita kuomba kuwa houseboy. Nikikosa basi nabadili plan. Ya tatu nikapata ila kwa kudanganya niliishia la saba.

Nilifanya Kazi za ovyo vya kutosha, mpaka nikatamani niendelee nimalizie kuomba kazi zile nyumba nyingine zilizobaki labda ningepata yenye nafuu.

Wazo likanijia ni bora niseme ukweli nilisoma labda kazi zitabadilika. Cha ajabu majukumu yakaongezeka. On top of all, ndio kwanza nikawa mwalimu wa tuition kwa watoto wa familia ya Boss. Wadogo wa kiume wako primary mmoja wa kike alikua chuo mwaka wa pili. Usisahau mshahara ni ule ule wa hovyo.

Kwa kazi za binafsi nilizokuwa namfanyia, ilifika mahala mke wa Boss akaanza kucatch feelings za kuhitaji niwe naye. Nilikua naelekea kukubali kwa sababu Sina namna. Ghafla Boss nadhani alihisi kitu akaona ni bora anisomeshe CPA (Wahasibu wanaelewa) ili niwe busy zaidi. Nilikua busy sijawahi ona.

Baada ya yoote, Boss aliniunganisha nikapata kazi. Kutoka kwenye familia ya Boss nilipata Mke Mwema ambaye ni mwanafunzi wangu. Japo mke wa Boss bado ananisumbua.

Ila uhauseboy sitakaa nisahau! Nilikuja kuapa sitakaa nimnyanyase msaidizi wangu wa kazi kwa vyotote iwavyo. Duh, Guys hawa watu wanapitia Magumu sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Aisee pole sana lakini pia hongera sanaa kwa kupambana.
 
Back
Top Bottom