Wakati Uingereza wako mbioni kuzuia umiliki wa vito vyenye ivory, Tanzania tunatoa vibali vya kununua pembe za ndovu!

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,751
2,000
UK na nchi nyingine za Ulaya wapo mbioni kupitisha sheria ya kuzuia watu kumiliki vito vyovyote vyenye pembe za ndovu hata kama kilitengezezwa in 1960s. Sheria hii ni kwa ajili ya kuisadia Africa hasa nchi kama Tanzania na Kenya ambazo zimekuwa zikitajwa tajwa kwenye hii biashara haramu.

Prince William ambaye alikutana na raisi Magufuli ikulu katika kuhamasisha vita ya anti poaching nimeshangaa kusoma leo utetezi kwenye sakata la Akram Aziz kwamba aliruhusiwa kununua pembe za ndovu...this makes a mockery of anti poaching campaign.

Britain to ban ivory items regardless of their age.

LONDON (Reuters) - Britain will ban the sale of ivory items regardless of their age in an effort to restrict the illegal ivory trade, tackle poaching and help protect elephants, the government said on Tuesday.

New legislation will create the toughest ban on ivory in Europe and one of the toughest in the world, it said, with a prohibition on the sale of nearly all antiques containing ivory.

International commercial trade in ivory has been illegal since 1990 and the sale of raw African Elephant ivory of any age is not authorized in Britain.

But currently, worked items produced before 1947 can be traded within Britain or other EU countries, as can items produced after 1947 that have government certificates.

Environment Secretary Michael Gove said the tougher restrictions, which follow a public consultation, would demonstrate Britain’s belief that “the abhorrent ivory trade should become a thing of the past”.

Ivory should never be seen as a commodity for financial gain or a status symbol, so we will introduce one of the world’s toughest bans on ivory sales to protect elephants for future generations,” he said in a statement.

There will be exemptions for antique items that contain less than 10 percent ivory by volume, some old musical instruments, and the rarest and most important items of their type, including portrait miniatures painted on slivers of ivory.

The World Wide Fund for Nature (WWF) said around 55 African elephants were killed for their ivory a day, with their tusks turned into carvings and trinkets.

“This ban makes the UK a global leader in tackling this bloody trade, and it’s something WWF has been fighting hard for,” chief executive Tanya Steele said.

“But if we want to stop the poaching of this majestic animal, we need global action. We hope the UK will continue to press countries where the biggest ivory markets are, most of which are in Asia, to shut down their trade too.”Baadhi ya sehemu ya utetezi uliotolewa na Kilombero North Safaris hapo chini:
upekuzi huo zimekutwa pembe sita za ndovu ambazo zina mihuli na vibali vyote vya serikali na pembe zote zina ‘serial numbers’ zikionyesha zilipatikana mwaka 2014. Hii ni kwa mujibu wa sheria.Kenya wameonyesha nia ya kweli ya kupambana na hii biashara ya haramu:
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,290
2,000
UK na nchi nyingine za Ulaya wapo mbioni kupitisha sheria ya kuzuia watu kumiliki vito vyovyote vyenye pembe za ndovu hata kama kilitengezezwa in 1960s. Sheria hii ni kwa ajili ya kuisadia Africa hasa nchi kama Tanzania na Kenya ambazo zimekuwa zikitajwa tajwa kwenye hii biashara haramu.

Prince William ambaye alikutana na raisi Magufuli ikulu katika kuhamasisha vita ya anti poaching nimeshangaa kusoma leo utetezi kwenye sakata la Akram Aziz kwamba aliruhusiwa kununua pembe za ndovu...this makes a mockery of anti poaching campaign.

Baadhi ya sehemu ya utetezi uliotolewa na Kilombero North Safaris hapo chini:
Kenya wameonyesha nia ya kweli ya kupambana na hii biashara ya haramu:
Unashangaa hilo wakati watu wana viwanja kwenye mbuga na hati miliki halali ziliotolewa na serikali.....
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,751
2,000
Unashangaa hilo wakati watu wana viwanja kwenye mbuga na hati miliki halali ziliotolewa na serikali.....
Wakulaumiwa hapa ni serikali. Nchi ambazo hazina tembo wala vifaru lakini wanapiga kampeni ya kuzuia hii biashara haramu. Sisi ndio tuna hamasisha kwa kutoa vibali!
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,290
2,000
Wakulaumiwa hapa ni serikali. Nchi ambazo hazina tembo wala vifaru lakini wanapiga kampeni ya kuzuia hii biashara haramu. Sisi ndio tuna hamasisha kwa kutoa vibali!
Sasa mkuu kama mtu umesha muuzia plot kwenye mbuga ya wanyama utamdhibiti je kutopata pembe kwenye ploti lake hilo ndo kosa la kwanza la serikali.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,751
2,000
Hamisi Kingwagwala amekuwa ana fanya kazi na amini atalifanyia kazi hili
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,047
2,000
Mbona wao wanaruhusu bangi yenye madhara kwa kiumbe Binadamu lakini hatuwasemi tumewapa Uhuru.

Pembe za ndovu sio zote zinapatikana kwa kuua Tembo .
Tembo kama viumbe wengine wanazaliwa wanakua na wanakufa kwa maelfu. Sasa Tembo akifa tumzike na pembe yake wakati Mungu ametupa utajiri wa hiyo pembe?

Tunachokataa ni kuua Tembo ili kupata pembe na meno lakini kama amekufa sioni kwa nini tusiuze na kupata fedha.
Jambo la msingi ni kuwalinda Tembo hai kama ilivyo binadamu anavyolindwa siku zote. Lakini kama Tembo anakufa kifo cha asili kwa kweli hili lijadiliwe kwa mapana zaidi.
 
introvert

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,370
2,000
babu M

Kuna tofauti kati ya hunting (uwindaji) na poaching (ujangili). The former is legal and the latter is illegal.

Trophies kama pembe, meno, ngozi n.k. ni legal na zinauzwa na Serikali kwa wawindaji. Kuna risiti zake kabisa kutoka wizarani. Hivyo kununua pembe, meno au ngozi si kosa!

Uelewa wetu juu ya hunting na poaching unafanya tuhukumu mtu yoyote anayefanya hunting kwamba ni poacher.
 
Ninaelewa hilo. Ninalopinga ni Tanzania kuwa na hiyo sheria ya kuwinda Tembo na ndovu.
1) Hii sheria ina encourage poaching. Mfano, hayo meno ya tembo yenye kibali na serial numbers. Ninaweza kuyauza ni kaenda kununua mengi kwa majangili na kuyaweka serial numbers zile zile na hatimaye kutumia kibali kile kile.

2) Ndovu na Tembo Idadi yao imepungua sana na wapo harini kuisha kabisa. Sasa kuendelea kutoa kibali ni kwamba hatutambui hilo tatizo.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,751
2,000
Mbona wao wanaruhusu bangi yenye madhara kwa kiumbe Binadamu lakini hatuwasemi tumewapa Uhuru.

Pembe za ndovu sio zote zinapatikana kwa kuua Tembo .
Tembo kama viumbe wengine wanazaliwa wanakua na wanakufa kwa maelfu. Sasa Tembo akifa tumzike na pembe yake wakati Mungu ametupa utajiri wa hiyo pembe?

Tunachokataa ni kuua Tembo ili kupata pembe na meno lakini kama amekufa sioni kwa nini tusiuze na kupata fedha.
Jambo la msingi ni kuwalinda Tembo hai kama ilivyo binadamu anavyolindwa siku zote. Lakini kama Tembo anakufa kifo cha asili kwa kweli hili lijadiliwe kwa mapana zaidi.

Mkuu, utawezaje kujua meno haya yamepatika kwa tembo waliokufa na haya ni kutokana na uwindaji?
Kwani watashindwa kuwa hua kwa njia ambazo zinaweza kuonyesha kwamba wamekufa kifo cha kawaida?
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,047
2,000
Meno ya Tembo yaliyothibitika hua yanatakiwa yawekwe S/N ya serikali.
Kwa hiyo mtu yeyote akiona Tembo aliyekufa lazima atoe taarifa kwa askari wa wanyama pori. Hivyo ni rahisi sana kujua.

Bado nasema kuwa Pembe wa tembo wetu waafrika kama wapo watu wanaowataka kwa fedha ili wananchi wetu wapate maendeleo ni vizuri tuwauze.

Mfano unakuta Serikali ina akiba ya meno yenye thamani ya bil 20 halafu anatokea mtu anasema kuwa zichomwe moto adharani kama ishara ya kupinga ujangili. Huu ni ujuha !! Uza meno, pata Bil.20 ,nunua , helkopta ya kuimarisha ulinzi kwenye hifadhi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom