Wakati Tanzania tukigawa mali zetu Argentina wataifisha

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Chanzo: mpayukaji blog[/h]

cristina.jpg

Rais Fernandez pichani

Rais mpya wa Argentina Cristina Kirchner Fernandez ameamua kutaifisha kampuni kubwa ya mafuta nchini humo ya YPF oil baada ya kugundua kuwa wawekezaji wa Kihisipania waliinunua na kuiua kampuni husika kama ambavyo tumeshuhudia nchini Tanzania.
Baada ya kutaifisha kampuni ya YPF Oil, nchi nyingi hasa zinazounga mkono Hispania zilitoa tishio kuwa hatua hii ingeogofya wawekezaji hivyo kuathiri uchumi wa nchi. Rais Fernandez aliwajibu kwa kusema, " Huyu rais hatapoteza muda kujibu matishio yoyote... kwa sababu ninawakilisha watu wa Argentina."
Rais aliongeza, " Mimi ni mkuu wa nchi na si jambazi." Laiti rais wetu mpenda kugawa gawa mali zetu angekuwa na lau nusu ya ujasiri wa mama huyu! Majambazi wa EPA na Dowans wasingeweza kumweka mfukoni mtu kama huyu. Uzuri ni kwamba alichaguliwa kidemokrasia na si kwa hongo wala uchakachuaji au kuhonga pesa ya wizi kama ile za EPA.
 
Taarifa hiyo kutoka Argentina imeripotiwa jana na vyombo vingi vikubwa vya habari duniani. Sasa kwa kuwa Vaso Da Gama yuko Brazil jirani na kule natumaini habari atakuwa ameipata kwa karibu zaidi na kama angekuwa makini sababu najua hayuko makini angefuatilia kujua kulikoni wenzetu wamefanyaje kujinasua na ubeberu.

Jambo hili kwa Tanzania haliwezekani kwa sababu pale Magogoni tuna KICHWA CHA NAZI na pia Mjengoni ndiyo usiseme vimejaa tele. Kule nataja kimoja tu! vingine mtaendelezea; LIVINGSTON
 
Tanzania ya CCM suala hili halitawezekana kwa kuwa Viongozi wetu kutoka CCM, karibu wote wana hisa kwenye Makampuni ya kifisadi. Wanapojisifia kuhusu 'Mafanikio' ya ubinafsishaji usidhani ni hivi hivi, wanajaribu kutuosha akili.
 
wameua shirika la reli ili wapate kazi ya kusafirisha mafuta nchi jirani wakati huo huo wakiharibu barabara ! Wanawalipa mshahara kudhibiti kelele
 
wameua shirika la reli ili wapate kazi ya kusafirisha mafuta nchi jirani wakati huo huo wakiharibu barabara ! Wanawalipa mshahara kudhibiti kelele

ukweli ni kuwa watanzania wengi tunaakili sana sema akili zetu tunazitumia kwenye wizi zaidi na UCHOYO ndo unatusumbua!
 
safi mwana mama chapa mwendo!sisi deni la nchi linaongezeka huku gesi na madini hayana mchango ktk pato la taifa
 
Sisi tulitaifisha zamani. Awamu hiyo ilipita ikaja ya ubinafsishaji. Baadaye ukaja ufisadi. Sasa sijui tuko katika utekelezaji wa kipi.
 
Tanzania ya CCM suala hili halitawezekana kwa kuwa Viongozi wetu kutoka CCM, karibu wote wana hisa kwenye Makampuni ya kifisadi. Wanapojisifia kuhusu 'Mafanikio' ya ubinafsishaji usidhani ni hivi hivi, wanajaribu kutuosha akili.
vijihisa,vijisenti na wengine walishakula tende na kuzinya.wanawalinda wakubwa zao ili msimu mwingine wa tende wasikose
 
Taarifa hiyo kutoka Argentina imeripotiwa jana na vyombo vingi vikubwa vya habari duniani. Sasa kwa kuwa Vaso Da Gama yuko Brazil jirani na kule natumaini habari atakuwa ameipata kwa karibu zaidi na kama angekuwa makini sababu najua hayuko makini angefuatilia kujua kulikoni wenzetu wamefanyaje kujinasua na ubeberu.

Jambo hili kwa Tanzania haliwezekani kwa sababu pale Magogoni tuna KICHWA CHA NAZI na pia Mjengoni ndiyo usiseme vimejaa tele. Kule nataja kimoja tu! vingine mtaendelezea; LIVINGSTON

Hata mimi nimeipata jana lakn huyu gamba hawezi kuthubutu tuombe mungu tukishinda cc chadema 2015 haya yatawezekana
 
Back
Top Bottom