Rais tupe haki yetu ya uhai pamoja na usalama na mali zetu

NANCA

Member
Jun 23, 2023
92
100
Hii nchi imekua ya mateso kwa miaka mingi hasa kwa watu wanyonge na maskini. Wanasiasa na wenye mamlaka wamekua wakionea sana watu wadogo, wamekua wakichukua uhai wa watu wanyonge mfano ditopile alivyo chukua uhai wa dereva pale kawe bondeni njia panda na wala hakuna hatua ya maana aliyochukuliwa.

Wanasiasa wamekua wakipokonya ardhi za wanyonge kimabavu, kwa kutumia sheria ya utwaaji au kwa kununua kilazima kwa bei ndogo, wanasiasa wamekuwa wakijikatia mapande ya ardhi kwa nguvu.

Watu duni wamekuwa wakiteswa kimwili na hata kuuwawa Kama ilivyo kung'olewa meno kwa Dr. Ulimboka, wanasiasa wamekuwa wakitumia nguvu na mabavu kuendesha biashara zao hasa mahala penye ushindani ambapo wapinzani wao wa kibiashara wamekuwa wakikiona cha moto.

Mfano unakuta mwanasiasa anasababishia ajari basi la kampuni nyingine kwa ifilisike na abakie yeye katika njia husika, kimsingi wanasiasa wetu wamekuwa wanatisha kuliko simba kwa wananchi ambao ndio hutumbukiza vipande vya kura ili kuwachagua.

Yaani wanasiasa wetu ndio wamekua kikwazo cha maendeleo, Jambo linalonufaisha umma hawalitaki Jambo linalowanufaisha wao ndio hulipigania.

Katika nchi hii masikini tunapitia wakati mbaya sana, wanasiasa wanataka kila kitu wanachodhani kizuri kiwe chao, wanaua, wanatesa na kunyanyasa, wanapora na kudhulumu wananchi wadogo.

Nimuombe Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atupe haki yetu ya uhai, usalama na mali zetu kwa kuhakikisha mwanasiasa au kiongozi yeyote anaepora chochote cha mtu duni basi ashughulikiwe ipasavyo, maana nchi inazidi kuwa masikini kwa kurudishwa nyuma watu masikini.

Haiwezekani wewe mbunge utake kuchukua ardhi yote ya Kijiji hata kufikia hatua ya kutishia watu, kutumia viongozi wa halmashauri na kulazimisha mtu akuuzie kilazima kwa bei unayotaka wewe na kama hataki unaanza kumfungia biashara zake kwa kuzishurutisha mamlaka nyingine zimshughulikie kwa manufaa yako.

Haiwezekani mwanasiasa akawa kama simba, hiyo NO!
 
Back
Top Bottom