Wakati Tanzania ipo gizani, Ethiopia kuzalisha 20,000MW! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati Tanzania ipo gizani, Ethiopia kuzalisha 20,000MW!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jun 29, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani 2005 mpaka 2010, serikali yake imeongeza uzalishaji wa umeme kwa 145 MW tu.
  Mpango mpya wa miaka mitano wa serikali umepanga kuhakikisha kuwa Tanzania inazalisha 2,780 MW kuanzia sasa mpaka 2015/16.

  Je, kama miaka 5 ya uongozi wa Kikwete imewekeza kwenye 145 MW, itatumia miujiza gani kuzalisha karibu 3,000 MW kwenye miaka 5 ijayo?

  Tuache hayo. Wakati Tanzania inafikiria kuzalisha pungufu ya 3,000 MW kwenye miaka 5 ijayo, nchi ya Ethiopia imepanga kuzalisha 20,000 MW (Twenty thousand megawatts) kwenye miaka 10 ijayo mpaka kuuza nje. Ethiopia wanawezaje na Tanzania ishindwe wakati nchi hiyo ina ukame mkubwa kufananisha na taifa letu?

  Ethiopia plans power exports to neighbours | Top News | Reuters
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hawa wanaweza si unaona hata shirika lao la ndege nina midege kama ya ulaya

  na wana mtu tajiri (bilionea mzalendo) anayependa nchi yake
   
 3. M

  Mtanzania Huru Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Kikwete na serikali yake ni kuwa they don't think big. Wao daima wanazungumzia miradi ya 45MW, 100MW au 300MW, wakati kwenye mradi mmoja tu Ethiopia wanazalisha 5,250 MW. Uko wapi mradi wa Stiegler's Gorge??!
   
 4. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hawa sio wenzetu kabisa, wakati sisi tunashangilia UDOM kila kukicha, hawa jamaa wao wanaplan big...
  Ethiopia Allocates Funds for 13 New Universities
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Raisi wetu yeye ana kata anga mida hii yuko kwenye pipa akielekea africa maghalibi. Hayo ya umeme hayamuhusu yeye
   
 6. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hawa wetu wanawaza kucheza KIDUKU, kulipana POSHO, kutowashtaki MAFISADI, kusafiri NG'AMBO, kutoa ahadi HEWA, kuongea PUMBA nk "wavivu wa kufiki na wazito wa kusikia"
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hivi jamani
  viongozi wetu hata wanavyo safiri hawaoni maendeleo ya wenzetu? je hawapati wivu juu ya hayo maendeleo

  hivi hata habari za hawa waethiopia wao hawazisikii? hata ndege za waethiopia viongozi hawazioni? yaani hawana hata wivu wa maendeleo kwa kile wakionacho wakati wakisafiri?

  mimi nashindwa kuelewa kabisaaa

  ina maana sisi wa JF ndio tuonayo haya peke yetu na viongozi wetu hawaoni,hawasomi habari,hawasikii, ama hawaoni umuhimu wa hii nchi kuendelea?

  inauzi kweli jamani
   
 8. M

  Mojo Senior Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani Kikwete kawekeza kwenye 145 MW tu za umeme kwenye kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano?! Kwa kweli huu mgao wa umeme unaoendelea kutusulubu Watanzania sasa hivi ni kosa la JAKAYA MRISHO KIKWETE. Inaniuma sana!
   
 9. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aisee kumbe Melesi Zenawi (sina uhakika na spelling) ni kichwa eeeeee? Bravo Ethiopia
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  tufanye mchakato mkubwa sana kuelekea mabadiliko. kila mwana jamiiforums ahakikishe kijijini/nyumbani anakotokea anaelimisha watu kadiri hali inavoruhusu juu ya ubaya wa seriakali ya ccm na namna ilivotuviza kimaendeleo kulinganisha na mali asili tulizojaaliwa na kwamba upinzani haumaanishi uvunjifu wa amani kama propaganda zinavopakazwa, watu waelezwe kutakuwa na maisha hata bila ccm (obvious yenye mafanikio zaidi) ili uchaguzi ujao wasiharibu ovyo kura kwa kuchagua ccm. tutashinda! tusiishie tu kusikitika humu jamvini maana wengi ya walio vjjini hata hawajui jamiiforums na unyang'au unaotendeka serikalini
   
 11. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Sharobalo hana muda na Tanzania kwa sasa, anatafuna maisha kwa kula kuku kwenye mawingu. Inabidi ashauriwe aende akatembee ISS huko juu karibu na mwezi. Watawasiliana na NASA kuwa sharabalo aende IIS kutembea
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Ethiopia has always been winners

  [​IMG]

  Mohammed Al Amoudi

  Sisi we cant even decide to build SERENGETI HIGHWAY tunawaachia wa KENYA na abunch of eco terrorists from WWF etc kutuamulia what's good or bad for us
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  well...sisi kumbe tuna megawats 600 tu bas!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwani Ethiopia kuna watu wangapi? Lakini, tujiulize vyanzo vyetu vyote vya umeme vina uwezo (vikiendelezwa) wa kuzalisha kiasi gani? labda tuna tatizo la vyanzo vya umeme.
   
 15. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dont forget Ethiopian Airways
   
Loading...