Wakati nchi ikijiandaa katika Vita ya kiuchumi na ACACIA, Mfahamu vizuri Peter Munk


Hatutakiwi kuogopa,maendeleo yetu yataletwa na UTAIFA wetu na hatutakiwi kuwa waoga kusema ukweli.Tuanze sasa kuwaambia watawala ukweli.

Waswahili wanasema.............'Mchelea mtoto kulia .................' na tumeanza kulia sababu tulichelewa kumliza mtoto
 
Mkuu ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Prof kaenda kuchunguza kilichomo kwenye makasha (containers) ndicho kilichomo kwenye mikataba? Prof kasema siyo tunaibiwa. Watu wamekazania mikataba mibovu jamani hebu tulizeni akili.
ili waongee lazima wataje mikataba mibovu na CCM.. vinginevyo hawana hoja...lol
 
Wakati hoja za ubinafsaji zinaligawa bunge, kuna wabunge huwa na vijembe sana kule bungeni na wakati mwingine huwa wanashangilia kwa kuzungusha viuno na makalio, nao ndio waleee, hao hao leo mmoja wao amejifanya anapigana vita vya kiuchumi...mie naona haya ni mazingaombwe tu maana mikataba hii ingekuwa imesainishwa na watu wa upande wa pili nafikiri kuna watu wangekuwa ndani mpaka sasa, ila Baba Tumsifu kajifanya hawajui waliotuumiza....
President ndio anaongoza baya ama zuri.. wabunge are nothing mkuu.. President huyu kaamua kufanya kivingine.
 
haki yangu sio kuvunja mikataba ya kimataifa na kusapoti ujinga ambao ni matokeo ya hao hao wanajifanya wamekua na uzalendo uliotukuka kumbe kiki tu wala hakuna jipya......wewe unakurupuka na kujifanya una uchungu na ujasiri sana wa kuipigania nchi yako bila hata kujua chanzo cha vita husika na maana halisi ya uzalendo
Nani kavunja mkataba? Kilichofanyika ni kusimamisha usafirishaji wa mchanga ili serikali ijihakikishie kiwango cha madini kilichomo kwenye concentrates.

Haikuwa kuvunja mkataba bali kuhakiki kama acacia hawakiuki makubaliano kwa kusafirisha kiwango kikubwa cha madini kwenye concentrates kuliko walichokubaliana.

Unatakiwa uelewe tofauti ya kuvunja mkataba na kuhakiki kama mkataba unatekelezwa ipasavyo
 
Sasa wewe ndugu yangu iwapo tayari umeonesha mwelekeo wako unaochagizwa ama na woga au hamadi kibindoni, utajipangaje pamoja na Watanzania wenye mwelekeo wa kizalendo? Kwa narratives ulizotoa kuhusu huyo role model wako zikiunganishwa na personal note yako, tayari mtu mwenye akili timamu anabaini kuwa unafungamana na Munk. You share ideology with Munk halafu unataka kushikamana na wanao-share ideology ya kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi yao! Wewe kula mkate wako. ila tukikughundua unatusaliti matokeo yake yanajulikana na wewe unayajua.
kwenda zako huko mbona mkapa alitusaliti ma badi yupo anadunda tu.
 
Nani kavunja mkataba? Kilichofanyika ni kusimamisha usafirishaji wa mchanga ili serikali ijihakikishie kiwango cha madini kilichomo kwenye concentrates.

Haikuwa kuvunja mkataba bali kuhakiki kama acacia hawakiuki makubaliano kwa kusafirisha kiwango kikubwa cha madini kwenye concentrates kuliko walichokubaliana.

Unatakiwa uelewe tofauti ya kuvunja mkataba na kuhakiki kama mkataba unatekelezwa ipasavyo
acha ujinga kuna dhana mbili hapa kutangaza kuvunja mkataba. na kukiuka mkataba ambako kimantiki ni kuvunja mkataba. hata kama hujadeclare
 
Wayahudi wamiliki wakubwa wa ACCACIA ni watu wa dini tofauti na akina mbowe na baraza lao kuu ambao Bia za Kilimanjaro ni kinywaji cha baraza kuu na akina tundu lisu . Wayahudi dhuluma iwe Ya kudhulumu nchi au mtu haina nafasi kwenye torati yao watasimama na magufuli. Management ya ACCCIA ijiandae kufungashwa virago wao na bodi yao
Unataka kuniambia kuwa Yesu aliuliwa na Wasambaa wa Mlalo?
 
Unataka kuniambia kuwa Yesu aliuliwa na Wasambaa wa Mlalo?
Walioua yesu sio wayahudi alihukumiwa kifo na mrumi ponsio pilato na askari wa kirumi ndio walimwuuua kwa kumgongomelea msalabani na kumchoma mkuki ubavuni. Walioua yesu ni warumi sio wayahudi.Usipotoshe historia kasome biblia uone Who actually killed Jesus.
 
WanaCCM,walikuwa wapi siku zote?Wakati akina Lisu na Zito wanapiga kelele Bungeni wanaCCM,wazalendo wa leo wanamapinduzi walikuwa wanazomea wamelikoroga wao,ubaya ni kwamba tutalinywa wote.Busara kwa wanaCCM,ni kunyamaza acha wazomewe maana wanastahili kuzomewa sasa.
 
Peter Munk (83), Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Barrick Gold Corporation, kampuni inayomiliki zaidi ya asilimia 60 ya Hisa za Acacia.
Alizaliwa November 8, 1927, Ni raia wa Canada, mfanyabiashara na mtoa misaada mashuhuri zaidi duniani . Munk ndie Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni kubwa zaidi ya madini duniani ya Barrick Gold Corporation .
Munk alizaliwa katika mji wa
Budapest, Hungary, katika familia ya kitajiri ya Wayahudi, kijana wa Katherine (Adler) and Louis L. Munk. Baada ya Hungary kuvamiwa na utawala wa Nazi wa Ujerumani chini ya Adolp Hittler mnamo Machi ,1944 Peter Munk alikuwa kijana mdogo wa umri usiozidi Miaka ishirini. Familia yake ilitoroka kupitia treni ya Kastner , Treni ambyo ilibeba wayahudi takribani 1,684 na kuwapeleka nchini Switzerland, mpango ulioratibiwa na Rudolf Kastner, Mhafidhina wa taasisi iliyojulikana kama Zionist Aid and Rescue Committee .
Taasisi hii ilitumika kuwatorosha Wayahudi kutoka Hungary kufuatia majadiliano na Afisa wa ngazi za Juu ya Ulinzi wa Hungary
Adolf Eichmann kwa kubadilishana fedha, dhahabu, almasi kwa kile kilichojulikana kama Mapatano ya damu na vito vya thamani ( "blood for goods" deals )
Munk alihitimu katika Chuo Kikuu cha
Toronto, Canada na kutunukiwa shahada ya electrical engineering mnamo Mwaka1952.
Mwaka 1958, Munk pamoja na wenzake walianzisha kampuni ya
Clairtone kwa usaidizi David GilmourFrank Sobey. Baada ya hapo, amekuwa na mafanikio na changamoto nyingi katika biashara zake.
Amewahi kuwa Mhadhiri katika Chuo kikuu James Gillies Alumni Lecture,
York University, Toronto. Amekuwa mjumbe katika bodi mbalimbali zikiwamo;

Pia Munk ni mjumbe wa heshima wa bodi ya taasisi ya Jewish National Fund (JNF) of Toronto, taasisi ambayo imekuwa na jukumu la kupora ardhi ya palestina na kuendeleza makazi ya Wayahudi kinyume na Azimio la Umoja wa Mataifa.
Taasisi hii ndio imekuwa kitovu cha ushirikino wa familia za Wahahudi wote ulimwenguni , ambapo moja ya jukumu lake kubwa ni kurudisha ardhi ya Israel iliyopotea kwa kuchangisha fedha na kununua ardhi kutoka kwa Palestine, kupanda miti, kujenga makazi na miundombinu mbalimbali.

Kutokana na uwezo, ushawishi na mafanikio yake, Munk amepata PHD za heshima katika Vyuo vikuu mbalimbali;

Kutokana na tuzo hizo, Munk anatajwa kuwa afisa ambaye anaheshimika zaidi nchini Canada
Pia ni mwanzilishi wa
Munk School of Global Affairs, kupitia mchano wa fedha kutoka taasisi yake ya Peter and Melanie Munk Foundation.
Note:
Kufahamu vizuri uwezo wa adui yako, inakupa fursa ya kutafakari njia bora zaidi ya kupambana nae. Ni wazi kabisa matumizi ya nguvu bila weledi hayatatuacha salama. Uzalendo wetu ujikite kuitumia elimu na maarifa yetu katika kupata tunachokitaka. Kutumia hoja za kijinga kwa kivuli cha Uzalendo ni hasara zaidi kwa kizazi cha leo na kesho. Kudhani kila anayeunga mkono kila jambo ndio Mzalendo bila kujali athari zake kwa Taifa ni nonsense. Tuungane katika msingi wa hoja zenye utetezi makini na si katika kelele, pongezi na vijembe. Kutumia jukwaa na kudai wale wanaotofautiana na Approach ya JPM wamehongwa au sio Wazalendo ni kikosa fikra, Kwamba kuhoji uhalali wa data za kamati ni kukosa Uzalendo. Tujipange katika hoja makini.
Acha kutufundisha uoga jombaaaaaa..
 
Umedadavua,, umezungumza vizuri,, hizo pesa wanazoiba na walizokwisha iba ndio walizokua wakitumia kuhakikisha CCM inaendelea kuwepo madarakani hata kwa bila ridhaa ya wananchi,, sasa basi ieleweke kua CCM wameibua vyanzo vingine vya mapato vinavyoweza kuwafadhili kwenye kila wizi wenye nia ya kuendelea kutawala,, CCM mpya inajengwa ambayo jeuri yake ime laydown foundation kwenye wiz,unyanyasaji, pamoja naukandamizaji wa haki..hayo yanayofanywa na serikali ni madhara ya usaliti naufedhuli.. Tutashuhudia mengi..!! bt kuna mengi tutayajua CCM ikiondolewa madarakani, hakuna marefu yasiyo kua na ncha.
 
Back
Top Bottom