Wakati Kenya wakigawa laptop kwa kila mwanafunzi, Tanzania tunahangaika na madawati

cantonna

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,120
439
KENYA YAANZA KUGAWA LAPTOP KWA WANAFUNZI

Kuanzia 3/5/2016 Kenya ilianza kutekeleza mpango wake wa kugawa laptop kwa wanafunzi wote nchini mpango huo umedhamiria kugawa laptop 600,000 mpaka kufikia mwezi Juny mwaka huu.

Wenzetu wakenya wakiwa na mkakati wa kuhakikisha angalau shule zote za msingi zenye miundo mbinu bora hasa ya umeme, wanafunzi wapatiwe laptop ili kuweza kuinua taaluma lakini Tanzania ya Mzee wa hapa kazi tuu yenyewe bila haya inatembeza bakuli la kuomba madawati ama kweli hii na aibu. Madawati utata kutoa Laptop kwa wanafunzi kama Kenya itawezekana? Kweli aibu.
6e25fffcfde78846841d76922b2db5a3.jpg
87537f02064cac5baf3c8ca2ad148239.jpg
b7746777c14d822621fc854eb9895104.jpg
 
Utasikia
madawati saaaaaafiiiii........
Madawati hoyeeeeeeeee......
Kukaaa saaaafiiiii.........
Tupige vigelegele na makofi tushangiliee!!!
Vituko Tz haviishi!!
Wanaandalia hadi na sherehe kabisa....wakuu wa mikoa no mwendo wa kuuza nyago mitandaoni eti wanakabidhiwa madawati!!!
 
Tusemage yote wala tusikwepe ukweli kuwa nchi ni masikini na vipaumbele vyetu sio lazima vifanane na vile vya Kenya ambao hata kiuchumi wako mbele yetu kidogo. Juhudi zilizofanywa na serikali zilizopita si za kubeza pia. Wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini tunayajua maumivu ya kukosa umeme na barabara kwa miaka 50 iliyopita, ambayo yamepunguzwa saaana na serikali ya JK. Sasa zingekuja hizo laptop zingewashiwa nini? Ni kweli hatukuwa na madawati, lakini yapo yaliyofanyika.
 
Back
Top Bottom