Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,765
- 36,354
Habari!
Siku moja kwa makusudi kabisa nikaamua kuwa mkaksi, nikasema nitanunua nyama kwenye duka(bucha) lenye mizani iliyo kamili kabisa.
Nikaanza duka la kwanza nikakuta upande wa kuwekea mawe kuna jiwe la nusu kg. Nikamuuliza muuzaji, "Hili jiwe la nini ilhali mizani iko free haina nyama" akasema kaweka tu. Nikalitoa hapohapo mzani ukaangukia upande wenye sahani ya kuwekea nyama. Hapa maana yake mzani hauko sawia. Sikununua nyama.
Nikaenda duka la pili, nikakuta kuna jiwe limewekwa upande wa kuwekea mawe huku mzani hauko kwenye upimaji. Nikamuuliza muuzaji hili jiwe la nini ilhali mizani iko free haina nyama akasema kaweka tu kutunza mizani. Nikalitoa hapohapo mzani ukaangukia upande wenye sahani ya kuwekea nyama wakati wa kupima kabla hata hakijawekwa kitu. Nikamwambia huniuzii Mimi nikaenda sehemu nyingine ya tatu.
Nikakutana na mauzauza mengine kidogo, sahani ya kuwekea nyama wakati wa kupima imewekwa mifupa. Na hii sahani mara nyingi wanaiseti upande ambao mnunuzi hasimami ili wakikutilia nyama mifupa iongeze uzito kidogo.
Nikaenda duka la nne nikakutana na mauzauza kama yale ya duka la kwanza na la pili. Nikaenda maduka kadhaa vivyohivyo.
Serikali ipige marufuku hizi mizani za kizamani, pia serikali (Wakala wa Vipimo) wasiishie kukusanya pesa tu kupitia kupiga muhuri mizani bali wafanye kazi yao kuu ya kumlinda mlaji asipunjwe.
Binafsi naona ni heri kununua nyama kwenye mabucha ya kisasa na supermarket ambako hakuna kupunjana. Hawa wauzaji wa mitaani hawana utu, washazoea unyonyaji.