Wizi wa nyama katika mabucha ya Kigamboni Ferry

The Saver

JF-Expert Member
Aug 21, 2014
202
650
WanaJF wa kigamboni

Naomba niwape mkasa ulionipata najua BUTCHER nyinyi za nyama wanaiba mwingine karibia 50gm, 100gm, hata 200gm. Kwa KIGAMBONI FERRY kuna Butcher kama 4 au 5 kama sijakosea.

Katika butcher hizo nimewai kununua kwenye butcher 2 na zote nimeibiwa.

BUTCHER ya kwanza nilienda kununua 2kg kufika nyumbani mama akaniambia hii sio 2kg

Nikarudi baada ya wiki mbili kununua tena 2kg kufika nyumbani kupima 1.5kg

Wiki iliyopita nikaenda kwenye butcher ya pili nikanunua 3kg alipomaliza kupima akanikatia nikamwambia toa sahani zote kwenye MZANI WAKE WA DIGITAL pima tena, kupima ikasoma 2kg 600g

WIZI HUU WA KIGAMBONI FERRY UNAFANYIKA HIVI

Wote wanatumia mizani ya DIGITAL anakuwa na visahani viwili vya kupimia nyama vya kuwekea juu ya mzani wa digital, kisahani kimoja kipo sawa kingine ndio kina uzito wa 400g mpaka 500g

ONYO: WANAKIGAMBONI NAJUA MKIWA MNATOKA MAKAZINI POSTA NA KWINGINEKO MNAPITIA KITOWEO PALE FERRY KUWENI MAKINI
 
Ukiingia kwenye mzani unakuta kisahani cha kawaida ambacho hakina uzito anakufanyia setting mzani usome 0.00 lakini akianza kupima anaweka kwenye kisahani kile KIZITO ndo anakupiga hapo
Sasa hiyo si direct kabisa unaona utofauti boss wangu. Acha tupite kwenye hizo duka tuone wanavofanya. Ziko sehemu gani? Maana npo mitaa hii nitoe ripoti.
 
Yani karibia wote wanao tumia kilo wanaiba
Hawa dawa yao ni moja Ukifika cha kwanza ni mkwara utaona kabisa akikupimia anakuzidishia kumbe ndio kakupa kamili
Mimi huwa nawaambia kabisa ukishapima silipi kwanza mpaka tukahakiki kwenye mzani mwingine usio wa buchani
 
dawa nenda na mzani wa kutundika.ila mabucha yata kukataa
images.jpeg-7.jpg
 
Cha muhimu akishaweka hicho kisahani kabla ya kuweka nyama bonyeza mwenyewe 'tare" au "zero" kwenye huo mzani alaf mwambie aanze kuweka nyama.
Atanuna lakn ndo njia pekee ya kuhakiki mzani uko zero
 
Awap hapo unapigwa coz akiinyanyua akiweka tena mzani lazma usome na Uzito wa kisahani mkuu😅😅😅
 
WanaJF wa kigamboni

Naomba niwape mkasa ulionipata najua BUTCHER nyinyi za nyama wanaiba mwingine karibia 50gm, 100gm, hata 200gm. Kwa KIGAMBONI FERRY kuna Butcher kama 4 au 5 kama sijakosea.

Katika butcher hizo nimewai kununua kwenye butcher 2 na zote nimeibiwa.

BUTCHER ya kwanza nilienda kununua 2kg kufika nyumbani mama akaniambia hii sio 2kg

Nikarudi baada ya wiki mbili kununua tena 2kg kufika nyumbani kupima 1.5kg

Wiki iliyopita nikaenda kwenye butcher ya pili nikanunua 3kg alipomaliza kupima akanikatia nikamwambia toa sahani zote kwenye MZANI WAKE WA DIGITAL pima tena, kupima ikasoma 2kg 600g

WIZI HUU WA KIGAMBONI FERRY UNAFANYIKA HIVI

Wote wanatumia mizani ya DIGITAL anakuwa na visahani viwili vya kupimia nyama vya kuwekea juu ya mzani wa digital, kisahani kimoja kipo sawa kingine ndio kina uzito wa 400g mpaka 500g

ONYO: WANAKIGAMBONI NAJUA MKIWA MNATOKA MAKAZINI POSTA NA KWINGINEKO MNAPITIA KITOWEO PALE FERRY KUWENI MAKINI
Na wanatufanyia hivyo kwasababu wanajua tukishuka kwenye pantoni tunakuwa na haraka tunakimbilia daladala
 
Hakuna kunyanyua. Akishakiweka, unabonyeza tare then ndo ananza kuweka nyama hapo juu..
In case akikinyanyua alaf akabonyeza zero, akikirudisha tu, mzanu utasoma hizo gram unless ukae kiboya akirudishe with nyama
 
Sasa hiyo si direct kabisa unaona utofauti boss wangu. Acha tupite kwenye hizo duka tuone wanavofanya. Ziko sehemu gani? Maana npo mitaa hii nitoe ripoti.
Ukishuka kwenye PANTONI KUNA BUTCHER mbili mwanzon pale ndio shule ya Wizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom