Wakala wa Shetani

Wakala wa Shetani

Wakala wa Shetani - 15.............


Baada ya kusema vile, msaidizi alitoka kumfuata mtoto na kubakia daktari Mzungu ambaye aliendelea kumdodosa mgonjwa.
“Eti mama umetokea sehemu gani?”
“Kabla sijakujibu naomba unieleze hapa ni wapi na nimefikaje?”
SASA ENDELEA...

“Ooh vizuri mama, hapa ni kituo cha watumishi wa kiroho, tupo kwa ajili ya kutoa misaada kwa watu wa maeneo ya karibu kielimu na kiafya. Taarifa zako tumezipata kutoka kwa wasamaria wema waliokuwa wakipita porini na kukuta ukiwa umepoteza fahamu, ilibidi tuwatume vijana wetu ambao walikuchukua na kukuleta hapa.
Baada ya kukufanyia uchunguzi haukuwa na tatizo kubwa zaidi ya njaa na uchovu wa kuonekana umetembea kwa muda mrefu bila kupumzika na pia ulikuwa hajapata chakula cha kutosha, kitu kilichofanya mwili ukose nguvu na kukufanya upoteze fahamu.
Nina imani umenielewa vizuri, una swali lingine?” daktari alimuuliza kwa sauti ya faraja.
“Ooh, asanteni sana Mungu aendelee kuwabariki.”
“Amen, mh! Nini kimekusibu mpaka kuwa katika hali hii?”
Ngw’ana Bupilipili kabla ya kujibu alivuta kumbukumbu jinsi alivyonyanyasika kwa ajili ya kujifungua mtoto albino na kifo cha mumewe huku akishangaa jinsi mwanaye alivyopewa huduma nzuri bila kubaguliwa kwa jinsia au rangi yake.
Bila kutegemea machozi yalianza kumtoka, mdomo ulikuwa mzito kutoa matamshi. Daktari alishtushwa na hali ile na kumfanya aamini lazima yule mama atakuwa na tatizo zito. Kabla hajanyanyua mdomo wake kutamka kitu. Mara mlango ulifunguliwa, akaingia yule msaidizi akiwa amempakatia mtoto.
Ngw’ana Bupilipili alitaka kunyanyuka kitandani baada ya kumuona mwanaye akiwa hai. Baada ya kupewa mwanaye alijikuta akimtazama mara mbilimbili huku akimgeuza kwa kumuangalia kama yupo sawa.
Baada ya kupata uhakika yupo sawa alimnyonyesha, mtoto akalidaka ziwa la mama yake na kunyonya kwa fujo kutokana na njaa kali.
Daktari na msaidizi wake walitabasamu kwa pamoja huku wakifurahia mtoto alivyofurahia ziwa la mama yake. Daktari hakutaka kumsumbua sana, alimwacha amnyonyeshe mtoto na kumuachia maagizo msaidizi wake.
“Pamela, baada ya kumaliza kunyonyesha mgonjwa apewe chakula, apate maji ya kuoga kisha apumzike, jioni nitakuwa na mazungumzo naye, anaonekana ana kitu kizito moyoni mwake.”
“Sawa dokta.”
Daktari alitoka na kumuacha msaidizi wake ameketi kwenye kiti kusubiri amalize kunyonyesha mtoto na kumpa huduma alizopangiwa.
***
Ngw’ana Bupilipili aliishi pale kwenye kituo cha kiroho na mtoto wake ambaye alikutana na watoto wengine wenye ulemavu wa ngozi. Hali ile ilimpa faraja kubwa na kuamini kijijini kwao imani za ushirikina ndizo zilizotawala na kuwafanya kila kukicha wamkosee Mungu.
Pamoja na kukaa pale kwa amani, moyo wake ulikuwa ukiumia kila alivyofikiria kifo cha mumewe na mali walizoziacha kijijini. Alijikuta akiapa lazima alipe kisasi cha kifo cha mumewe na mtoto wao wa kwanza albino aliyeuawa kwa imani za kishirikina.
Kila kukicha alikuwa akibuni njia ya kulipa kisasi kwa wanakijiji waliosababisha yote yale. Siku moja akiwa anafanya usafi kwenye stoo aliona pakiti ndogo iliyokuwa imeanguka chini na kumwaga unga mweupe chini.
Aliiokota na kutafuta sehemu ya kuiweka, wakati huo Sister Lucy alikuwa akiingia stoo na kushtuka kumuona Ngw’ana Bupilipili ameshika pakiti ile tena bila ‘gloves’ mkononi. Alionekana kushtuka sana.
“Mama Kusekwa kwa nini unashika dawa hiyo bila gloves?”
“Nimeikuta hapa chini ndio nilikuwa natafuta sehemu ya kuiweka.”
“Hii ni sumu, ukiiweka mdomoni utakufa dada yangu.”
“Sumu?”
“Eeh.”
“Mungu wangu, kama ni sumu inafanya nini humu ndani?”
“Si sumu kwa maana imetengenezwa kuua watu, ni dawa ya kuua wadudu katika mitaro, mashimo ya maji hata wadudu warukao na watambaao.”
“Sasa inakuwaje unasema sumu kumbe dawa ya kuulia wadudu?”
“Mama Kusekwa, hii ni dawa lakini ukiitia mdomoni inageuka sumu na kukudhuru.”

Itaendelea Jumamosi ijayo....
 
jumamosi jumamosi ndio nini sasa as if imekuwa gazeti la udaku ndio tununue???
mzizimkavu bwana haya wekend njema
 
Wakala wa Shetani - 16..

“Mungu wangu, kama ni sumu inafanya nini humu ndani?”
“Si sumu kwa maana imetengenezwa kuua watu, ni dawa ya kuuwa wadudu katika mitaro na mashimo ya maji hata wadudu warukao na watambaao.”
“Sasa inakuwaje unasema ni sumu kumbe ni dawa ya kuulia wadudu?”
“Mama Kusekwa, hii ni dawa lakini ukiitia mdomoni inageuka sumu na kukudhuru.”
SASA ENDELEA...

“Mmh, sawa.”
“Tena dawa hii kama utakumbuka kuna mwaka mtu mmoja aliiweka kwenye tanki la maji na kuua familia nzima.”
“Mmh! Sasa inakuwaje mtu aweke kwenye tanki la maji wafe watu wengi, kwani ina nguvu gani isiyopungua katika maji mengi?”
“Hii ni sumu kali sana ndio maana nikashangaa kukuona umeishika kwa mkono. Unatakiwa kunawa vizuri na sabuni mikono yote na kuhakikisha unakuwa msafi kabla ya kumshika mtoto wako.”
“Nashukuru Sister Lucy. Basi ningetoka hapa ningepewa embe mimi ningekula tu bila kujua kama nina sumu mkononi.”
“Basi kuanzia leo unatakiwa kuvaa gloves kabla ya kupanga vitu vya humu ndani.”
“Nitafanya hivyo, hivi kama ukiitia dawa hii kwenye lambo la kijijini si unaweza kuua watu wengi?”
“Tena usiombe kufanya kitu kama hicho, na dawa hizi hupatikana sehemu kama hizi madukani hazipo kwani ni kali sana, zinaua mara moja.”
Baada ya maelezo yale Ng’wana Bupilipili alikwenda kunawa kwa sabuni na kisha aliendelea na kazi yake.

***
Jioni ya siku ile akiwa amejilaza kitandani kwake, wakati huo mwanaye akiwa anaendelea kufaidi ziwa tamu la mama yake, alijikuta akikumbuka maneno aliyokuwa akizungumza na Sister Lucy kuhusu ukali wa ile dawa ya kuulia wadudu kuwa ni sumu kali kama mwanadamu atainywa.
Aliamini kupitia sumu ile itakuwa njia nyepesi ya kulipa kisasi, alijua akienda kuiweka katika chanzo cha maji ambayo hutumiwa na wana kijiji lazima ataua watu wengi.
Alijikuta akiwachukia watu wote wa kijiji cha Nyasha kwa kuamini kila aliyetoka katika dawa ya wauaji nao walitakiwa kuipata hukumu ile kwa kuamini kama wao walifurahia vifo vya watoto wenye ulemavu wa ngozi basi nao watoto hao nao watafurahi kusikia mauti yao.
Alijikuta akiapa lazima alipe kisasi tena kikubwa na kuacha historia ya vifo vya watu wengi. Alipanga siku ya pili akiingia kufanya usafi achukue paketi nne za sumu ambazo zote ataziweka katika vyanzo vya maji ya Kijiji cha Nyasha.

***
Siku ya pili akiwa anafanya usafi stoo alichukua paketi nne za dawa ya kuulia wadudu na kuificha kwenye kanga. Baada ya usafi alitoka nayo na kwenda kuificha chumbani kwake.
Baada ya kuipata ile dawa alipanga siku moja ataondoka kwenye kambi ile saa kumi za usiku kwenda Kijiji cha Nyasha.
Baada ya kujipanga na kuipanga siku ya kwenda kulipa kisasi, alimtaarifu shoga yake wa karibu kuhusu safari yake lakini alimdanganya kuwa anafuata vitu vyake.
Baada ya kukubaliana siku ya pili majira ya saa kumi za usiku Ng’wana Bupilipili aliamka na kwenda kumuamsha shoga yake ambaye alikuwa amelala.
“Vipi, safari imeiva?”
“Eeh, shoga, niangalizie mwanangu,” alimpa mtoto wake aliyekuwa bado na usingizi.
Shoga yake alimchukua na kumuingiza ndani na kumlaza kitandani kisha alitoka ili amuage.
“Basi shoga safari njema.”
“Nashukuru shoga, Mungu akijalia tutaonana.”
Ng’wana Bupilipili kabla ya kuondoka aliingia chumbani kwa shoga yake na kumnyanyua mtoto wake kitandani na kumkumbatia kwa uchungu huku machozi yakimtoka. Hali ile ilimshtua shoga yake na kuhoji kulikoni.
“Vipi mbona unalia?”
“Basi acha tu, nimekumbuka vitu vingi hasa baada ya kukumbuka kifo cha mume wangu na leo narudi hukohuko.”
“Kama ni hivyo kwa nini unakwenda tena?”
“Hapana kuna vitu vyangu vingi na vya muhimu sana lazima niende.”
“Sasa utaingiaje pale kijijini?”
“Hapana siendi nyumbani nitaishia shambani kwetu.”
“Unajuaje kama shamba bado lipo mikononi kwenu?”
“Yote nitayajua huko huko.”
“Basi bwana akutangulie safari yako yote.”
“Amen.”
Alimrudisha mtoto kitandani baada ya kumbusu, alimgeukia shoga yake na kumkumbatia kabla ya kugeuka na kuondoka kuwahi safari yake ambayo aliamini mpaka saa mbili asubuhi atakuwa Kijiji cha Nyasha.
Hakutokea mlango wa mbele, aliruka ukuta kuogopa kuulizwa na mlinzi anakwenda wapi. Baada ya kufanikiwa kutoka salama nje ya kambi alianza safari kuelekea Kijiji cha Nyasha moyoni akiwa na dhamira nzito ya kuwa tayari kupambana na lolote litakalotokea mbele yake.


Itaendelea wiki ijayo.
 
Wakala wa Shetani - 17-

Katika kijiji cha Nyasha ilikuwa siku ambayo iliwachanganya watu wengi baada ya kila nyumba kulalamikia tatizo la tumbo. Hospitali zilijaa wagonjwa ambapo wengi walipoteza maisha. Ilibidi taarifa zifike haraka mkoani na kutumwa timu ya wataalamu kuja kufanya uchunguzi.

Ilionesha watu wa kijiji kile wamekunywa sumu iliyokuwa kwenye maji, mifugo yote ilikufa na kufanya kijiji kiwe katika janga zito la maafa ya watu na mifugo. Ilibidi wagonjwa wote wahamishiwe mjini lakini wengi walifia njiani.


SASA ENDELEA...


KaYA nyingine zilipoteza familia nzima na nyingine zilipoteza zaidi ya watu watatu.
Mara moja watu wa Kijiji cha Nyasha walipigwa marufuku kunywa maji yote, uchunguzi ukaanza kufanywa ambapo ilibainika kuwa vyanzo vyote vya maji vilikuwa na sumu.
Ilibidi iletwe dawa na kuondoa sumu katika sehemu zote zenye vyanzo vya maji lakini wakati huo Kijiji cha Nyasha kilikuwa na msiba mzito wa kupoteza nusu ya wanakijiji.
Taarifa za msiba mzito uliowakuta wanakijiji wa Nyasha zilimfikia Ngw’ana Bupilipili ambaye alijawa na furaha kuamini mpango wake umefanikiwa. Pamoja na kufanikiwa kuua watu wengi, bado dhamira yake ilikuwa haijatimia. Alipanga kukifanya kijiji kile kiwe cha historia kwa kuwamaliza wanakijiji wote na kubakiza magofu.

***
Baada ya kufanikisha zoezi la awali la kukiteketeza Kijiji cha Nyasha, Ngw’ana Bupilipili aliendelea na mchezo wake ule, kila hali ilipotulia alikwenda kuweka sumu kwenye maji. Hali ile ilikiweka Kijiji cha Nyasha kwenye mashaka na kuamua kufanya uchunguzi wa kina juu ya nani anayefanya mchezo huo.
Makachero toka serikalini walianza uchunguzi wa siri bila mtu yeyote kujua. Walilinda kwa saa 24 vyanzo vyote vya maji kwa kubadilishana kufuatilia mtu aliyekuwa akisababisha mauaji ya wanakijiji cha Nyasha.
Ngw’ana Bupilipili kama kawaida yake baada ya mambo kutulia alirudi tena kwenye Kijiji cha Nyasha kuendeleza hukumu yake ya kuhakikisha anakisafisha kijiji chote.
Kurudi kijiji pale ilikuwa mara ya nne, kama kawaida alimuaga shoga yake na kumuachia mwanaye Kusekwa aliyekuwa ametimiza miaka miwili.
Alitembea katika mbuga kama ilivyo kawaida yake, kwa vile alikuwa ameshakuwa mzoefu, hakuwa na hofu tena ya kutembea mbugani peke yake. Kutokana na uzoefu alikuwa akitoka usiku zaidi ili alfajiri imkute ameshamaliza kazi yake.
Baada ya mwendo wa saa tatu bila kupumzika, aliingia Kijiji cha Nyasha kukiwa bado na giza, hakukuwa na mtu yeyote. Alijisifu kuondoka mapema kwa kuamini atamaliza kazi zake bila mtu yeyote kumuona.
Baada ya kuangalia usalama wa eneo lile na kuona hakuna tatizo, aliifungua ile sumu na kuitia kwenye chanzo cha maji kisha aliifunga na kuelekea kwenye kisima cha akina mama. Wakati akifanya vile walinzi wa eneo lile walikuwa bado hawajamuona.
Wakati anataka kuondoka eneo lile askari mmoja alishangaa kumuona mwanamke akitokea kwenye chanzo cha maji.
“Hey, wee mama unafanya nini alfajiri hii?”
“Nakwenda shamba,” Ngw’ana Bupilipili japo alikuwa katika mshtuko mkubwa lakini alijitahidi kujibu kwa kujiamini.
“Shamba, mbona majibu yako yana utata, unakwenda shamba gani ikiwa mashamba hayapo eneo hili?”
“Achana naye bwana, si unajua tumemaliza lindo salama,” alisema mlinzi mwingine.
“Haya potea hapa.”
Ngw’na Bupilipili alimshukuru Mungu kumuepusha na watu wale, ndipo alipofumbuka macho kuwa sehemu ile ina ulinzi. Aliteremka kuelekea bondeni kwa kuhofia kugeuza lazima wangemtilia wasiwasi.
Aliamua kutafuta njia nyingine ya kumuokoa kwa kuondoka eneo lile ambalo aliamini limezungukwa na ulinzi mzito. Alitembea kwa tahadhari akipita pembeni kutafuta njia ya kutokea nje ya Kijiji cha Nyasha.
Askari mmoja alimuona Ngw’ana Bupilipili akitembea kwa mashaka na kuamua kumfuatilia taratibu. Baada ya mwendo mfupi alikutana na sehemu kubwa iliyokuwa imetengeneza kama bwawa.
Alipoiangalia sehemu ile ilimuonesha kabisa watu huchota maji. Akili yake ilimtuma sehemu ile vilevile inatakiwa kuwekwa sumu. Kwa tahadhari kubwa alitoa paketi ya dawa ya kuulia wadudu na kuanza kuinyunyizia kwenye maji yake.
Askari aliyekuwa akimfuatilia alimshangaa na kujiuliza yule mwanamke ananyunyiza nini kwenye yale maji.
Hakutaka kumshtua alimsogelea taratibu mpaka alipokuwa na kusimama nyuma yake bila Ngw’ana Bupilipili kumuona. Baada ya kuimiminia ile dawa iliyobaki aliirudisha kwenye paketi yake kisha aliifunga kwenye mfuko wa plastiki na kuiweka katika mfuko wa kaptura aliyokuwa amevaa.
Wakati anavua gloves ndipo yule askari alipomshtua.
“Unafanya nini?”
Ngw’ana Bupilipili alishtuka na kuanza kutimua mbio, lakini hakufika mbali alikamatwa.



Itaendelea wiki ijayo.
 
Wakala wa Shetani -18-

Daktari Father Joe alipoingia ndani alimkuta Ng’wana Bupilipili akiwa amejilaza kitandani. Lakini aliamini kabisa mlalo ule si wa mtu kupoteza fahamu bali wa usingizi wa kawaida. Akiwa bado hajapata jibu juu ya kuwa katika hali ile alimgeukia msaidizi wake Sister Marry.
SASA ENDELEA...


“Eti sister nini kilichomtisha na kumfanya akimbie na kuanguka kisha kupoteza fahamu?”
“Kwa kweli mpaka sasa hatujajua ila niliambiwa alitoka mara moja.”
“Alikuwa amekwenda wapi?”
“Mmh, hapo sijui ngoja tutamuuliza mwenyewe akipata fahamu.”
Ng’wana Bupilipili alizifahamu vizuri sauti za Father Joe na Sister Marry hali iliyomfanya ashushe pumzi kwa kuamini yupo sehemu salama. Alijifanya kujigeuza kitu kilichowafanya wasogee kitandani. Sister Marry akamwita:
“Mama Kusekwa... Mama Kusekwa.”
“Abee,” aliitika na kujinyoosha.
“Vipi unajisikiaje?” Sister Marry alimuuliza kwa sauti ya upole.
“Mmh, sijambo kiasi,” alijibu huku akifumbua macho.
“Eti tatizo nini?”
“Nilikuwa natoka kutafuta baadhi ya vitu vyangu nilivyoviacha porini wakati nakuja, ndipo nilipokutana na mnyama mkali aliyeanza kunifukuza, kwa kweli nilikimbia kwa nguvu zangu zote.
“Sikumbuki kilichoendelea na kujikuta nipo hapa,” Ng’wana Bupilipili alitengeneza uongo unaofanana na ukweli.
“Ooh, pole sana.”
“Asante.”
“Hakukujeruhi?” Father Joe aliuliza.
“Sidhani najiona nipo salama ni maumivu madogomadogo ambayo sijui ni ya nini.”
“Unaweza kwenda chumbani kwako, kama utasikia tatizo lolote mwilini mwako utatujulisha.”
Ng’wana Bupilipili alinyanyuka kitandani na kutembea kwa kuchechemea kwa muda kisha alitembea kawaida. Alikwenda hadi chumbani kwake na kujilaza bila kumfuata mtoto kwani hakuwa na mawazo ya mwanaye zaidi ya kujifikiria jinsi alivyookoka katika mikono ya askari waliokuwa wakilinda chanzo cha maji.
Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa huenda wakafanya msako na kwa vile askari yule ameshaiona sura yake, lazima angemtafuta na kumpata. Aliamini katika msako wao lazima wangefika kwenye ile kambi na lazima angemtambua na kumkamata.
Ng’wana Bupilipili aliamini kabisa kwa upande wake muda ule kwake kuwepo pale kambini hakufai, kwa kuamini wakimkosa porini lazima watamtafuta kwenye kambi ile.
Wazo lake kubwa lilikuwa ikifika usiku atoroke na mwanaye na kutimkia sehemu asiyoijua japokuwa alijua ni hatari, lakini aliamini bora akafie mbele kuliko kukamatwa na kuhukumiwa kifo.
Hata shoga yake alipoingia hakumuona kwa vile alikuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo.
“Shoga nakuona upo mbali vipi umeumia sana?”
“Walaa, kawaida tu.”
“Mh! Za huko?”
“Shoga mbona yamenikuta leo makubwa.”
“Yapi hayo?”
“Kidogo leo nishikwe na askari waliokuwa wakilinda vyanzo vya maji.”
“Vyanzo vya maji?”
“Eeh, japokuwa nilikuwa sijakueleza ukweli wa safari yangu, kwa vile wewe umekuwa mtu wangu wa karibu na muhimu sana lazima nikueleze ukweli hata nikishikwa ujue tatizo langu.”
“Ushikwe kwa kosa gani tena?” shoga yake alishtuka.
“Tulia basi nikueleze usiwe na pupa na nitakachokueleza naomba ibakie siri yako.”
“Hakuna tatizo shoga.”
Ng’wana Bupilipili alimueleza yote aliyoyafanya baada ya kufiwa na mume wake na ahadi ya kisasi aliyoiweka ya kukisambaratisha Kijiji cha Nyasha, siku ile jinsi alivyokamatwa na askari na kufanikiwa kumtoroka. Shoga yake Bupe hakuamini alichoelezwa na Ng’wana Bupilipili na ujasiri aliouonesha wa kutimiza dhamira yake.


Itaendelea wiki ijayo.
 
[h=1]Wakala wa Shetani - 19-[/h]
NG'WANA Bupilipili alimueleza yote aliyoyafanya baada ya kufiwa na mume wake na ahadi ya kisasi aliyoiweka ya kukisambaratisha Kijiji cha Nyasha.
Siku ile jinsi alivyokamatwa na askari na kufanikiwa kumtoroka. Shoga yake Bupe hakuamini alichoelezwa na Ng'wana Bupilipili na ujasiri aliouonesha wa kutimiza dhamira yake.
SASA ENDELEA...


"Mmh, nimekusikia, nakupa hongera, wewe ni mwanamke wa shoka kwa yote uliyofanya. Huna kosa shoga kwani ulichokifanya ni sawasawa, kuwatia adabu mashetani wale.
"Sijui kwa nini hukuniambia na mimi nikusindikize, hata mimi nina kisa changu kizito sikuwahi kukueleza na sababu ya mimi kufika hapa."
"Kisa gani hicho shoga?"
"Kwa vile wewe umeniamini na kunipa siri yako nzito, nami sina budi kujiweka wazi kwako. Mimi nilikuwa nimeolewa katika Kijiji cha Ng'wana Nsimba, Shinyanga vijijini na mume aliyekuwa na mali ya wastani.
"Kwa bahati mbaya mume wangu alifariki, ndugu walinidhulumu mali zote na kuonekana sina thamani mbele ya watu. Kwa kweli roho iliniuma kwa vile tangu nilipoolewa nilikuta ng'ombe ishirini tu, kwa vile sikutaka mume wangu apate shida, katika ng'ombe zangu sabini za mahari nilichukua 40 na kuzichanganya na za mume wangu.
"Kwa miaka minane zizi lilikuwa na ngombe mia nne ishirini. Kwa bahati mbaya mume wangu alifariki, ndugu wakanifukuza kama mbwa, hata nilipoomba ng'ombe zangu 40 walininyima. Sikutaka kubishana nao, niliondoka na kurudi nyumbani na wanangu wawili.
"Nikaapa kuwashikisha adabu japokuwa walinidhihaki na kuniona siwezi kufanya kitu chochote kwa vile waliamini wanawake ni viumbe dhaifu.
"Moyoni nilipanga pigo zito, ndipo siku moja niliwavizia wamelala na kutia moto nyumba zao za nyasi kwa kuanzia milangoni. Kwa vile nyumba nyingi za vijijini za nyasi madirisha yake ni madogo, walikosa pa kutokea, nikaiteketeza familia yote ya marehemu mume wangu.
"Siku ya pili taarifa zilizagaa juu ya vifo vya familia ya mume wangu, sikutaka kuitwa kutoa ushahidi kutokana na kutoa maneno makali siku waliyonidhulumu mali zangu.
"Niliamini mtu wa kwanza nitakuwa mimi, basi nilitoroka bila mtu yeyote kujua na kutembea kwa miguu kwa muda wa siku tatu, usiku nililala na asubuhi niliendelea na safari zangu.
"Ndipo siku moja nilipotokea mbele ya kambi hii nikiwa nimevimba miguu kwa kutembea. Kwa kweli watu wa hapa kwa ukarimu waliniokota na kunitibu kisha walinitunza mpaka leo hii.
"Najua walinitafuta nami nilijificha huku, sijui nitatoka lini kwa vile najua nikionekana kijijini kwetu nina kesi ya mauaji. Basi mdogo wangu matatizo yetu yanafanana na kisasi chetu kinafanana japo wewe ulidhamiria kufyeka kijiji kizima na mimi nilitimiza nadhiri yangu ya kuipoteza familia yote.
"Japo ni dhambi lakini namshukuru Mungu kuniwezesha kulipa kisasi, hata leo nikifa nitakuwa nimekufa bila kinyongo. Kwa kweli sikushangai kwa hatua uliyochukua, kisasi ni hapahapa dunia kwa Mungu hesabu, naamini hata uliowaua umelipa kisasi kwa kiasi kikubwa," Bupe alisema kwa hisia kali zilizomkumbusha donda na maumivu ya moyo.
"Mmh! Umeona dada watu walivyo na roho za kikatili kuliko wanyama? Ni kweli kabisa kisasi duniani kwa Mungu hesabu."
"Umeona eeh!"
"Ila shoga kuna kitu kinanichanganya sana akili yangu."
"Kitu gani tena?"
"Wasiwasi wangu huenda wale askari wakaendesha msako mkali, wakinikosa porini lazima watafika huku. Heri ningekuwa nimewaua wanakijiji tu msako wake usingekuwa mkali lakini nimewaua baadhi ya askari waliopiga mswaki asubuhi kwenye mto ule.
"Hawawezi kukubali kirahisi, lazima watanisaka kwa udi na uvumba, wakinikosa porini watakuja kunitafuta hapa na lazima watanikamata."
"Sasa ulikuwa na wazo gani?"
"Nitoroke."
"Uende wapi?"
"Nitokemee zangu mbele kwa mbele huku nikimlinda mwanangu na wanyama wakali."
"Kwa nini usibakie ili siku wakija ujifiche usijitokeze?"
"Mmh, hiyo itakuwa yamkini, hujui wana ujuzi gani katika kusaka wahalifu, wanaweza kunikamata kama kuku wa mdondo, shoga niache nitokomee zangu Mungu anajua majaliwa yangu na mwanangu."
"Sema tu wasiwasi wako, basi wakipita hao watu urudi sidhani kama watarudi mara mbili."
"Sawa shoga."
"Sasa kwa nini usimuache Kusekwa ili uende peke yako? Si unajua jinsi pori linavyotisha hasa usiku huu."
"Hapana shoga huenda hii ni safari yangu ya mwisho, hivyo siwezi kumuacha mwanangu japokuwa kiza cha nje kinatisha pia hatufahamu tunakwenda wapi. Ila tuombee kwa Mungu atulinde ili tuonane tena."
Je, nini kitafuatia? Usikose wiki ijayo.
 
[h=1]Wakala wa Shetani -20-[/h]
"Hapana shoga huenda hii ni safari yangu ya mwisho, hivyo siwezi kumuacha mwanangu japokuwa kiza cha nje kinatisha pia hatufahamu tunakwenda wapi. Ila tuombee kwa Mungu atulinde ili tuonane tena."
SASA ENDELEA...


"Yaani huwezi amini moyo wangu umekuwa mzito kwa nini usiahirishe kuondoka usiku huu, uondoke asubuhi?"
"Hapana shoga, niamuapo kitu siwezi kukisitisha, niache niondoke nitarudi baada ya siku mbili. Nina imani huenda asubuhi ya kesho wakaingia hapa."
"Mmh sawa, nakuombea safari njema na Mungu akutangulie kwa jambo lolote."
"Amen."
Bupe alimuacha Ng'wana Bupilipili apumzike kwa ajili ya safari yake ya usiku wa manane.

***
Baada ya tukio la kushtukiza la vifo vya askari watatu waliokuwa wakilinda na kutoroka kwa mtuhumiwa, jeshi lilijipanga upya kumsaka mtuhumiwa kwa kuagizwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kumsaka muuaji ambaye alionekana ni mzoefu tena mtu hatari.
Baada ya kupatikana silaha na askari wa kutosha, msako mkali ulipangwa kuanza siku ya pili alfajiri kwa kusaka pori lote na maeneo ya karibu. Kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa watu nao walijipanga kwa kuamini adui yao ni mzoefu wa kutumia silaha za moto.
Msako ulianza saa kumi na moja alfajiri wakiwa wamepishana robo saa na muda aliopanga Ng'wana Bupilipili kutoka kambini. Wao walikuwa nyuma kwa nusu saa Ng'wana Bupilipili aliondoka majira ya saa kumi na nusu.
Ng'wana Bupilipili aliondoka kambini majira ya saa kumi na nusu akiwa amembeba mwanaye mgongoni kwa kumfunga madhubuti na kitenge.
Kwa ujasiri mkubwa, aliingia ndani ya pori lenye kiza kinene. Akiwa amejitolea kwa lolote litakalotokea mbele yake, alianza safari yake kwa kupita kwenye mbuga iliyokuwa ikitisha huku milio ya wanyama na wadudu watembeao usiku ikitawala.
Hali ya hewa ilikuwa ya baridi kali lakini hiyo haikumsumbua. Alitembea huku akimuomba Mungu amfikishe salama na kumlinda na vitu vibaya japokuwa hakujua anakwenda wapi usiku mnene kama ule.
Baada ya mwendo wa robo saa wingu zito lilitanda na kuongeza kuimeza nuru ndogo ya nyota na kuongeza hofu kwa Ng'wana Bupilipili.
Alimuomba Mungu amuokoe na mvua ile kwa vile sehemu aliyokuwa akienda hakukuwa na sehemu ya kujikinga asilowane.
Dua yake haikufua dafu kwani baada ya dakika tano mvua nzito ilishuka.
Alijikuta akipata wazo la kurudi kambini, kwani sehemu aliyokuwa akielekea ilikuwa haionekani vizuri kutokana na kiza kizito.
Hakujua ajifiche wapi, alisimama akiwa amemkumbatia mwanaye aliyemtoa mgongoni na kumweka kifuani. Alijikuta yupo kwenye uamuzi mzito.
Mvua iliendelea kuwanyeshea ikiambatana na upepo mkali. Aliamini kabisa kurudi ni kujitia ndani ya kitanzi, akapiga moyo konde na kuamua kuendelea na safari.
Lakini kwa upande mwingine aliona kama ataendelea na safari itakuwa sawa na kuhatarisha maisha ya mwanaye kwa mvua na baridi kali ya usiku huo.
Hakuwa akijua mvua itakatika saa ngapi, hivyo lazima mwanaye angepata matatizo ya baridi ambayo yangemfanya awe katika wakati mgumu wa kumhudumia mtoto pia kujificha na maadui zake.
Alijikuta akipiga moyo konde na kuamua kuendelea na safari yake kwa kuamini haitanyesha muda wote uliobakia kufika asubuhi. Alitembea huku amemkumbatia mwanaye.
Alitembea bila kupumzika kwa zaidi ya saa moja huku mvua ikipungua na kumfanya aendelee na safari yake kwa kuingia ndani ya vidimbwi vya maji bila kujua kwa vile kiza kilikuwa kizito hasa kutokana na wingu zito lililokuwa limetanda.
Baada ya mwendo mfupi alijikuta akipita kwenye njia ambayo ilikuwa na shimo na kumfanya ateleze na kutumbukia kwenye shimo lililokuwa limejaa maji.
Alipiga kelele za woga na kujikuta akizama mpaka chini na mwanaye, alianza kuhangaika ndani ya maji kuokoa maisha yake na ya mwanaye.
Alibahatika kushika mzizi uliokuwa ndani ya maji, kwa nguvu zake zote aliufuata ule mzizi hadi kufanikiwa kutoa kichwa chake nje na cha mwanaye.
Aliung'ang'ania ule mzizi huku akichezesha miguu na kufanikiwa kukanyaga jiwe lililokuwa pembeni ndani ya maji mle shimoni.
Alijisogeza hadi juu ya jiwe na kusimama juu yake. Mikono yake ikiwa bado imeshikilia ule mzizi ambao ulikuwa kama nguzo yake mle ndani ya maji.
Baada ya kusimama ndani ya maji aliweza kujitoa mpaka sehemu za kifua, sehemu iliyobaki ilibakia ndani ya maji. Bado hakuona nje wala kujua urefu wa shimo lile. Alimuomba Mungu amuokoe mwanaye kama kifo basi kimkute yeye.

Je, nini kitafuatia? Usikose wiki ijayo.
 
Wakala wa Shetani -21-


Alijisogeza hadi juu ya jiwe na kusimama juu yake. Mikono yake ikiwa bado imeshikilia ule mzizi ambao ulikuwa kama nguzo yake mle ndani ya maji.
Baada ya kusimama ndani ya maji aliweza kujitoa kwenye mpaka sehemu za kifua, sehemu iliyobaki ilibakia ndani ya maji. Bado hakuona nje wala kujua urefu wa shimo lile. Alimuomba Mungu amuokoe mwanaye kama kifo basi kimkute yeye.
SASA ENDELEA...

Kikosi maalum kiliendelea na msako wa nguvu katika pori lile kwa kumtafuta Ng’wana Bupilipili kila kona bila mafanikio, kwa kupita pori kwa pori.
Watu wote walitawanyika na kuziba njia zote za kutokea kusubiri kupambazuke ili msako kamili uanze.
Wakati kunapambazuka Ng’wana Bupilipili alijikuta yupo ndani ya shimo ambalo pembeni yake kulikuwa na mti mkubwa ulioingiza mizizi yake ndani ya shimo.

Ilikuwa ajabu muda wote wa misukosuko mwanaye hakupiga kelele, alikuwa kimya na kutulia kwa mama yake.

Ilifika hatua ya Ng’wana Bupilipili kufikiri mwanaye huenda amefariki kutokana na ukimya wake. Alipomuita aliitikia kumuonesha mama yake yupo salama.

Baada ya kuhakikisha mwanaye yupo salama alishika mizizi ya ule mti na kupanda hadi juu. Alifanikiwa kutoka ndani ya shimo salama, kwa vile alikuwa amechoka na maji ya mvua alijilaza pembeni ya mti na mwanaye ambaye alimuachia ziwa anyonye.


Akiwa katikati ya usingizi alisikia sauti za watu wakibishana.

“Sidhani kama atakuwa amefika huku.”
“Bwana wee kwani nani alikuambia adui huwa ana mpaka wa sehemu ya kukimbilia?”
“Kwa hiyo tuendelee kumtafuta, nina uhakika tutampata.”
“Haya jamani safari iendelee mvua ya leo inatisha tumekesha nayo na kuamka nayo, nguo zote zimetota maji.”
“Hii ndiyo kazi ya jeshi.”
“Haya jamani nataka mpaka saa sita mchana tuwe na jibu tumempata au la.”
“Haya jamani tunaweza kuendelea tumepumzika vya kutosha.”

Ng’wana Bupilipili alijua amekwisha, lazima wangemuona hakuwa na sehemu ya kukimbilia. Sauti za askari zilizidi kumsogelea, hakuwa na ujanja zaidi ya kumchukua mwanaye bila kufikiria anafanya kitu gani na kujitupa naye ndani ya shimo la maji ili kujificha.


Kama mwanzo aliporomoka ndani ya maji na kwenda hadi chini ya maji kisha alirudi juu na kufanikiwa kuishika mizizi ya mti ambayo ilimsaidia kumpandisha juu.


Aliwasikia watu wale wakizungumza huku wakisogea kwenye lile shimo. Ng’wana Bupilipili alizama chini ya maji na mwanaye kwa muda ili watu wale wasimuone.


Baada ya muda alitokeza kwa juu kuvuta hewa. Aliwaona wakiwa wamempa mgongo, aliweza kuwaona askari waliokuwa wamebeba silaha kali za kisasa kama walikuwa wakimsaka Osama.


Moyoni alijiuliza kama watamkamata watamfanya nini. Pembeni ya shimo lile kulikuwa na majani ambayo angeweza kusimama chini yake na mtu wa juu asimuone.


Alijisogeza chini ya yale majani ambayo yalimficha. Aliendelea kumuomba Mungu wale watu waondoke haraka kwani maji ya mle shimoni yalikuwa ya baridi tena machafu.


Wasiwasi wake mkubwa uchafu na baridi lile ni hatari kwa afya ya mwanaye. Akiwa bado anamuomba Mungu alimsikia mtu mmoja akisema.

“Ngoja nikojoe shimoni.”
Haikupita muda mkojo ulitua kichwani kwa Ng’wana Bupilipili. Ilibidi atulie na kuuacha mkojo ule umwagikie kichwani. Baada ya jamaa kumaliza aliwasikia wakishauriana kuhusiana na msako uliokuwa ukiendelea bila mafanikio.
“Jamani kwa nini tuendelee kumtafuta porini kwa nini tusiende hata kwenye kile kituo cha kiroho labda atakuwa amekimbilia kule?“ mmoja alitoa wazo.
“Wazo zuri, wengine watakwenda kule na tuliobaki tutaendelea kumtafuta.”
“Kwa hiyo?”
“Muda huu tupumzikeni kidogo kama nusu saa kisha tutaendelea na msako, tuhakikishe mpaka jioni kila kitu kiwe kimeeleweka,” aliagiza mkuu wa msako ule.
“Hakuna tatizo.”

Baada ya muda Ng’wana Bupilipili alisikia kimya sehemu ile, hakuwa na haraka aliongeza dakika tano kuthibitisha kweli wameondoka.

Baada ya dakika tano kupita alishika mizizi na kujipandisha juu, alipofika juu alishukuru Mungu hakukuwa na mtu yoyote.

Taratibu kama komandoo wa kivita aliyekuwa akiwatoroka maadui, alifanikiwa kuwatoroka baada ya kuwaona kwa mbali.

Alielekea upande wa Mashariki kuwakimbia adui zake. Baada ya mwendo mfupi aliamua kupumzika kwani mwanaye alianza kutetemeka kwa baridi.
Alijitahidi kumkumbatia lakini haikusaidia kwa vile naye mwili wake kwa baridi la muda ule na ubaridi wa maji uliufanya mwili wake uanze kufa ganzi.

Itaendelea wiki ijayo.
 
[h=1]Wakala wa Shetani - 22-[/h]Taratibu kama komandoo wa kivita aliyekuwa akiwatoroka maadui, alifanikiwa kuwatoroka baada ya kuwaona kwa mbali.
Alielekea upande wa mashariki kuwakimbia adui zake. Baada ya mwendo mfupi aliamua kupumzika kwani mwanaye alianza kutetemeka kwa baridi.
Alijitahidi kumkumbatia lakini haikusaidia kwa vile naye mwili wake ulikuwa wa baridi la muda ule na ubaridi wa maji uliufanya mwili wake uanze kufa ganzi.
SASA ENDELEA...

Kila dakika hali ya mwanaye ilibadilika na kuonesha kupoteza uwezo wake wa kawaida. Hali ile ilimfanya Ng'wana Bupilipili kuchanganyikiwa na kuona jinsi alivyokuwa akimpoteza mwanaye huku akimuona.
Baada ya kuanza kuhema kwa shida, alijilaumu kwa kukaidi ombi la shoga yake Bupe la kumuacha mtoto kambini. Aliamini kama mwanaye atakufa yeye ndiye atakayebeba lawama kwa vile hali ile isingemtokea kama angemuacha mtoto kambini.
Moyoni alijuta na kuona kama mwanaye atakufa, basi kwake yeye hakuwa na sababu yoyote ya kupoteza maisha ya mume wake, kupoteza maisha ya wanakijiji na sababu ya yeye kuteseka vile.
Hali ya mwanaye ilizidi kuwa mbaya hata akawa haoneshi kupumua. Aliamini kabisa njia iliyokuwepo ya kumsaidia mtoto wake ni kujisalimisha kwa wale askari ambao wangeweza kuokoa maisha ya mwanaye kama wakifanikiwa.
Kwake hakuona hatari yoyote kama atafungwa au kunyongwa na mwanaye kubakia salama japokuwa hakujua mtoto wake ataishi maisha gani.
Alimchukua mtoto wake na kumuweka begani na kuwafuata wale askari waliokuwa wakimsaka huku akitokwa na machozi kwa uchungu wa mwanaye. Askari waliokuwa wamejipumzisha walishtuka kumuona mwanamke akiwa amembeba mtoto begani huku akionekana ametota kwa maji.
Wote walimtazama na kujiuliza anatoka wapi. Alipofika mbele yao alimbwaga mtoto wake mbele yao huku akisema:
"Haya mleni nyama sasa," alisema huku akifoka kwa sauti ya kilio.
"Mbona hatukuelewi, tumle nyama kivipi?" askari mmoja alimshangaa.
"Si mlikuwa mnataka kuona mwanangu anakufa? Haya amekufa furahini, haya nipelekeni mkaninyonge sasa."
Mkuu wa oparesheni hiyo alimchukua haraka yule mtoto na kugundua tatizo lake ni baridi yabisi, kwa haraka walitengeneza joto ambalo lilimsaidia mtoto kurudi katika hali ya kawaida kisha alichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo chao cha huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
Wakati huo Ng'wana Bupilipili alikuwa ame wekwa chini ya ulinzi baada ya kugundulika ndiye adui aliyekuwa akitafutwa. Hakutaka kuwabishia.
Walimshangaa mtu ambaye walikuwa na wasiwasi huenda ni mkakamavu tena mwenye mafunzo ya kijasusi, kumbe ni mwanamke. Mkuu wa oparesheni ile alishtuka na kuuliza mara mbili.
"Ndiye huyu?"
"Ndiyo mkuu," alijibu askari aliyekimbiwa na Ng'wana Bupilipili.
"Sasa mbona anaonekana tofauti na sifa nilizosikia, nilijua ni mkakamavu mwenye mwili wa mazoezi."
"Mkuu usimtazame kwa macho, ni zaidi ya gaidi, mwanamke huyu kama alivyoniahidi alipania kukimaliza kijiji kizima."
"Eti mama ni kweli?" Mkuu alimuuliza kwa upole.
"Maswali ya nini, si mmeshanikamata? Ninyongeni basi au niueni kwa risasi si mmekuja na bunduki kuniua?" Ng'wana Bupilipili alisema huku akilia kwa hasira.
"Hatuwezi kukunyonga kwa vile sisi si mahakama, la muhimu maelezo yako yanaweza kusababisha tukuache huru."
"Hayatasaidia kitu kwa vile maelezo ya awali nimueleza huyu kaka, lakini mliamua kunisaka kama gaidi. Mmefanikiwa kunikamata nipelekeni nikanyongwe ili mfurahi. Lakini naapa Mungu atalipa kwa kila roho isiyo na hatia," Ng'wana Bupilipili alizungumza kwa uchungu huku akimwaga machozi.
"Serikali haipo kwa ajili ya kumuonea mtu bali kuhakikisha kila mwanadamu anaishi kwa uhuru na amani bila kuvunja sheria," mkuu alionesha ustaarabu kwa kujibu kwa upole.
"Kwa vile wao wamekufa ndiyo serikali imeliona hilo, na sisi tuliopoteza roho za watoto wetu na waume zetu serikali yetu ni ipi?"
"Mmepotezaje hizo roho?"
Ng'wana Bupilipili alirudia maelezo ya mauaji ya albino Kijiji cha Nyasha na kifo cha mumewe, ikiwemo kuporwa mali zao na wanakijiji cha Nyasha.
Baada ya kumsikiliza mkuu alisema:
"Bado hukutakiwa kuchukua sheria mkononi kwa vile kuna vyombo vya sheria."
"Mmh! Vyombo vya sheria kwa vile wamekufa wao, mbona vifo vya watoto albino hamkuwahi kuja hata siku moja ila hivi ndiyo mmetengeneza mtego wa kuninasa, ndiyo maana nikasema nipelekeni mkani.ni..ni..ni.. Haaa!"
Ng'wana Bupilipili alishika chini ya titi la mkono wa kushoto baada ya kusikia mchomo mkali kwa ndani kama kumepasuka.
Maumivu yalikuwa makali na kuhisi kama mbavu zinagusana. Alipiga kelele za maumivu na kuanguka chini akiwa amepoteza fahamu.
***
Ng'wana Bupilipili baada ya kurudiwa na fahamu, alipofumbua macho alijiona yupo ndani ya hema amelazwa chini kwenye turubai lililokuwa limetandikwa na pembeni yake alikuwepo mwanaye Kusekwa ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi.
Alijikuta akijiuliza pale ni wapi na amefikaje, alimuangalia mwanaye ambaye alikuwa amelala huku akionekana yupo katika hali ya kawaida. Ili kuhakikisha mwanaye ni mzima aliweka sikio kifuani ambako alimsikia akihema vizuri.
Akiwa bado anamuangalia vizuri mwanaye, alishtushwa na sauti za watu waliokuwa wakisogea kwenye hema lile huku wakizungumza.
"Huenda amesharejewa na fahamu, ngoja tukamuangalie, yule mwanamke simuamini kabisa."
"Lakini mbona sifa za yule mwanamke hazilingani naye? Huenda kuna wahusika wakuu na yeye ni mtu wa kutumwa tu," askari mmoja alisikika akisema.
Ng'wana Bupilipili alipowasikia wamekaribia alirudi sehemu aliyokuwa amelala na kujilaza kana kwamba hajarudiwa na fahamu kwa kujitahidi kuhema kwa taratibu sana. Askari wale waliingia hadi ndani na kumkuta amelala, hata kuhema kwake hakukuwa kwa kawaida.
"Bado hajaamka twende zetu," alisema mmoja baada kuwa na uhakika mtuhumiwa bado amelala.
"Sasa tutaondoka saa ngapi?"
"Mkuu amesema tumsikilizie kwa muda zaidi ya hapo tutambeba na kuondoka naye."

Itaendelea wiki ijayo.
 
Wakala wa Shetani - 23-


ASKARi wale waliingia hadi ndani na kumkuta amelala, hata kuhema kwake hakukuwa kwa kawaida.
"Bado hajaamka twende zetu," alisema mmoja baada ya kuwa na uhakika mtuhumiwa bado amelala.
"Sasa tutaondoka saa ngapi?"
"Mkuu amesema tumsikilizie kwa muda zaidi ya hapo tutambeba na kuondoka naye."
SASA ENDELEA...


"Unajua bado siamini kama ni yeye ambaye katupa taabu ya miezi zaidi ya sita."
"John anasema yule mama kwa macho haoneshi hatari yake kwani alisema alifanya vile kulipa kisasi cha mume na mtoto wake aliyeuawa na wanakijiji kwa imani za kishirikina."
"Mmh! Basi ni kiboko, ni wanawake wachache wenye moyo wa ujasiri kama yeye."
"Ndiyo maana mkuu amesema ulinzi uwe mkali."
"Sasa unataka kuniambia huyu mwanamke na mtoto wake walikuwa wanaishi wapi na hii mvua?"
"Kutokana na maelezo ya John alisema anaishi porini kama mnyama."
"Utani huo, kwa muda gani?"
"Huu ni mwezi wa saba sasa."
"Mungu wangu, alikuwa anakula nini na kulala wapi?"
"Hapo ndipo unatakiwa ujiulize juu ya uwezo wa kikomandoo wa huyu mwanamke."
"Au amewahi kupitia jeshini?"
"Hilo kwa kweli sijui, ila mwanamke huyu kama ni kweli ni zaidi ya mwanajeshi wa kawaida."
"Ina maana yupo peke yake?"
"Kutokana na maelezo inaonekana aliondoka kijiji pale baada ya kuuawa mtoto na mumewe na kuamua kulipa kisasi kwa mkono wake."
"Lakini mkuu si amesema lazima aseme ukweli au ateswe sana, kwa mateso ya bosi hata awe komandoo lazima atasema."
"Ngoja tuone."
"Mmh, twende tupeleke taarifa."
Ng'wana Bupilipili aliwasikia wakiondoka, alitulia kwa muda kisha alinyanyuka taratibu alipolala na kunyata hadi kwenye mlango wa kutokea. Alichungulia kwa chati nje, aliwaona askari wawili waliokuwa wamekaa juu ya gogo la mti wakicheza karata wakiwa wamempa mgongo.
Aliangalia upande mwingine ambapo aliwaona wengine kwa mbali wakinywa pombe kali kukata baridi. Upande wa pili kulikuwa na mbuga ambayo ilikuwa ni vigumu mtu kutoka nje ya hema bila kuonekana.
Akawa na wazo la kutoroka kwa kuamini akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria lazima hukumu itamuumiza yeye. Aliamini anaweza kupita kwa mwendo wa kunyata nyuma ya wale askari. Lakini wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kama ataonekana basi atajiweka katika wakati mgumu sana.
Aliamini ukweli wowote hautaaminiwa zaidi ya kuteswa ili kulazimishwa aseme asichokijua. Aliamini njia nyepesi ni kutoroka na kupania kama atafanikiwa kutoroka asingesimama kwa siku mbili kutembea pori kwa pori mpaka atakapotoka nje.
Akiwa bado anatafakari jinsi ya kutoka ndani ya hema lile, macho yake yalitua kwenye uwazi uliokuwa upande wa chini ya hema. Wazo la haraka lilikuwa kupitia katika upenyo ule ambao hakukuwa na ulinzi wowote, wazo la kumbeba mtoto wake aliliweka pembeni kwani aliamini kutokana na kauli za wale watu mwanaye yupo salama.
Alimchukua mtoto wake na kumkumbatia kwa muda huku machozi yakimtoka, kwa sauti ya chini alimueleza mtoto wake:
"Kusekwa baba, nakupenda sana mtoto wangu, nina imani mpaka sasa upo katika mikono salama ila mama yako hatari nzito ipo mbele yangu. Nakuacha baba ili nami niokoe maisha yangu kwani bila hivyo kitanzi kipo shingoni kwangu.
"Kusekwa baba, mama yako sijui niendako, japo wewe ni mtoto usiyejua lolote lakini niombee mama yako nitoke salama, safari yangu iwe yenye muongozo mwema na Mungu aniongoze nifike kwenye mikono salama.
"Nakupenda mwanangu, nakupenda sana na Mungu akulinde kwa jambo lolote baya, Mungu akipenda tutaonana siku yoyote kama bado tunaishi na kama siyo duniani basi kwenye ufalme wake wa milele."
Baada ya maombi yaliyomtoa machozi huku moyo ukimuuma kutengana na mwanaye kipenzi kama angefanikiwa kuwatoroka, alimrudisha kwenye turubai na kusimama kwa muda akimuangalia mwanaye huku moyo ukizidi kumuuma.
Alishika mikono kifuani huku akilia, akageuka na kupiga magoti kupekenyua sehemu iliyokuwa na uwazi kwa chini na kutoka kwa kutambaa. Baada ya kufanikiwa kutoka bila kuonekana, aliingia porini kwa mwendo wa kuinama na kunyata.
Ilifikia hatua ya kutembelea tumbo kama komandoo aliyekuwa akivamia kambi, baada ya kufanikiwa kufika mbali kidogo ambako aliamini kabisa hawezi kuonekana, alitimua mbio kukata pori bila kujua hatari atakayokutana nayo mbele.
Alikimbia kwa mwendo wa mbio za marathoni bila kupumzika kwa kuamini uwezo wake wa kukimbia bila kupumzika ndiyo utakaookoa maisha yake. Alikimbia kwa saa tatu bila kupumzika na kujikuta ametokea kwenye barabara kubwa ya lami. Alisimama na kuanza kuhema kwa kasi, hali iliyomfanya ahisi kizunguzungu. Bila kupenda alianguka chini na kupoteza fahamu.
***
Baada ya muda kukatika, mkuu wa kikosi maalumu cha kumsaka muuaji wa Kijiji cha Nyasha alimtuma askari akamuangalie tena Ng'wana Bupilipili kama ameamka ili kama bado amelala wambebe na kuondoka naye. Askari alikwenda hadi kwenye hema kuangalia kama mtuhumiwa wao ameamka.
Alikwenda hadi ndani ya hema lakini katika hali ya kustaajabisha, ndani ya hema hakukuwa na mtu yeyote zaidi ya mtoto aliyekuwa bado amelala. Ilibidi awaulize wenzake waliokuwa wanaendelea kucheza karata.
"Oyaa washikaji yule mwanamke yupo wapi?"
"Si amelala humo ndani."
"Mbona simuoni?"
"Sele hebu acha utani, yupo humo ndani."
"Kweli washikaji yupo mtoto peke yake."
Wale askari waliokuwa wakicheza karata walinyanyuka na kwenda hadi ndani ambako hawakumkuta. Walijikuta wakichanganyikiwa na kuanza msako kuzungaka hema lakini hakukuwa na mtu yeyote eneo hilo.
Walijikuta wakipagawa na kujiuliza watamwambia nini mkuu wao aliyewapa jukumu la kumlinda yule mwanamke aliyeonekana dhaifu mbele ya macho ya watu lakini ni hatari kwa vitendo.

Itaendelea wiki ijayo.
 
Kwani ile Mama yangu adui yangu imepotelea wapi? au ndo utakuwa unaleta story zinafika mahali unaishiwa maneno basi unashindwa kumalizia???
 
Wakala wa Shetani - 24-

Wale askari waliokuwa wakicheza karata walinyanyuka na kwenda hadi ndani ambako walikuta patupu. Walijikuta wakichanganyikiwa na kuanza msako kuzunguka hema lakini hakukuwa na mtu yoyote eneo hilo.

Walijikuta wakipagawa na kujiuliza watamwambia nini mkuu wao aliyewapa jukumu la kumlinda mwanamke huyo aliyeonekana dhaifu mbele ya macho ya watu lakini ni hatari kwa vitendo.

SASA ENDELEA...

Waliotumwa walirudisha taarifa za kutoweka kwa Ng'wana Bupilipili na kumtelekeza mtoto. Sherehe yote ya kumpata mtuhumiwa iliyeyuka na kuamuliwa ufanywe msako wa haraka. Kila askari alitawanyika kwenda anapopajua ili mradi arudi na mtuhumiwa.
Askari wote walitawanyika huku waliofanya makosa ya kizembe wakichanganyikiwa zaidi kwa kukimbia ovyo bila kujua wanakwenda wapi.

Askari wengine walibakia pamoja na mkuu wao kwa ajili ya kulinda usalama wa mtoto.

Msako ulifanyika mpaka usiku wa manane lakini hawakupata chochote, mkuu wa oparesheni ile aliwaeleza waliofanya uzembe wahakikishe

mtuhumiwa anapatikana la sivyo wasirudi. Hawakupata muda wa kupumzika, walirudi kufanya msako.

Waliona hawawezi kukaa na yule mtoto aliyeanza kumlilia mama yake. Kwa vile kituo cha kulea watu wanaoishi katika mazingira magumu kilikuwa

karibu, siku ya pili walimchukua na kumpeleka katika kituo kile. Walipofika mkuu wa kikosi cha kumsaka muuaji alijitambulisha kwa Father Joe, baada ya kujitambulisha walimueleza sababu ya kuwepo pale.

Father alikubali kumpokea mtoto yule na kumlea, lakini alishangaa kumuona ni mtoto wanayemfahamu.

"Ha! Huyu mtoto si wa hapahapa kambini?"


"Hapana Father huyu tumemuokota porini na mama yake," alijibu mkuu wa oparesheni.


"Huyu wa hapahapa kambini na mama yake anakaa hapahapa, jina lake anaitwa Kusekwa."


"Hapana huyu mama yake ni muuaji tena amekimbia baada ya kumkamata na kumtelekeza huyu mtoto," mkuu wa oparesheni alizidi kubisha.


"Hapana, mama yake ni mkimbizi wa Kijiji cha Nyasa, si muuaji," Father Joe alimtetea Ng'wana Bupilipili.


"Father hebu tuitie huyo mwanamke tumuone na amtambue mtoto wake," mkuu wa oparesheni alimuomba Father Joe.


Father Joe alinyanyua simu na kumwita sister mmoja, baada ya muda mfupi Sister Mary aliingia.


"Sister Mary naomba uniitie Ng'wana Bupilipili."

"Sawa Father," sister aligeuka na kuondoka.
Baada ya muda alirudi akiwa peke yake.
"Vipi yupo wapi?"
"Hayupo father."
"Atakuwa amekwenda wapi?"

"Kwa kweli jirani zake hawana taarifa zozote mpaka jana usiku wanakwenda kulala walikuwa wote."

"Chumba chake kina vitu vyake?"

"Ngoja nikahakikishe," sister alisema huku akiondoka.


Sister alitoka tena na kwenda chumba cha Ng'wana Bupilipili ambako hakukuwa na mabadiliko yoyote. Alirudi na kutoa taarifa, baada ya kusikia vile mkuu wa oparesheni aliuliza.


"Kwani huyo mnayemsema mnayo picha yake?"

"Ndiyo."
"Basi tupeni tuiangalie kama siyo yeye tuondoke tukaendelee na msako wetu."
Father Joe alifunua faili lililokuwa na picha za watu wote waliokuwa kwenye kambi ile. Alichambua picha mojamoja kwa umakini mpaka akaipata picha ya Ng'wana Bupilipili.
"Picha yake hii hapa," Father Joe alisema huku akiwakabidhi.

Waliichukua ile picha na kuitazama kwa muda na kugundua kumbe mbaya wao hakuwa akikaa porini kama alivyojinadi bali alikuwa anakaa kwenye kambi ile.


"Father ndiye huyu!"

"Mna uhakika?" Father Joe aliuliza macho yakiwa yamemtoka pima.
"Kwa asilimia mia moja."
"Mmh! Mnataka kuniambia huyu mwanamke ni muuaji?" father alishtuka.
"Ndiyo father, ameua watu wengi Kijiji cha Nyasha na askari wenzetu wawili."

"Lakini si ndiyo kijiji alichokuwa akiishia zamani kabla ya kukimbia kuokoa maisha ya mwanaye huyu mlemavu wa ngozi na kujikuta akimpoteza mumewe aliyeuawa na wanakijiji na kufanikiwa kukimbilia hapa tulipowahifadhi siku zote za maisha yao?"

"Ni kweli father, maelezo yako na ya huyo mwanamke yapo sawa, aliahidi mbele yangu kuwa analipa kisasi na kama asiponyongwa baada ya

kumkamata, atahakikisha Kijiji cha Nyasha kinabakia historia, atakifagia chote," alisema askari aliyemkamata Ng'wana Bupilipili.

"Mmh, kumbe ndiyo hivyo, mbona mimi nilikuwa sijui!" father alishtuka huku Sister Mary naye akisikia habari ya kumshangaza.

"Basi father yule mwanamke ni zaidi ya gaidi, ameua watu wengi kwa sumu ya dawa ya kuulia wadudu katika maji."

"Dawa ya kuua wadudu ni dawa gani hiyo?"
"Kwa kauli yao nakubaliana nao, Ng'wana Bupilipili anahusika, chumbani kwake chini ya godoro nimeikuta hiyo dawa zaidi ya paketi tatu," Sister Mary aliwaunga mkono.

"Mmh, kama ni hivyo yule mwanamke ni mbaya sana, nilikaa naye na kumueleza awasamehe na kumuachia Mungu na kunikubalia. Kumbe alikuwa na siri yake nzito moyoni ambayo sote humu ndani tulikuwa hatujui," Father Joe alisema kwa masikitiko.

"Kwa kuonesha huyu mwanamke ni mzoefu hii ni mara ya pili tunamkamata na kutoroka juzi tulimkamata lakini alifanikiwa kututoroka."
"Mmh, sasa napata picha inawezekana siku hiyo ndiyo aliyokimbia na kuangukia mlango wa kuingilia getini na kudanganya alikimbizwa na mnyama mkali," Father alitoa ushuhuda.

"Kwa usemi huo ni kweli kabisa, mmh! Mwanamke yule basi ni mzoefu kama ameweza kukaa hapa na kufanya mauaji bila mtu yeyote hapa kambini kujua ni mzoefu wa hali ya juu," Sister Mary alisema kwa masikitiko makubwa.

"Sasa atakuwa wapi?" Father Joe aliwauliza wale askari.

"Kwa kweli mpaka sasa hatufahamu kakimbilia wapi, kwa sababu mazingira ya kututoroka ni ya hali ya juu. Inawezekana alishapitia mafunzo fulani ya jeshi, si rahisi mtu wa kawaida akawa na uwezo wa kufanya vile hata kuweza kutembea porini peke yake na kukimbia kwa umbali mrefu."

"Sasa mtafanya nini?"

"Tutaondoka na picha hii ambayo tutaiweka katika vyombo vya habari, lazima atakamatwa tu."

"Lakini nina imani kama ni tabia yake ya kurudi kambini basi lazima atarudi na sisi tutawajulisha mara moja," Father Joe alitoa wazo.
"Mtatusaidia sana."
Walikubaliana wamuache mtoto Kusekwa ambaye ni mlemavu wa ngozi na kuamua kuendelea kumsaka Ng'wana Bupilipili.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki ijayo.
 
MziziMkavu uko juu stori inaelewelka ile mbaya na ina fundisha sana ila naomba kukusahihisah kidogo tu Magu na si Mangu
 
Wakala wa Shetani - 25-


“Kwa usemi huo ni kweli kabisa, mmh! Mwanamke yule basi ni mzoefu, kama ameweza kukaa hapa na kufanya mauaji bila mtu yeyote hapa kambini kujua ni mzoefu wa hali ya juu,” Sister Mary alisema kwa maskitiko makubwa.

“Sasa atakuwa wapi?” Father Joe aliwauliza wale askari.

“Kwa kweli mpaka sasa hatufahamu amekimbilia wapi, kwa sababu mazingira ya kututoroka yana

utata wa hali ya juu. Inawezekana alishapitia mafunzo fulani ya jeshi, si rahisi mtu wa kawaida akawa na uwezo wa kufanya vile hata kuweza kutembea porini peke yake na kukimbia kwa umbali mrefu.”


“Sasa mtafanya nini?”

“Tutaondoka na picha hii ambayo tutaiweka katika vyombo vya habari, lazima atakamatwa tu.”
“Lakini nina imani kama ni tabia yake ya kurudi kambini basi lazima atarudi na sisi tutawajulisha mara moja,” Father Joe alitoa wazo.
“Mtakuwa mmetusaidia sana.”

Walikubaliana wamuache mtoto Kusekwa ambaye ni mlemavu wa ngozi na kuamua kuendelea kumsaka Ng’wana Bupilipili.

SASA ENDELEA...


Ng’wana Bupilipili aliposhtuka, alijikuta amelala kwenye kitanda kilichoashiria kuwa pale ni hospitali. Alijiuliza amefikaje mahali pale, akajikuta akichanganyikiwa. Alipotaka kuamka, mwili wake haukuwa na nguvu na kumfanya arudi kulala kitandani.

Akiwa bado amejilaza na maswali lukuki yakiendelea kupita kichwani kwake, ghafla mlango ulifunguliwa, Ng’wana Bupilipili alifumba macho kwa haraka na kutulia tuli kitandani kusikilizia aliyeingia ni nani.

“Itakuwa amepata nafuu,” ilikuwa ni sauti ya kiume.
“Ni kweli, ilionesha alitumia nguvu nyingi sana pia mwili umepungukiwa maji.”
“Atakuwa anatoka wapi?”
“Hilo swali tumsubiri aamke mwenyewe.”
“Kwa hiyo tumuache alale?”
“Hapana mshitue aamke ili apewe uji wa maziwa na baadaye chakula aweze kupata nguvu, zaidi ya hayo hana tatizo kubwa.”
Baada ya muda, Ng’wana Bupilipili alisikia akitingishwa taratibu huku akiitwa.
“Mama mdogo... mama mdogo.”
“Mmh,” Ng’wana Bupilipili aliitikia kama yupo usingizini.
“Dokta anaamka.”
“Muamshe kabisa kisha fanya nilivyokueleza, mimi nipo ofisini taarifa zingine utaniletea.”
“Sawa dokta.”
Yote Ng’wana Bupilipili aliyasikia na kuamini sehemu aliyokuwepo ni salama kwake. Alipoitwa mara ya pili aliitikia huku akifumbua macho, akakutana na muuguzi mbele yake.
“Pole,” muuguzi alisema kwa sauti ya upole.
“Asante.”
“Unajisikiaje?”
“Mwili hauna nguvu.”
“Basi amka upate uji kisha ule chakula utajisikia vizuri.”

Ngw’ana Bupilipili aliamka kitandani kwa msaada wa muuguzi na kukaa kitako, muuguzi alitembea naye akiwa amempa msaada wa kumshika mkono hadi chumba cha chakula. Alimketisha kwenye kiti na kumletea uji wa maziwa ambao aliunywa wote.

Baada ya kunywa uji, alijikuta akitokwa na jasho jingi, muuguzi aliyejitambulisha kuwa anaitwa Sabina alimuonesha bafuni ambako alienda kujimwagia maji na kupata nguvu. Alirudi naye chumba cha chakula na kumpatia chakula ambacho nacho alikila chote kuonesha alikuwa na njaa kali.

Baada ya kula alirudishwa wodini ili apumzike kabla ya kuonana na mganga mkuu. Baada ya nusu saa, alifuatwa na muuguzi kupelekwa kwa mganga mkuu. Ng’wana Bupilipili aliongozana na yule muuguzi akijua lazima kuna maswali ya kuulizwa juu ya kuwepo pale na mahali alikotokea.

Aliingizwa katika ofisi ambayo haikutofautiana na ya Father Joe, pia mganga mkuu alikuwa Mzungu. Alipowaona wanaingia, aliacha kazi zake na kuwakaribisha.
“Ooh, karibuni.”
“Asante,” alijibu Ng’wana Bupilipili.
“Pole na matatizo.”
“Asante.”
“Unaitwa nani?”
“Malimi,” Ng’wana Bupilipili alidanganya.
“Unatokea wapi?”
“Kijiji cha Sanza.”
“Kijiji cha Sanza mpaka huku umefikaje?”
“Kulitokea vita ya familia ambayo ilifanya wanakijiji tutawanyike na kukimbia kusikojulikana kuokoa maisha yetu.”
“Umetumia muda gani kufika barabara kuu?”
“Siku tatu.”
“Mmh, pole sana.”
“Asante.”
“Una mpango gani?”
“Kwa kweli mpaka sasa sijajua niende wapi hata hapa nimefika sijui ni wapi?”
“Hapa ni Sangema, je, upo tayari kurudi kijijini kwako?”
“Bora nife lakini sipo tayari kurudi huko.”
“Una familia?”
“Yote imeteketea vitani.”
“Pole sana.”
“Asante.”
“Basi mama, sijui unaitwa nani?”
“Baba si nimekueleza naitwa Malimi.”
“Ooh samahani, sasa mama Malimi utaishi hapa kwa vile kituo hiki kinatunza watu wenye shida.”
“Nashukuru baba yangu, asanteni kwa moyo wenu wa kujitolea Mungu awazidishie.”
“Amen.”
“Sabina kamuoneshe chumba apumzike mambo mengine atapangiwa kesho.”
Sabina alimchukua Ng’wana Bupilipili na kwenda kumuonesha chumba cha kupumzika.


MIAKA SABA BAADAYE
Kusekwa aliendelea kukua vizuri akiwa katika kambi aliyoachwa huku akiendelea na masomo ya awali ya chekechea wakati akiandaliwa kwenda shule ya msingi. Kabla hajaanza shule ya msingi, alitokea Mzungu mmoja aliyekuwa akimiliki machimbo ya dhahabu.

Mzungu huyo aliyejulikana kwa jina la John Brown ‘Mr Brown’ alikuwa na mgodi mkubwa uliokuwa na wachimbaji wengi sana. Kutokana na uwezo wake wa kifedha aliweza kuwasaidia wanakijiji waliokuwa jirani na machimbo yale. Alijenga zahanati na

miradi ya maji na umeme ambayo ilikuwa msaada tosha kwa wanakijiji ambao walifaidika na machimbo yake.
Mr Brown ndani ya eneo lake la machimbo alijenga shule kwa ajili ya watoto kuanzia miaka miwili na kuendelea. Sifa zake zilizagaa kila kona ya nchi na kuifanya serikali impunguzie kodi pamoja na kumpa misamaha katika vitu alivyokuwa akiingiza nchini.

Itaendelea wiki ijayo.

 
Wakala wa Shetani - 26-


MIAKA SABA BAADAYE
Kusekwa aliendelea kukua, akafikia hatua ya kwenda shule iliyokuwa katika kambi hiyo, akaanza chekechea na kuandaliwa kwenda shule ya msingi. Lakini kabla hajaanza

shule ya msingi alitokea Mzungu mmoja aliyekuwa akimiliki machimbo ya dhahabu.

Mzungu huyo aliyejulikana kwa jina la John Brown ‘Mr Brown’ alikuwa na mgodi

mkubwa uliokuwa na wachimbaji wengi sana. Kutokana na uwezo wake wa kifedha aliweza kuwasaidia wanakijiji waliokuwa jirani na machimbo hayo. Alijenga zahanati na

miradi ya maji na umeme ambayo ilikuwa msaada tosha kwa wanakijiji ambao walifaidika na machimbo yake.


Ndani ya eneo lake la machimbo, Mr Brown alijenga shule kwa ajili ya watoto kuanzia miaka miwili na kuendelea. Sifa zake zilizagaa kila kona ya nchi na kuifanya serikali

impunguzie kodi pamoja na kumpa misamaha katika vitu alivyokuwa akiingiza nchini.

Kingine ambacho kiliungwa mkono na wengi ilikuwa ni kuwachukua walemavu wa ngozi (albino) ambao walianza kusoma pale na baadaye kuwapeleka nje ya nchi kwa masomo zaidi.
SASA ENDELEA...

Kusekwa naye alichukuliwa na Mr Brown na kuanza masomo yake ya darasa la kwanza.
Baada ya miezi miwili, Kusekwa alipata nafasi ya kusafiri kwenda Ulaya kimasomo. Aliandaliwa sherehe kama wenzake waliotangulia na safari yake ilikuwa siku ya pili alfajiri.

Kama kawaida, Kusekwa alikwenda kulala kusubiri asubuhi asafiri. Siku hiyo alilala sehemu tofauti na anapolala siku zote. Majira ya saa nane za usiku, alishtushwa na watu walioingia chumbani kwake wakiwa wameziba nyuso zao, kabla hajajua nini kinaendelea alivamiwa na kuzibwa mdomo kisha alibebwa juujuu na kupelekwa asikokujua.


Kusekwa alibakia na mawazo wale ni akina nani na mbona wamembeba vile au ndiyo mtindo wa wote wanaosafiri kwenda Ulaya? Alijifikiria kama wangekuwa ni majambazi au watu wabaya wamepitia wapi mpaka kuingia kule chumbani kwenye kambi yenye ulinzi mkali?


Alijikuta akiwa njia panda huku wale watu wakimpeleka kimyakimya bila kuongea chochote. Baada ya muda, aliingizwa kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa na kiti na kukalishwa pale. Baada ya kukalishwa, mtu mmoja aliwasha swichi, mikono na miguu ya Kusekwa ilishikiliwa na vyuma.


Kusekwa alizidi kushangaa watu wale kumfanya vile walikuwa na shida gani tena walionesha siyo wema kwake. Baada ya kubanwa na vyuma, mashine iliwashwa ili kumkata viungo. Lakini ilikuwa ajabu mashine iligoma kuwaka, kitu kilichowachanganya wale watu na kujaribu mara ya pili lakini iligoma.


“Sasa itakuwaje?” Mmoja aliuliza jasho likimtoka baada ya mtambo kugoma.

“Tatizo hili lilitokea hata mwezi uliopita tulipotaka kumkata viungo yule albino lakini baadaye ilikubali na kufanya kazi yake.”

Kauli ile ilimshtua sana Kusekwa na kuona kumbe safari ya Ulaya ni kifo, alianza kulia kwa sauti kuomba msaada lakini aliambulia makofi yaliyomfanya anyamaze kusubiri hatima yake. Alimuomba Mungu kwa kila lugha aliyoifahamu. Aliiomba mizimu ya baba na mama yote imtangulie kumponya katika kinywa kile cha mauti.


Walikubaliana kumfungua ili kurekebisha ule mtambo ambao uligoma kukata viungo vya albino. Walimfungua Kusekwa ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa woga wa kupoteza maisha. Walimlaza chini na kuanza kuufanyia matengenezo mtambo ili uweze kufanya kazi yake vizuri.


Walijitahidi kufanya kazi kwa haraka ili waifanye kazi kwa wakati na kurudisha salamu kwa Mr Brown. Wakiwa katika hali ya kutengeneza mtambo, walimuacha Kusekwa amelala chini kwenye sakafu akiwa kifua wazi. Kutokana na ubaridi wa kwenye sakafu uliosababishwa na kiyoyozi, Kusekwa alizinduka.


Alipofumbua macho taratibu, aliwaona wabaya wake wakihangaika kutengeneza mtambo wa kukatia viungo vya albino. Alitembeza macho taratibu na kuangalia mandhari ya mle ndani na kugundua kuna mitambo mingine miwili na milango minne, kati ya hiyo mitatu ilikuwa wazi.


Ndani ya kile chumba kilichokuwa na mtambo mmoja wa kukatia viungo na mitambo mingine ambayo hakuifahamu, pia kulikuwa na majokufu yaliyoonekana yana kazi ya kuhifadhi viungo vya albino.


Watu wale walikuwa wamemsahau na akili zao zote zilikuwa katika mashine. Akiwa bado amejilaza chini bila kujitikisa kwa kuogopa kumuona na kuhamishia mawazo yao kwake, Kusekwa alipata wazo la kutoroka kwa kunyata huku akimuomba Mungu aweze kutoka salama.


Kabla hajachukua uamuzi huo ambao kwake ilikuwa ni kama kucheza mchezo wa pata potea. Umeme ulikata ghafla na wote waliokuwa katika kile chumba walishtuka, alimsikia mmoja akisema.


“Huu mkosi gani? Mashine ilibakia kidogo kieleweke, kukatika kwa umeme kumeturudisha nyuma kabisa.”


“Unajua kazi hii tunaidharau lakini inaweza kututoa jasho,” mwingine aliongeza.

“Wasiwasi wenu tu, umeme unawaka na kazi inaendelea, tatizo tumeshalijua hatutachukua muda mrefu kulitatua,” wa tatu naye alisema.

Kusekwa aliwashangaa wale watu ambao hawakuwa na chembe ya huruma kwa kutengeneza mtambo ule haraka ili wamgawanye viungo vyake bila huruma. Akiwa bado amejilaza chini, aliwashangaa watu wale pamoja na umeme kukatika hawakumgusia yeye zaidi ya mtambo uwahi kupona na kumtenganisha viungo vyake.


Aliamini muda ule wakati wauaji wasio na huruma wakisubiri umeme uwake naye angejaribu bahati yake ya kutoroka. Alinyanyuka taratibu pale chini alipolazwa na kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata. Aliutafuta mlango, akafanikiwa kuupata na kutoka kwa kunyata bila kujua anaelekea wapi.


Aliendelea kutembea kuelekea nje katika giza nene huku akimuomba Mungu amuepushe na kikombe kile. Baada ya kutembea kwa muda huku akipapasa na kuomba Mungu umeme usiwake upesi, alijikuta akijigonga kwenye kitu, alipopapasa aligundua ni gari.


Alipopapasa vizuri aligundua ile ni Toyota Pick Up, akiwa anajiuliza pale ni wapi, mara umeme uliwaka. Kusekwa alijiona yupo kwenye maegesho ya magari ambayo yalikuwa na magari mengi, kabla hajaamua afanye nini aliwasikia watu wakielekea kwenye ile gari wakizungumza.


“Inabidi tuwahi kuondoka muda huu mzigo umefika tangu saa saba.”

“Itakuwa vizuri, Mr Brown alikuwa hana raha kabisa.”

Sauti zile zilimfanya Kusekwa aingie chini ya gari ile na kujificha, akiendelea kumuomba Mungu. Kuwaka kwa umeme kulifanya eneo lote ling’ae kama mchana na kumfanya aamini lazima atakamatwa kutokana na kuwaona askari wakipishana kuhakikisha ulinzi wa mule mgodini.


Itaendelea wiki ijayo.
 
Back
Top Bottom