Wakala wa majengo nchini (TBA) yatoa ufafanuzi baada ya kupatikana nyufa katika Hosteli za chuo kukuu cha Dar(UDSM)

HUYU JAMAA ANADHAN NCH YETU NI YA MWAKA 50? INA WAJINGA WENG MPAKA ALETE FIX HV?

PSPF TWIN TOWER PALE MTAA WA SOKOINE NDYO JENGO REFU KULIKO YOTE TANZANIA, LINA GHOROFA 35 NA UREFU WA MITA 151 LAKINI HALINA NYUFA.

JENGO LA TPA

BENJAMIN MKAPA

GOLDEN JUBILEE

BOT

PPF TOWER ETC.

AU HYO PROCESS INAPITIA KWENYE HOSTEL TU? AACHE KULETA USANII KWENYE MAISHA YA WATU
 
Mbona ni nadra sana nyumba/majengo yaliyojengwa na mzungu kupata nyufa tofauti na yanayojengwa na Waafrika na nacho madogo?
 
Hakuna kitu kama hicho jengo lilokizi viwango halipaswi kuwa na ufa kwa muda mfupi tangu mradi kukamilika. Kuna makosa ya kiuandisi katika tendo zima la ujenzi wa majengo hayo. Mbona ubungo plaza halikupata nyufa kama hilo jengo?
 
Hahahaha nyie wanafunzi mnaoish humo endeleeni na life lenu, mtaalamu kasema ni 'kawaida'. Mkidondokewa watakuja na majibu tofauti. Awamu hii ni siasa tu
 
Hivi, nyumba inanyufa halafu watu watake ufafanuzi UPI zaidi ya nyufa kuzungumza hali halisi ya hostel!!

Majibu yenye akili na smart alitakiwa kusema hivi :-
Yaani "ni kweli kabisa, hostel zina nyufa ila ni matatizo madogo ya kiufundi tupo tunayashughulikia kitaalamu ili kuweka hali hii katika mazingira mazuri".

Hapo kila mtu angeelewa.
Na kutoka katika ujumbe kama huo sasa ambaye angesambaza picha basi , angekuwa na makosa kama yapo hayo makosa anayoyasema japo binafsi naona hakuna makosa ya kusambaza picha zenye nyufa naye kakili kabisa kuwa kuna nyufa.

Ila hii statement, kuwa nyumba "zinafanya settling" haaa haaa haaa ngoja nicheke kama vile ni jambo zuri.

Kwa kweli watu watasambaza picha na hata ufafanuzi wa kutoka kwako hauhitajiki maana nyufa zinafafanua kila kitu.

Kwa statement yake hiyo mwambieni aache ngojera na comedy.
 
Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.



SIJAELEWA HAPA:
Anaposema kwamba "Ni Jambo la Kawaida kwenye HATUA ZA UJENZI...". Kwann anasema kwenye hatua za ujenzi wakati jengo limeshaisha, limeshakabidhiwa, na watu wameshaanza kukaa..?? Ina maana bado tu lipo kwenye hatua..??

Aliyeelewa anisaidie tafadhali. Hahahahaha
Hata mie nimeshangaa hiyo kauli ya
"hatua za ujenzi"

Mie naona ametumia hiyo kauli ili kuwaandaa mtakapo waona wanarudi kwenye hayo majengo kuyafanyia marekebisho(kama inawezekana) basi msipige makelele kwasababu ni hatua za ujenzi
 
Labda majengo yao hayana "Extension joints" ...............!!

Huyo jamaa ajiandae tu kwa aibu aliyompa Mzee!!!
jamani kama kuna mzazi au mlezi mwenye mtoto humu amtoe haraka, tuzipishe siasa ziendelee kwanza
 
Kipara kipya hawezi kanyaga kabisa kwenye hii page... barafu nakuonaga ni mtu pekee wa chama unayeadmit mapungufu kama ni ya .kweli
Tangu jana sijawaona akina jingalao, Barbosa, Maswa 1.... Kwenye hizi habari.

Najua frustration imewapanda zaidi
 
March 25, 2017
TBA YAWABEBA VIJANA KATIKA AJIRA
Alichokisema Mtendaji Mkuu wa TBA Elius Mwakalinga baada ya kutembelewa na kamati ya bunge ya miundombinu na kuhojiwa utendaji wa wakala huyu mkuu wa ujenzi wa serikali ya Tanzania...

Source: MCL Digital
 
Hahah haya ndio majibu ya wataalamu wetu

Ngoja yaporomoke uje na ngonjera zako kwamba ni kawaida majengo marefu kuwa na nyufa

Hivi Benjamin Mkapa towers sio refu ? Lina nyufa lile ghorofa ?
 
Kama hizo nyufa huyo engineer anasema ni expansion joint, basi ERB haraka sana imfutie registration, ni aibu kwa msomi kama yeye kusema uongo wa kiasi hicho, hakuna expansion joint za aina hiyo duniani. Hizo nyufa zinaweza kutokana na sababu mbalimbali mfano
  • Poor desing, yani foundation haiendani na mzigo wote wa jengo.
  • Poor mix design ratio, hapa kama ilitakiwa kutumika concrete class 30 - 45 wao walitumia below 20.
  • Poor Curing, kama zege halikupata curing ya kutosha baada ya kulimwaga
  • No allowance for expansion joint, kama hakukuwa na expansion joint kwenye jengo huwa ni sababu kubwa ya jengo kupata cracks.
Amejibu kisiasa sana badala ya kuagiza uchunguzi wa kina, siku hizi kuna vifaa vya kisasa vinavyoweza kupima capacity ya jengo, kuanzia nondo zilivyopangwa , thickness zake, class ya concrete n.k. Ila muda ni mwalimu mzuri kuna siku atayajutia haya majibu yake ya leo.
 
Back
Top Bottom