Wakala wa majengo nchini (TBA) yatoa ufafanuzi baada ya kupatikana nyufa katika Hosteli za chuo kukuu cha Dar(UDSM)

Wananchi msiwe na wasiwasi,mnachokiona jengo lina undergo expansion ili liwezo kusettle vizuri,

Yaani, huyu sijui mhandisi anastahili viboko. Siyo kwa matamshi ya hivyo.

Pale UDSM majengo ya miaka ya 1960s , 70s to 80s hayana hata kijistari cha ufa.

Ila, leo hii jengo la nusu mwaka linafanya settling and expansion!?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Usipoziba ufa? Tatizo chabo noma sana! Unagegeda jamaa room ya pili anakuzoom,
 
Sitashaangaa nikisikia ni marufuku kusambaza picha za pombe hostel atakayefanya hivi kukiona!
 
Ulitegemea jibu la maana toka kwake? Kabla ya kujibu lazma apate maelekezo ya cha kuwaeleza nyie msio na uzalendo mnaosambaza picha mpaka ulaya. Kwanza picha zinatisha wakati vicrack vyenyewe vidooogo.
haaaa!! Vicrak vidogo???? Crack ni crack tu!!!! Hujasikia msemo wa usipojenga ufa utajenga ukuta??? Crack ni hatari kwenye nnyumba siyo ya kubeza. Na hao waliosambaza picha kosa lao nini??? Wametuhabarisha tuliokuwa hatujui. Unataka uzalendo kwenye maisha ya watu??? Hilo lisipotatuliwa haraka maisha ya vijana yatakuwa hatarini. Tomeona gorofa nyingi sana na anachosema huyo TBA hatujakiona. Hizo si gorofa za kwanza kujengwa TZ!!!
 
TBA yakiri kubomoka kwa mabweni
Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.

DQLqCivX4AEqx7P.jpg

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.

"Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga.

Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.

EATV

Hosteli za Magufuli chuoni UDSM zimeanza kubomoka. Nini chanzo? Watoto wetu watapona?
wavunje haraka iwezekanavyo.au wataziacha kwa sababu ni za magufuli
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kama ufa mkubwa hivi kwa macho tuu unaogopesha!, halafu mkurugenzi wa TBA anasema ni kitu cha kawaida, amini msiamini, serikali makini, haiwezi kusubiri hadi maafa ndipo huyu jamaa apumzishwe, hii ni picha moja tuu nyufa 3, na hata mwaka bado!, hii sio dalili nzuri hata kidogo, there is no excuse, majengo haya yamelipuliwa!, tukubali makosa, tujirekebishe, tusonge mbele, and from now, BOQ za tenda zote kubwa za TBA, zifanyiwe independent verification.

P.
Na nani? Hii ndio hasara kubwa kumkabidhi mtu mmoja mioyo na matarajio yote!!

Kama serikali imejiondoa kwenye mpango wa uwazi na inayojinasibu si ya mafisadi na mpenzi wa Mungu unategemea nini?

Muda ni mwalimu mzuri kwa tamaa za huyu bwana na mambo yake ya gizani utawala huu utazalisha ufisadi mzito kuliko tawala zote....

Kwa BoQ ile niliyofanikiwa kuiona kwa insiders wa NAOT na gharama tuliyotangaziwa ni wazi ufisadi sio mtu ni mfumo.

Yetu macho na masikio.
 
Hapa, tusubirie hizo expansion and settling ziendelee ili mwisho wa siku, after a proper expansion and settling then, a building will sink.

Kisha, ,TBA na huyo jamaa, watatuletea ngojera mpya, kuwa baada ya proper expansion and settling ,,,
,, ,, hostel sasa zinaweka msingi kwa upya maana, kifusi kitakachozama kitaleta msingi imara,,,.

Hadi hapa, nashindwa kuelewa hatua atakayochukuliwa huyo mhandisi na timu yake.
 
Yaani crack inahitaji ufafanuzi kweli?
Halafu bila aibu unasema crack ni kitu cha kawaida?
Ndio maana hata kununua watu na kupiga watu risasi imekuwa kawaida.
...hata ku-recruit watu wanao uzika na kugeuzwa mabango ya target ni kawaida yenu.
 
TBA yakiri kubomoka kwa mabweni
Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.

DQLqCivX4AEqx7P.jpg

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.

"Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga.

Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.

EATV

Hosteli za Magufuli chuoni UDSM zimeanza kubomoka. Nini chanzo? Watoto wetu watapona?
INJINIA SHIKAMOO....UKUTA UMEPASUKA TUNAAMBIWA NI EXPANSION JOINT......MIE HGL WACHA NIPITE TU.
 
Jamaa kajibu kisiasa sana, sijui wasomi wetu wanakula harange la wapi, eti ufa ni kitu cha kawaida..

Hapo pakipita tetemeko kidogo hapo maelfu ya wanafunzi watakufa kama kuku,, kinga ni bora kuliko tiba huyu jamaa ache ujinga wake,

Ingekuwa china au N.Korea sasa hivi huyo boss wa TBA amesha chezea kamba,
 
Ukiona maelezo hayana hata mfano mmoja ujue huo ni uongoo. Jengo lipi lingine lilipitia hatua kama hiyo?
 
Back
Top Bottom