Wakala wa majengo nchini (TBA) yatoa ufafanuzi baada ya kupatikana nyufa katika Hosteli za chuo kukuu cha Dar(UDSM)

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Baada yakuripotiwa kuwa na Nyufa kadhaa katika Jengo jipya la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilizobuniwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), Desemba 3, 2017, TBA wamefanya ukaguzi katika Jengo hilo nakubaini kuwa nyufa hizo zimetokea kwenye 'Expansion Joint' iliyopo Block A.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga amesema kuwa kwa kawaida katika taaluma ya ubunifu wa majengo, Majengo mapana huwekewa nafasi (Expansion Joint) ambayo huyatenganisha na kuwa sehemu mbili au zaidi ili kuruhusu Jengo kupumua inapotokea kutitia kwa udongo, au kutanuka na kusinyaa kwa udongo kutokana na hali ya hewa.

Mhandisi Mwakalinga amesema 'Expansion Joint' ni sehemu ambayo iantarajiwa Nyufa kutokea, katika ubunifu wa Majengo hayo, amesema kuwa TBA ilizingatia hitaji hilo ambapo kila jengo (Block) lina jumla ya Expansion Joint tatu (3).

Amesisitiza kuwa Nyufa zilizotokea katika Block A ziko kwenye Expansion Joint, kwa hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa ubunifu au ujenzi bali umetokea katika maeneo yaliyokusudiwa (Expansion Joint).

"Katika ukaguzi wa awali uliofanywa na wataalaamu wa TBA, ilionekana upande mmoja wa ile Expansion Joint, uko vizuri kwani ule uwazi umeonekana kufunikwa na kipande cha ubao bilo kujazwa udongo wa Saruji", amesema Mwakalinga.

"Upande wa pili wa ule uwazi ulijazwa kimakosa na udongo wa Saruji na kuondoa urahisi wa sehemu mbili za jengo kupumua. Upande wa pili wa uwazi uliojazwa udongo ndiyo unaonyesha dasari ya Nyufa zilizojotokeza, kutokana na ripu kwenye ukuta mzima wa sehemu ile kuungana na ule udongo ulioingia kwenye 'Expansion Joint'.

TBA imewatoa hofu watumiaji wote wa majengo hayo kwa kuwaambia kuwa ni salama kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kutokea kwa Nyufa za kawaida katika ujenzi wa Majengo na zimetokea sehemu iliyokusudiwa ambayo itafanyiwa marekebisho stahili.
tba.jpg
tba2.jpg

DQLqCivX4AEqx7P.jpg



Habari zaidi soma=> Hosteli za Magufuli chuoni UDSM zimeanza kubomoka. Nini chanzo? Watoto wetu watapona?
 
Back
Top Bottom