Wakaka wamekuaje tena?

Wakaka wamekuaje tena?

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Daaaaaa...
Hapa duniani kuna mengi sana.

Kwa heshima naomba nitangulize salamu kwa jukwaa hili pendwa. Kwa kweli mkasa ambao umenipata, nitapenda kuuongelea ili iwe funzo kwa wadada wengine wadogo ambao wanapata changamoto hizi ndogondogo.

Hivi karibuni baada ya kuachwa na mwenzangu ambaye tulidumu muda sana katika mapenzi, tukipita changamoto mbalimbali hususan za kiuchumi, nafikiri mwenzangu alipata mtu mwingine. Nami kwa kuwa nilishachoka kuwa mpiganaji wa kulinda penzi letu, nikaona sawa tu, aende nipate pumziko kwingine, pengine hatukuandikiwa...

Baada ya kama miezi 3, tukaanza mahusiano na kijana mwingine mtu mzima kidogo. Kwa kweli, alinijali sana na kunipenda sana. Lakini katika maongezi ni kama tulikuwa watu wawili tofauti. Wakati mimi nikimwambia mategemeo yangu katika mahusiano yetu ni kutulia na kutokuwa na dramas, mwenzangu alikuwa anaongea kana kwamba tuna urafiki wa sex tu na and nothing. Sikuwa na pupa kujua nini alimaanisha.

Kwa bahati mbaya mwenzangu alipata changamoto fulani mambo ya msiba, hivyo akalazimika kubeba majukumu katika familia yao kipindi hiko cha Covid 19. Alinishirikisha nami bila hiyana nikaona nimsaidie jambo ambalo lilimshangaza sana kwani hakutegemea kama ningeweza kujitoa kiasi kile tena katika kipindi cha Covid 19.

Baada ya hapo, upendo uliongezeka ikawa too much sasa kwa uapande wake jambo ambalo mimi nikaanza kupata wasiwasi. Wasiwasi wangu ukazidi pale ambapo jamaa akaanza tabia za kuonyesha dalili zote za kutaka niwe nampatia pesa. Ingawa anafanya masihara lakini ni yale masihara ya kweli. Mara nina ndoto za kufanya hivi nitafutie pesa, mara nataka kile in the future kitatusaidia but kitakaa kwangu and so many dramas.

Kwa kweli maisha ya namna hiyo, nikaanza kupoteza interest naye. Sababu ninaamini kusaidiana kupo na ni jambo la kawaida katika maisha either ya mapenzi ama la, lakini mtu anapomchukulia mwenzake aliyemsaidia kama kitega uchumi, kwa kweli, kwanza inasikitisha lakini pili itakufanya upoteze trust kwa mtu. Hii ni kwa ke na me.

Mpaka sasa nina mwezi sina interest kabisa ya kumtafuta mwenzangu. Sina interest naye kabisa naona hata yeye amegundua hivyo na ndio maana hanitafuti.

Mwenye kuona funzo na aone.
 
Inategemeana unajiwekaje,,mwanamke haitakiwi kuonesha demand ya ndoa au mahusiano kuliko mwanaume,ulipoonyesha kudemand jamaa akaku keep low,inatakiwa mwanaume ndo a demand penzi lako,kwa ushauri njoo pm

California love
 
Ni kuwa mwanamke amelelewa "kupokea" sio kutoa! Sasa unapoona unatoa tu bila kupokea unakwazika.. Relax Meridah, tusaidiane ni maisha tu
 
...tatizo wanaume walio serious kuwaoa mnawaona hawafai na hao wasio kuwa serious ndo manawauna wanafaa...

We unaona kabsa mwanaume masaa 24 anatupia picha zaidi ya kumi status tena uku akirembua na kukaa pozi tofautitfauti uku akinesha thamana ya vtu alivyovyaa....afu unasema apa kuna mume..!

Wadada ukiona mwanaume anajipist post hovyohvyo kweny hii mitandao kuwa makini huyo sio mume bado akili haijafikia phase ya uanaume.
 
Aisee noma sana sema Mwanamke akitoa pesa yake kwa Jambo linalomuhusu mwanaume huwa inamuuma sana hata kama ni ndani ya Ndoa ndo maana kuna familia mama hawezi toa hata hela ya kununua chumvi..!! Nadhani ni nature na huwezi pingana nayo.. So ulipomsaidia kipindi kile akajua kumbe pesaa unayo bhasi acha akupe plan mfanye kitu japo hio ni balaa wachache sana huwa na mwisho mzurii...hapo mwisho wa siku ni vilioo na kusaga menoo
 
Miezi mitatu baada kutoka kwenye uhusiano ushaingia kwenye uhusiano mpya?

Haraka ya nini?

Inaonesha wewe ni mdada mwenye malengo kwenye maisha yako na uko tayari kutulia na mtu mmoja mwenye lengo kama lako. Nakushauri chukua mda kama unataka kumpata mtu wa uhakika. Haraka haraka haina baraka.

Tumia mda wako kumjua mtu hili uweze kujua nia, malengo, na hali yake katika kuangaika kimaisha imekaaje.

Stop representing yourself like you're so desperate for a longterm relationship/marriage. Let things work out natural or they will use you like a piece of toilet paper.
 
Tatizo lako nyodo, kwenye ile ID nyingine nakutafuta unazingua, sahv umekuja na nyingine
 
C uliondoka kwangu kwa nyodo karma hio

Joke
 
Duuuuuuh ina maan mtu mzima kawa marioooh? Au mie ndo sijaelewa lol
 
Daaaaaa...
Hapa duniani kuna mengi sana.

Kwa heshima naomba nitangulize salamu kwa jukwaa hili pendwa. Kwa kweli mkasa ambao umenipata, nitapenda kuuongelea ili iwe funzo kwa wadada wengine wadogo ambao wanapata changamoto hizi ndogondogo.

Hivi karibuni baada ya kuachwa na mwenzangu ambaye tulidumu muda sana katika mapenzi, tukipita changamoto mbalimbali hususan za kiuchumi, nafikiri mwenzangu alipata mtu mwingine. Nami kwa kuwa nilishachoka kuwa mpiganaji wa kulinda penzi letu, nikaona sawa tu, aende nipate pumziko kwingine, pengine hatukuandikiwa...

Baada ya kama miezi 3, tukaanza mahusiano na kijana mwingine mtu mzima kidogo. Kwa kweli, alinijali sana na kunipenda sana. Lakini katika maongezi ni kama tulikuwa watu wawili tofauti. Wakati mimi nikimwambia mategemeo yangu katika mahusiano yetu ni kutulia na kutokuwa na dramas, mwenzangu alikuwa anaongea kana kwamba tuna urafiki wa sex tu na and nothing. Sikuwa na pupa kujua nini alimaanisha.

Kwa bahati mbaya mwenzangu alipata changamoto fulani mambo ya msiba, hivyo akalazimika kubeba majukumu katika familia yao kipindi hiko cha Covid 19. Alinishirikisha nami bila hiyana nikaona nimsaidie jambo ambalo lilimshangaza sana kwani hakutegemea kama ningeweza kujitoa kiasi kile tena katika kipindi cha Covid 19.

Baada ya hapo, upendo uliongezeka ikawa too much sasa kwa uapande wake jambo ambalo mimi nikaanza kupata wasiwasi. Wasiwasi wangu ukazidi pale ambapo jamaa akaanza tabia za kuonyesha dalili zote za kutaka niwe nampatia pesa. Ingawa anafanya masihara lakini ni yale masihara ya kweli. Mara nina ndoto za kufanya hivi nitafutie pesa, mara nataka kile in the future kitatusaidia but kitakaa kwangu and so many dramas.

Kwa kweli maisha ya namna hiyo, nikaanza kupoteza interest naye. Sababu ninaamini kusaidiana kupo na ni jambo la kawaida katika maisha either ya mapenzi ama la, lakini mtu anapomchukulia mwenzake aliyemsaidia kama kitega uchumi, kwa kweli, kwanza inasikitisha lakini pili itakufanya upoteze trust kwa mtu. Hii ni kwa ke na me.

Mpaka sasa nina mwezi sina interest kabisa ya kumtafuta mwenzangu. Sina interest naye kabisa naona hata yeye amegundua hivyo na ndio maana hanitafuti.

Mwenye kuona funzo na aone.
mimi sijamuona huyo funza kama vipi mtoe kabisa mambo yaendelee

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom