Wajuzi wa TEHAMA njooni hapa mtupe somo

Ndama dume

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
858
1,480
Habarini za asubuhi wanajamvi wenzangu, imani yangu mko salama na tunaendelea kupambana kila kukicha huku tukiombea JF idumu milele.

Naomba kwenda kwenye mada ama ulizo fupi. Kuna rafiki yangu anataka kutengeneza darasa la online na kuna elimu ambayo atakuwa anaitoa japo kwa sasa bado ni siri yake kwanza ila darasa hili litakuwa live streaming ya video kwenye social media mfano YouTube, Instagram, Facebook na kwa wale ambao watakuwa wanatumia Zoom kwa ajili yao private.

Swali langu Je, ni Camera gani ambayo itaweza kummulika yeye mwalimu na ubao wake pasipo kushikiwa kamera hizo na mtu mwingine na kuonekana vizuri kabisa?

Na Camera hizo zitahitaji taa kwa ajili ya kuongezea mwanga na muonekano mzuri?

Karibuni wajuvi na kama upo mtaalaamu wa kuja kufunga kabla hujanifuata PM basi mwagika hapa nipime utaalamu wako huenda pia ukaokota zabibu chini mpera (ajira).

Angalizo usikimbilie kunifuata PM bila kumwagika hapa kwanza jamvini mimi nikiona upo vizuri mwenyewe nitakufuata na kukupa ajira.

Karibuni sana, Yesu anawependa mno na yupo karibu kurudi
 
Pascal Mayalla karibu kwa ajili ya kutoa ushauri na nasaha
Asante kunishtua, ngoja tuwashauri hawa madogo ..
Ndama dume, Mimi sio mjuzi wa tehama, ni Digital Audio Visual Producer.

Technology imepiga hatua kubwa siku hizi, kitu unachohitaji ni kurusha tu signals kwa kuanzia kiwango cha Full HD 1080, hadi 4K. Wala huhitaji hata kuwa na camera, ukiwa na simu janja ya HD unaweza kabisa kujirekodi na kupiga hilo darasa lako. Unahitaji tuu vitu viwili, tripod stand ya simu, na bluetooth earpiece ili uweze kutumia simu hands free.

Advantage ya kutumia simu,
  1. its cheap and very convenient
  2. huhitaji taa,
  3. Una connect online directly
Disadvantage
  1. ni lazima utumie a single shot na single direction, simu huwezi ku change shot wala direction, hivyo somo likiwa refu with a single shot, lazima litaboa.
  2. Wakati ukitumia simu, ukipigiwa simu ita disrupt recording.
Tukija kwenye camera unaweza kununua simple camcorders zozote za HD, ushauri wangu nunua brand ya Sony.

Advantage
  1. Unapata picha nzuri kuliko ya simu interms of quality hadi quality ya 4K
  2. Unaweza ku change shots na directions
Disadvantage
  1. Good cameras ni expensive
  2. Lazima uwe na extra external mic to get good sound quality
  3. Lazima uwe na HDMI extension kutuma HG signals kwenye computer ili kurusha live
Kama unafanya kitu professional, then lazima utumie professional equipments na kazi ifanywe professionally with professionals there is where I came along.

Advantage
  1. Best video quality
  2. Best sound quality
  3. Professional products
Disadvantage
1. Very expensive
2. Lazima utumie ma pro.
3. Lazima utumie lights
4. Hakuna kufanya mwenyewe unless na wewe ni pro.

P
Rejea
Jee Una Kipaji cha Utangazaji?. Jinsi ya Kujiajiri Utayarishaji na Utangazaji Vipindi Vyako vya TV.
 
Asante kunishtua, ngoja tuwashauri hawa madogo ..
Mimi sio mjuzi wa tehama, ni Digital Audio Visual Producer.

Technology imepiga hatua kubwa siku hizi, kitu unachohitaji ni kurusha tu signals kwa kuanzia kiwango cha Full HD 1080, hadi 4K. Wala huhitaji hata kuwa na camera, ukiwa na simu janja ya HD unaweza kabisa kujirekodi na kupiga hilo darasa lako. Unahitaji tuu vitu viwili, tripod stand ya simu, na bluetooth earpiece ili uweze kutumia simu hands free...
Ndio raha ya kuwa na wazee Mungu akubariki. Ila sasa uache ili tabia yako baba angu maana umekulia kwenye uzalendo kuwa mzalendo kweli kweli hadi mbinguni
 
Ndama dume,
Back to the topic:
Honestly uncle katoa ushauri mzuri uliochanganyika na uzoefu. As an IT expert nakazia ushauri wake.
 
gspain,
Ahsante nashukuru kwa kukazia ushauri wa ancle, kwa hiyo wewe ni binamu yangu et mtoto wa shangazi
 
kuna kamera za 3D nimesahau jina lake, ila linaonyesha mwalimu na darasa, mwanafunzi ataamua angle anayotaka kuangalia.
zinatumika sana Japani. Just google 3D cameras
 
kuna kamera za 3D nimesahau jina lake, ila linaonyesha mwalimu na darasa, mwanafunzi ataamua angle anayotaka kuangalia.
zinatumika sana Japani. Just google 3D cameras
Waooh ahsante sana ngoja niangalie
 
kuna kamera za.3D nimesahau jina lake, ila linaonyesha mwalimu na darasa, mwanafunzi ataamua angle anayotaka kuangalia.
zinatumika sana Japani. Just google 3D cameras
Kuna mdau mmoja kaniambia pia ninunue vile vicamera vya streaming live social media ninue viwili hivi alafu ninunue na stand vitakuwa poa sana je ni kweli
 
Nimefuatilia maelezo ya Mr. Pascal Mayalla amekuhusisha kwa usahihi kwa kiwango chake. Naomba kuongeza kupitia mstari wake!

Ukihitaji kufanya Live Streaming hasa katika Digital Streaming Platforms na Playgrounds sio lazima kuwa na heavy equipments rather medium equipments (As Mr. Pascal said utaweza kutumia simu).

Katika simu bado UTAWEZA kufanya multi stream na kubadili angels kutokana na setup utakayofanya. Kwa kuintergrate na Streaming Softwares na kuhakikisha umeweka mf, simu tatu sehemu tatu tofauti.

Utaziunga na Production au Live Streaming Softwares ambazo lazima zihusike ku-integrate katika uchakataji wa kurusha katika mitandao husika hapa software zikiwa on air haziathiliwi na other moduli na functionality za simu i.e calls stuff to interrupt!

Katika hili utahitaji mtu behind the deck kuhakikisha somo lako linafika kwa usahihi kwa kutumia integration na Live Streaming Softwares/Services mfano wa AI Media, BoxCast, DJI, EasyLive, Vimeo Live, Stage Ten, StreamYard kuwezesha kurusha the same story at the same time katika mitandao husika. For the conference mode wengi wataenda na Zoom lakini ni kuenesha kiwango kidogo cha matumizi ya akili pia hutoa data zao kwa Uchina.

Light and Audio Setup ni muhimu kuongeza ufanisi na kwa sasa zinapatikana kwa kiasi affordable.
 
Nimefuatilia maelezo ya Mr. Pascal Mayalla amekuhusisha kwa usahihi kwa kiwango chake. Naomba kuongeza kupitia mstari wake!

Ukihitaji kufanya Live Streaming hasa katika Digital Streaming Platforms na Playgrounds sio lazima kuwa na heavy equipments rather medium equipments (As Mr. Pascal said utaweza kutumia simu)...
Waooh hebu njoo PM huku tuhojiane vizuri mbona nimependa mwandiko wako ghafla njoo nifundishe kusoma a to z
 
Back
Top Bottom