Wajuzi wa kesi za ardhi hii imekaaje

the kind

JF-Expert Member
Nov 6, 2019
773
574
Kwanza poleni na pilika za kutafuta lakini pia hongereni kwa ile riziki tuliyoipata, hakika Mungu ni mwema na wa kutumainiwa.

Bila kuwachosha, kuna kesi ya ardhi ambayo ipo baraza la ardhi Wilaya ambayo inawahusisha familia ya mzee fulani na shule ya jumuiya ya wazazi.

Kimsingi kuna eneo lenye ukubwa wa hekari 2 ambalo lilikuwa linamilikiwa na mzee fulani eneo ambalo limepakana na shule hiyo ila yule mzee alifariki miaka 5 imepita sasa na eneo lile kwa sasa linamilikiwa na familia ya mzee huyo.

Hapo awali walikuwa wanalitumia eneo hilo kama shamba lakini baadae wakaanza kukata viwanja kwa wao wenyewe na baadhi kuuza kwa watu kadhaa.

Siku moja, mmoja wa ile familia alikuwa anaandaa tofali eneo hilo kwa ajili ya ujenzi ndipo uongozi wa shule ukaibuka na kudai kuwa lile ni eneo la shule na wasitishe ile shughuli, na siku chache baadae second master akawa amekwenda kufungua kesi mahakamani dhidi ya yule mwanafamilia kuwa amevamia eneo la shule.

Baada ya hukumu Mahahakama ilimpa haki yule mwanafamili kuwa ndio mmiliki halali wa eneo lile.

Baada ya uongozi wa shule kushindwa kesi mahakamani wakaamua kuipeleka kesi ile baraza la kata lakini nako mwanafamilia yule alipewa haki kuwa ndio mmiliki halali wa eneo lile na akakabidhiwa kisheria.

Then mwezi wa 9 kukawa na zoezi la urasimishaji sasa watu wa ardhi wakawa wamekuja kwenye kata hiyo kwa ajili ya upimaji. Wakati wanataka kuanza kupima eneo hilo uongozi wa shule ukaibuka tena na kuomba wasipime kwani eneo hilo lina mgogoro na wakadai kuwa kesi hiyo iko baraza la ardhi Wilaya. So ikabidi watu wa ardhi waache kupima baada ya kusikiliza pande zote mbili.

Ikapangwa tarehe ya kusikilizwa shauri hilo kwenye baraza la ardhi (Mahakama ya ardhi) kama niko sawa ambayo ilikuwa ni tarehe 7/11/2019 na ilipofika tarehe hiyo shauri halikusikilizwa kwani hakimu alikuwa na udhuru na ikapangwa tena tarehe ya leo 14/11/2019 lakini pia shauri halikusikilizwa sababu mlalamikaji alidai kuwa Wakili wake amepata ajali hivyo shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena tarehe 4/2/2020.

Swali la msingi:
Nini kifanyike kwa upande wa familia maana muda unapotea lakini pia mambo ya pesa yamekuwa changamoto kwao kundeshana na kesi na pia wanashindana na jumuiya ya wazazi ambao ndio watawala wa nchi.

Kwa ambae ana uelewa na mambo kama haya au amepitia changaamoto kama hii, ushauri wenu wanajamvi.

Nawasilisha.

20191114_105006.jpeg
 
Wamekata rufaa au wamefungua kesi upya, maana kama walishindwa baraza la kata walitakiwa wakate rufaa baraza la wilaya.
 
Baada ya uongozi wa shule kushindwa kesi mahakamani wakaamua kuipeleka kesi ile baraza la kata lak
hapo hapaeleweki! hiyo ni mahakama ipi? maana nijuavyo, mashauri ya aedhi huanzia baraza la kata, then baraza la wilaya, then high court kitengo cha ardhi, and finally Court of appeal! sasa hiyo mahakama kabla kwenda kata ni ipi?
 
Back
Top Bottom