Wajuzi wa karate, ni kwanini Bruce Lee alikuwa anajikaza sana wakati wa kupigana?

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,871
8,381
Watalaam wa karate naomba mnisaidie hili, Ni kwa sababu gani Bruce Lee akiwa anapigana alikuwa anajikaza Sana mwili na kutoa sauti Kama za paka, Mara apige kelele za ajabu.

Yaani kajamaa unkuta kamekakamaa yaani.

1608187992960.png
 
Kujikaza ni mwembwe tu ili aonyeshe misuli yake.Kumbuka alikuwa ni mcheza sinema.Mpiganaji hodari mara nyingi anapigana akiwa amerelax ili asipoteze nguvu.Angalia wale ma-master wa kung fu jinsi wanavyokuwa wamerelax

Zile sauti za ajabu zinaitwa Kiai.Lengo lake ni kuongeza mzuka wa kupigana.
 
Picha na video nyingi za Bruce Lee ni za kwwnye movies na sio za maisha yake halisi
Acha kudanganyika yule jamaa inasadikika chanzo kikubwa cha kifo chake ni uvimbe ambao ulijitengeneza kwenye ubongo wake kwa sababu alizidisha mazoezi kupita kiasi.Kitendo cha kukakamaa ni mbinu za kikarate kwenye kuutia ganzi mwili ili mwili uwe kama resistance kwa pigo kutoka kwa adui pia inasaidia kwenye kuachia effective pigo kwa adui.
 
Sawa doniyeni
 
Watalaam wa karate naomba mnisaidie hili, Ni kwa sababu gani Bruce Lee akiwa anapigana alikuwa anajikaza Sana mwili na kutoa sauti Kama za paka, Mara apige kelele za ajabu.

Yaani kajamaa unkuta kamekakamaa yaani.
Bruce alikuwa anapigana na kuigiza reality, kipindi kile hakuwa na mambo mengi ya kusaidiwa na mixers za computer..kama sasa.

ile kutoa sauti ndy style yake,, analia sauti kama paka au kuramba damu au kujifuta pua kwa dole gumba.

Yote ni ktk kujipa mzuka kwenye mapigano.

waigizaji wa sasa wengi wanasaidiwa na computer ktk kuigiza picha za mapigano.
 
Sadhguru alisema ili kuamplifiy CHI.

Hivyo ndo maana anaweza kumpiga mtu one inch punch na kuangua huko tena anavaa na protector ili asiumie tumbo au kifua.

And that's why anakuwa anatoa sauti za paka nk kuamplifiy CHI.

According to sadhguru.
 
Back
Top Bottom