Wajuzi kwenye biashara ya mazao

Wajuzi kwenye biashara ya mazao

sinyoritah

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2012
Posts
552
Reaction score
346
Habari ya mchana wakuu,

Wenye ufahamu na biashara ya mazao naomba tupeane ABCD hapa. Kuhusu ununuaji, uuzaji vitu vya kuzingatia masoko n.k wa mazao mfano Mahindi.

Tufundishane pia jinsi ya kuanza chini (start low) kwa wasio na capital, njia za kupita na hatimaye kufanikiwa.
 
sinyoritah,

Nimewahi seat nasubir mazao kama tangawizi, alizeti, mchele, vitunguu swaum, korosho.....
 
Nami nilikua na wazo la kuanzisha biashara ya nafaka, nasubiri wajuzi wa mambo
 
Kuna ndugu yangu alikuwa ananunua mahindi meeengi kipindu cha mavuno halafu anayapiga dawa na kuyahifadhi mpaka yatakapoanza kupanda bei ndo anayauza lakn aliacha sijui ata sababu ilikua ni nini..... Ngoja nkamuulize akinipa jibu ntarudi apa
 
Mchele, korosho Na ufuta ndo mazao ya Pesa Na utajir nje nje, Ukiwa Na mtaji tu,, Kwa mfano mchele, sahiv had 1100 ukienda mikoani unaupata
 
Mazao yote yana faida, tafuta chanzo, jua bei ya kununua, kusafirisha...... Tafuta soko na ujue taratibu zake.... Dalali hakwepeki hapa
 
Mazao yote yana faida, tafuta chanzo, jua bei ya kununua, kusafirisha...... Tafuta soko na ujue taratibu zake.... Dalali hakwepeki hapa
Umenena vyema na ndo maana pia ya uzi huu wanaojua watusaidie chanzo,watwambie bi ya kununulia na watujuze masoko yake yakoje the rest mtu ataenda research mwenyewe physically akiwa kapata mwanga
 
Andaa mtaji wako kadri uwezavyo zama mtwara msimu ni mwez wa tisa mpaka wa kwanza mwanzoni. Utanunua kwa wa kulima kwa bei kati ya 1500-2200 per kg na utauza ghalani kwa njia ya mnada kati ya 3600-4000 kulingana na soko likoje.

Hili ni kwa zao la korosho.

Maeneo zinako patikana kwa wingi ni nachingwea, masasi, tandahimba, liwale n.k kimsingi ukikomaa vizuri unatoka.

Mwez wa NNE mpk wa sita kuna zao la ufuta utanunua kwa 1500-1700 utauza 2200-2800 kulingana na soko likoje.

Nimeshea ninacho fahamu ngoja wengine waje
 
Ni biashara inayohitaji hela, ukishakuwa na hela kazi yako kujua faida kiasi gani unapakia mzigo.....
 
M2pc

Asante Mkuu hii nilishawahi ifanya ila kwakua kazi yangu ilikua kuagiza nilidhurumiwa nalipwa kidogo kidogo hadi leo pesa ya toka mwaka jana mwezi wa 10 na nahisi silipwi tena ,cha msingi katika hizi mazao nadhani unahitaji kujiengage mwenyewe ila sasa kwa walioajiriwa changamoto inaanzia hapo,wenzetu mnafanyaje?
 
Back
Top Bottom