"kupenda" ni hisia chanya ya kuingiwa na kitu moyoni kwa sababu ya mvuto au uzuri wake. Lakini kutamani ni hisia ama chanya au hasi ya kuwa na shauku kubwa na kitu. Mfano ukiwa na shauku kubwa ya machungwa, basi unaweza kusema, "Natamani machungwa." Na hiyo ni hisia chanya. Lakini inakuwa hasi pale inapochanganyikana na hisia ya kutotaka wengine wapate. Mfano, umepewa chakula kiasi chako, lakini unataka upate zaidi (yaani bila kujali kuwa mwingine atakosa) - hiyo ni tamaa - lakini kama hisia hasi.