GE2025 Wajumbe Arusha wafanya yao kura za maoni viti maalum, Catherine Magige atupwa nje

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Ndoto za waliokuwa wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kurejea bungeni huenda zikakwama baada ya kushindwa kuwashawishi wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha.

Wabunge hao amao wamapata kura pungufu, sasa watasubiri huruma ya Kamati Kuu ambayo ndiyo itatoa uamuzi wa mwisho. Katika uchaguzi uliomalizika usiku wa kuamkia leo, Wanasiasa Martha Kivunge na Chiko Issa wameibuka kidedea katika kura za maoni za kusaka ubunge wa Viti Maalum (UWT) Mkoa wa Arusha baada ya kuibuka na idadi ya kura nyingi katika uchaguzi uliohusisha wagombea wengine sita.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kennani Kihongosi alitangaza matokeo ya uchaguzi huo kuwa Martha alipata kura 1004, akifuatiwa na Chiko aliyepata kura 775. Wajumbe wa uchaguzi huo walikuwa 1,261.

Kura halali zilizopigwa zilikuwa 1,245 na kura saba ziliharibika.

Wagombea wengine na idadi ya kura walizopata ni pamoja na Catherine Magige (213), Asanterabi Lowassa (196), Zaytuni Swai (141), Navoi Mollel (95), Martha Amo (50) na Lilian Badi (9).
 
Lilian Badi alipata kura za wale watu 9 aliowalambisha asali.
 
Wasubiri chadema ikifungua milango wahamie huko
sub
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…