MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,209
- 2,389
Wabongo ndiyo maana kina Andrew Chenge na mafamba yao ya Harvard wanawafisadi kila siku, tuambie wamefanya au hawajafanya nini, sio wana au hawana vyeti gani.
Watu wa dizaini hii ndio wale ukiwapigia suti kali, umeingia ofisini na mpambe wa kizungu, unawatapeli mpaka unawauzia kiwanja baharini pale Salender Bridge, si unaonekana mtanashati? Wao wanaangalia vitu kwa nje nje badala ya kuangalia undani wa mambo.
Actually kumuita mtu mwenye elimu rasmi ndogo (mkazo upo katika neno rasmi, mtu anaweza kuwa na elimu rasmi ndogo lakini akawa na elimu kubwa, na kuwa na elimu rasmi kubwa na kuwa na elimu ndogo) ... so kumuita mtu mwenye elimu rasmi ndogo Kihiyo ni matumizi mabaya ya hilo neno.
Neno Kihiyo lilianza kutokana kwa bwana Kihiyo aliyefoji vyeti na kujifanya amepata elimu rasmi kubwa kuliko ukweli. Kwa hiyo, hata kama mtu hajaenda shule kabisa, kama hajafoji vyeti huwezi kumuta Kihiyo.
NA WEWE UNAANGUKIA HUMO HUMO NINI, MBONA UMEKUJA JUU HIVYO!!!! ACHA LONGO LONGO SHULE MUHIMU BWANA!:smile-big: