Wajue Rockafeller Family: Familia tajiri zaidi Marekani na Duniani

Mkuu C.T.U ok,ntasubiri kwani hapa hatubishani tunaelimishana tu,tena ukizingatia tunazungumzia dunia ambayo hatukuwepo,ni muhimu kuresearch,ila sielewi ni kitu gani ambacho watu wanabishana na wewe kuhusu authority unayotumia wewe kuutaja utajiri wa Rockefeller mbona mie naona uko sahihi tu!umetoa link ya wealthiest historical figures toka wikipedia,sasa humo kwenye wikipedia mbona wametaja hiyo figure?tena hawajasema familia bali wamemtaja mtu mmoja JOHN D ROCKEFELLER kuwa mwaka 1937 wakati anakufa alikuwa na net worth in the range of 392 to 663 billion dollars equal to 1.53% of the total U.S annual GDP in his day!wakaongezea kuwa "when considering the real value of his wealth,Rockefeller(John D) is widely held to be the wealthiest person in history.tena huyu John hakurithi huu utajiri,aliutafuta mwenyewe(kwa mujibu wa hizi mainstream media mnazoziona ziko sahihi ingawa mie siamini kila wasemacho) kama akina Gates(kama kweli utajiri ni wa Gates mwenyewe isijekuwa ni Rockefellers hao hao secretly behind Microsoft kukwepa case kama za standard oil zisiwakute tena!),akitokea kuwa wholesale grocer?si kama namkubali no,simpendi huyu mtu kwa kuwa utajiri wake aliupata kwa usanii wa hatari!jamaa alianzisha kampuni ya kusafisha mafuta huko U.S.baadae akaanza kununua kampuni moja moja za kuchimba mafuta.akaanzisha stores na stations,akawa anachimba yeye,anasafisha yeye,anauza yeye.kuwamaliza wapinzani wake waliobakia akaweka mkakati ambao kila nikiukumbuka naangua kicheko huku hasira zimenishika.mafuta yalikuwa yakichimbwa kwa kiwango kikubwa kwenye eneo moja la U.S liitwalo Cleveland.jamaa aliongea na railway companies zote zilizokuwa zikisafirisha mafuta toka machimbo kuja viwandani,akawapa rushwa ili watengeneze rebate kwa mapipa yake na ya wapinzani wake,yaani kila pipa kama gharama yake ya kusafirisha ni 60 basi waipandishe hadi 100 halafu hiyo 40 inayozidi wamrudishie baadae lengo likiwa ni kuwakomoa wapinzani wake.hata zile 40 zilizozidi kwenye pipa za wapinzani wake akawa analamba na jamaa wa treni.kwa hiyo kadri wapinzani wake walivyosafirisha mapipa mengi walikuwa wakimchangia yeye na kujimaliza wao kwa pesa zao wenyewe.halafu wakifika sokoni,yeye mafuta bei chini,wenzie bei juu,jamaa wakafilisika mmoja baada ya mwingine na kumuachia machimbo mengi akawa main producer.kuwamaliza wenye viwanda vya kusafisha mafuta na station,stores kama zake,akaanza kupunguza uzalishaji mafuta huku akipandisha bei ya crude oil,matokeo yake wenzie wakashindwa kununua mafuta kwake,as long as yeye ndio mchimbaji mkubwa ikabidi wamwachie biashara yote hadi kuuza.akawa ana-monopolize biashara ya oil marekani nzima.jamaa wakamstukia na kumshitaki kukiuka sheria ya Sherman inayotetea uwepo wa ushindani wa kibiashara na 1911,mahakama kuu ya marekani ikaamuru standard oil igawanywe kuwa kampuni ndogo 33.kampuni hizi ndizo msingi mkuu wa makampuni makubwa ya mafuta marekani na duniani leo hii kama vile Esso,ExxonMobil,Carter Oil,Imperial Oil,Mobil,Chevron,Texaco,Amoco(imeungana na BP leo)Atlantic,Anglo-american na utitiri wa makampuni ya mafuta yenye jina la standard oil kulingana na states yalipo mf.standard oil of New Jersey,Brazil etc!hata hao Forbes wanalist jamaa kama the richest american in history huku akiwa na utajiri ambao ni 1.53% of U.S economy wakati huo.Wapo na wengine ambao utajiri wao ulivuka 100 billion kama Cornelia Vanderbilt(178.4 billion),Jacob Astor(116 billion),Andrew Carnegie(297.8 billion),J.P Morgan etc!hiyo 663.4 bilion ni mtu mmoja anaitwa JOHN D ROCKEFELER na si familia.(narudia kwa mujibu wa media rasmi mnazopenda nyie mie siamini sana story zao)haya yameandikwa wikipedia na mtu akitaka source wikipedia imetoa reference kibao,Forbes ikiwemo.sasa sielewi kwa nini watu bado wanabisha!labda sijaelewa dhana ya mabishano yenu!
Duh

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom