Wajue hijra, ama jinsia ya tatu kutoka India

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,171
2,077
Jamii ya Hindu huko India tangia zamani za kale wamekuwa wakiishi na watu wanaojitambulisha kama wasio na jinsia, yaani sio wa kike wala sio wa kiume. Ndani ya jamii, watu hawa wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kutoa baraka kwa watoto, baraka kwa wenzi wa ndoa ili kuongeza uzazi, biashara ya kulala, kupitia shughuli hizi ndivyo walivokuwa wakijipatia kipato.

Jamii ya watu hawa huzaliwa kama wanaume ila wakishajitambua huukacha mwanaume na kuanza kuishi kama wanawake. Pia hawabaki nyumbani, huondoka na kwenda kuishi kwa kikundi kilicho karibu nawo.

28THELOOK10-jumbo-v2.jpg

angalia aunti alivyopendeza tizama shingo yake ilivyo ndefu.

mkoloni anachafua hali ya hewa

Mnamo karne ya 19, mwingireza alitawala India kwa kuweka sheria zake. Mojawapo ya sheria ilikuwa ni kosa kwa mwanamme kumjua kingono mwanamme mwenzake. Watu wa India walikuwa wakiendelea na taratibu zao za Kuwalala kwa pesa hawa hijra na mkoloni alikuwa hajui kinachoendelea. kasheshe ikaanza baada ya kesi ya mauwaji kufunguliwa, kesi ilikuwa ikimuhusu hijra mmoja aliyeuawa na mwanaume aliyesemekana ni mpenzi wake wa zamani kutokana na wivu wa kimapenzi. Hapa ndipo mkoloni anashangaa ! Kumbe hizi njema zinabanduana, mkoloni kwa kutumia vyombo vyake akanza kamata kamata kubwa, na kupiga marufuku shughuli zote za hijra Ata zile za kubariki.

Jumla ya miaka 83 mkoloni aliyotawala ilitosha sana kuwapakaza taswira mbaya hawa viumbe maana hata baada ya mkoloni kuondoka hii jamii imekuwa haitendewi haki kama ilivyokuwa siku za kale. Wengi wanaishi kwa kuomba omba, kuuza baraka na biashara ya ngono, ambako mara nyingi wanazurumiwa na wateja korofi. Na kupata haki kumekuwa ni kitendawili.

Mara baada ya Mkoloni kuonja na kuonjwa, amekuwa akihaha usiku na mchana kupiga kampeni kuhamasisha watu wa mataifa waungane naye kwenye huo mchezo. Labda ni kwasababu ya ulimbukeni wakee tu au akikua ataacha au ni laana aliyoipata baada ya kutowatendea vyema hivyo ana jukumu la kusambaza.

Hata hivyo jamii ya namna kama hirja ilikuwepo sehemu mbalimbali katika tawala mbalimbali, mfano china walikuwepo, kwa waarabu walikuwepo na pia kwa herufi kubwa UGANDA walikuwepo kipindi yupo kabaka inasemekana alikuwa akiwalala watu wa namna hiyo, tusubiri mda tu huyu Mganda ndiye atakuwa kampeni meneja wa Haya Mamboo mark my words.
 
Jamii ya wa Hindu wanaamini Gender zipo tatu, Masculine, Feminine and Gender Neutral (ndio hao wakina Hijras) hata hivyo India inatambua uwepo wa Transgender na sheria zimewekwa za kuwalinda.
 
Jamii ya wa Hindu wanaamini Gender zipo tatu, Masculine, Feminine and Gender Neutral (ndio hao wakina Hijras) hata hivyo India inatambua uwepo wa Transgender na sheria zimewekwa za kuwalinda.
Bado kuna stigma tofauti na hapo kale. Ingawa Hijra wakongwe wanakuambia unafuu wa sasa ni kuwepo kwa operesheni za kubadili jinsia mahospitalini hapo kale walikuwa wanajifanya wenyewe kienyeji... Siwezi kuimagine maumivu waliyokuwa wanapata.
 
Back
Top Bottom