Wajasiriamali tuongee na kupeana uzoefu

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,358
Naomba wajasiriamali au wafanyabiashara tupeane uzoefu hasa kwenye kuajiri:

1. Unatumia vigezo gani kumuajiri mtu?
2. Unapataje mtu sahihi wa kukufanyia kazi zako?
3. Unatumia vigezo gani kumuamini kumpa aendeshe kitengo kizima?
4. Unatumia vigezo gani kumlipa?
5. Unatumia vigezo gani kufanya "delegation"?
6. Ni wakati gani muafaka wa kufanya "delegation"?

Copy to:
FaizaFoxy Money Stunna Malila Chasha Poultry Farm Kubota Red Giant mexence melo Mike McKee
 
Last edited by a moderator:

hapa nafikiri naweza jibu maswali kama matatu maana projects zangu bado ndogo.
1. swali la kwanza. mi naajiriri mtu/kibarua kwa kuangalia gharama yake, ukaribu kwenye eneo la kazi na majukumu yake. watu wenye majukumu mengi hasa ya kifamilia ni vigumu kufanya nao kazi hasa kama ndiyo unaanza na hauna mtaji mkubwa. pia watu waliokupita sana umri hawafai, watataka kukupatronize kwenye kazi yako.

2.swali la pili. mii hutafuta watu ambao wamewahi fanya hiyo kazi na mi mwenyewe hufanya sana research ili kazi isiharibike.

3. swali la nne. mi huangalia wengine huwa wanalipaje.
 
Nashukuru kwa mchango wako mkuu
 
1.kigezo cha kumuajiri mtu kila mtu anaangalia ambacho anaona sahihi kwake,wengine wanaangalia elimu ya mtu,wengine wanaangalia uzoefu wa mtu

2.Namna ya kumpata mtu sahihi ni kutangaza,na kupokea maombi kisha kuyachuja kulingana na vigezo vyako.

3.Unamuamini mtu kwa kumsoma tabia yake kulingana na unavyokaa naye na kuona utendaji wake wa kazi,na kumfanyia uchunguzi uko kwenye social media kama facebook ni vitu gani anapost,mfano mzuri kuna dada mmoja aliniomba nimsaidie kutafuta kazi tanzania au popote pale ni raia wa Uganda,nikawa kabisa kwenye hatua ya kumsaida lakin nikaona anaweka picha za dushelele tena govi kama picha yake kwenye whatsapp,nikaacha na kufuta wazo la kumsaidia kutafuta kazi.
 
Naomba wajasiriamali au wafanyabiashara tupeane uzoefu hasa kwenye kuajiri:

1. Unatumia vigezo gani kumuajiri mtu?
2. Unapataje mtu sahihi wa kukufanyia kazi zako?
3. Unatumia vigezo gani kumuamini kumpa aendeshe kitengo kizima?
4. Unatumia vigezo gani kumlipa?
5. Unatumia vigezo gani kufanya "delegation"?
6. Ni wakati gani muafaka wa kufanya "delegation"?

Copy to:
FaizaFoxy Money Stunna Malila Chasha Poultry Farm Kubota Red Giant mexence melo Mike McKee

1. Sina kigezo maalum cha kumuajiri mtu. Inategemea na kazi yenyewe lakini karibu mara zote ni "trial and error" na ndiyo maana tuna "probation period".

Unamuajiri kwanza kisha ndiyo unaona kama anaiweza kazi anayoifanya na kama haiwezi (ambazo ni mara nyingi zaidi) huwa anaondoka mwenyewe na kupotea kabla hajafukuzwa.

2. Hii imekuwa ni shida kubwa sana Tanzania, na nnadiriki kusema ikiwa umempata mtu "sahihi" Tanzania hii wa kukufanyia kazi zako ni bahati kubwa sana, na ni muujiza.

Mpaka sasa sijapata mfanyakazi ambae hata aliyefikia (80% reliability), ni shida kuwa sana.

3. Sijawahi kupata wa kumuamini 100% kumpa aendeshe kitengo kizima, tunaowaacha waendeshe kitengo, tunajaribu kuwa na "close monitoring" ya kuweza kubaini mapungufu mapema na kusawazisha.

4. Hapa ni tatizo kubwa sana na sina kigezo, natumia njia ya "Boss na mbwa wake", umeshawahi kusikia kisa cha "boss na mbwa wake?" Hakuna zaidi.

5. Inategemea na kazi afanyayo huyo unaempa "delegation of authority". Kwanza uzoefu wake, kisha muelekeo wake "attitude".

6. Always, ni lazima uwe na certain degree ya ku delegate authority. Ukipenda usipende, its unavoidable.
 
1.kigezo cha kumuajiri mtu kila mtu anaangalia ambacho anaona sahihi kwake,wengine wanaangalia elimu ya mtu,wengine wanaangalia uzoefu wa mtu

2.Namna ya kumpata mtu sahihi ni kutangaza,na kupokea maombi kisha kuyachuja kulingana na vigezo vyako.

3.Unamuamini mtu kwa kumsoma tabia yake kulingana na unavyokaa naye na kuona utendaji wake wa kazi,na kumfanyia uchunguzi uko kwenye social media kama facebook ni vitu gani anapost,mfano mzuri kuna dada mmoja aliniomba nimsaidie kutafuta kazi tanzania au popote pale ni raia wa Uganda,nikawa kabisa kwenye hatua ya kumsaida lakin nikaona anaweka picha za dushelele tena govi kama picha yake kwenye whatsapp,nikaacha na kufuta wazo la kumsaidia kutafuta kazi.

Wazo zuri mkuu. Nataka kuweka formal kila kitu ninachofanya. Nataka nikiajiri niweze kuwaachia wasaidizi wasimamie kila kitu na nikirudi nikute hakuna kilichoharibika.
 
1. Sina kigezo maalum cha kumuajiri mtu. Inategemea na kazi yenyewe lakini karibu mara zote ni "trial and error" na ndiyo maana tuna "probation period".

Unamuajiri kwanza kisha ndiyo unaona kama anaiweza kazi anaifanya na kama haiwezi (ambazo ni mara nyingi zaidi) huwa anaondoka mwenyewe na kupotea kabla hajafukuzwa.

2. Hii imekuwa ni shida kubwa sana Tanzania, na nnadiriki kusema ikiwa umempata mtu "sahihi" Tanzania hii wa kukufanyia kazi zako ni bahati kubwa sana, na ni muujiza.

Mpaka sasa sijapata mfanyakazi ambae hata aliyefikia (80% reliability), ni shida kuwa sana.

3. Sijawahi kupata wa kumuamini 100% kumpa aendeshe kitengo kizima, tunaowaacha waendeshe kitengo, tunajaribu kuwa na "close monitoring" ya kuweza kubaini mapungufu mapema na kusawazisha.

4. Hapa ni tatizo kubwa sana na sina kigezo, natumia njia ya "Boss na mbwa wake", umeshawahi kusikia kisa cha "boss na mbwa wake?" Hakuna zaidi.

5. Inategemea na kazi afanyayo huyo unaempa "delegation of authority". Kwanza uzoefu wake, kisha muelekeo wake "attitude".

6. Always, ni lazima uwe na certatin degree ya ku delagate authority. Ukipenda usipende, its unavoidable.

Namba 2, 3 & 5.

Nimeona baadhi ya makampuni yanaajiri mtu awe kiongozi wa kampuni au branch ya kampuni. Kama Bakhressa alivyofanya kwa Azam Media inayoongozwa na mtu mwingine kabisa. Na baadhi ya makampuni yanafanya hivyo, utakuta ameajiri COO wa kampuni labda toka sehem nyingine na yeye anakuwa pembeni anaendelea na shughuli zake. Kuna baadhi ya makampuni yanaajiri CEO's.

Hii inakaaje kwa hapa Tanzania, ukatafuta mtu aliebobea huko nje ya nchi ukamuajiri akusukie kitengo kizima kiwe productive and operational?
 
Changamoto za huko nje ni tofauti na za hapa Tanzania,huyo CEO anatakiwa awe amepitia mazingira yenye changamoto nyingi na ngumu kama hizi hapa nchini na akafanikiwa,huyo ataweza kua productive kwenye ofisi yako.
 
Namba 2, 3 & 5.

Nimeona baadhi ya makampuni yanaajiri mtu awe kiongozi wa kampuni au branch ya kampuni. Kama Bakhressa alivyofanya kwa Azam Media inayoongozwa na mtu mwingine kabisa. Na baadhi ya makampuni yanafanya hivyo, utakuta ameajiri COO wa kampuni labda toka sehem nyingine na yeye anakuwa pembeni anaendelea na shughuli zake. Kuna baadhi ya makampuni yanaajiri CEO's.

Hii inakaaje kwa hapa Tanzania, ukatafuta mtu aliebobea huko nje ya nchi ukamuajiri akusukie kitengo kizima kiwe productive and operational?

Kwanza Azam kama group of companies, imewachukuwa muda mrefu sana kufika hapo walipo, "trial and error" method imetumika sana walipokuwa "wadogo" na inaendelea kutumika hapo Azam hadi leo hii.

Katika level ya kuweza ku delegate authority, S.S Bakhresa & Sons, wameajiri watu wa nje wengi na Watanzania wachache ambao wako "close monitored", always.

Pia usisahau, Azam wana wafanyakazi waliotoka nao tangu wapo "wadogo" ambao waliwapata kwa njia hiyo hiyo ya trial and error ambao wengi wao hawana elimu ya juu lakini ni wachapa kazi na waaminifu, hao wapo na ingawa kuna wasomi lakini utashangaa hawa few reliable waliokuwepo wanathamani zaidi kwa Azam. Na sasa wengi wao watoto zao wameenda shule na wanaajiriwa hapo hapo kutokana tu na umahiri walioonyesha wazee wao.

Ukibahatika kupata muujiza wa kupata wafanyakazi "reliable" Tanzania hii, hakuna cha kukuzuwia kufanikiwa.
 
Nimeelewa kitu. Asante
 
Namba 2, 3 & 5.

Nimeona baadhi ya makampuni yanaajiri mtu awe kiongozi wa kampuni au branch ya kampuni. Kama Bakhressa alivyofanya kwa Azam Media inayoongozwa na mtu mwingine kabisa. Na baadhi ya makampuni yanafanya hivyo, utakuta ameajiri COO wa kampuni labda toka sehem nyingine na yeye anakuwa pembeni anaendelea na shughuli zake. Kuna baadhi ya makampuni yanaajiri CEO's.

Hii inakaaje kwa hapa Tanzania, ukatafuta mtu aliebobea huko nje ya nchi ukamuajiri akusukie kitengo kizima kiwe productive and operational?
Kama biashara yako ni mpya unashauriwa utumie angalau miaka 3 kuisuka vile unavyotaka iwe, kumbuka wewe kama founder ndio mwenye vision ya jinsi gani unataka biashara yako iwe na wapi inaelekea, kwani biashara yako ina turnover kiasi gani hadi unataka kuweka ceo na wewe utakuwa unafanya nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom