Wajasiriamali jihadharini na utapeli huu

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,150
2,000
Yaani sijui ni ugumu wa maisha au sijui ni kukua kwa utandawazi.Walaji wa sungura hapa nchini wameongezeka na wanazidi kuongezeka kwa kasi kweli kweli, kuliko hata walaji wa kuku, mbuzi, Kitimoto, ng'ombe nk.

Sungura mmoja aliyechomwa au kubanikwa huuzwa kati ya TZS 36 - 65,000.

Kampuni ya NAMAINGO ndiyo kampuni inayojishughulisha na uuzwaji na usambazaji wa sungura nje na ndani ya nchi. Wanafanya kazi na benki ya NMB na TFDA - Tanzania Food & Drugs Authority katika kuwahakikishia walaji ubora wa chakula /nyama ya sungura.

Wahi fursa hiyo.
Watanzania wenzangu msidanganyike na kuingia kwenye biashara hii. This is a typical white elephant business.
Ni nani ambaye yuko tayari kununua sungura mmoja kati ya TZS.36,000/- hadi 65,000/-????
Mnunuzi yuko Tanzania hii hii ya Magufuli ambayo hadi mabiashara makubwa yanaanguka kwa kukosa wateja?
Namaingo acheni utapeli. Namaingo acheni ubabaishaji. jsenyinah tafuta shughuli halali ambayo MUNGU atakubariki nayo, wacha kuwaingiza wenzako choo cha watoto ambacho kimejaa ma poti na pampas zilizotumika, wakapata aibu ya kujisaidia maungoni.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,150
2,000
Utapeli mwingine huu.
Namaingo mlituaminisha biashara ya kware inalipa na tiba, kumbe uwongo mtupu.
Sungura na wenyewe ni muendelezo wa utapeli wenu.
Ni Wapi sungura wa kuchoma wanauzwa DSM?
Namaingo mlisababisha kuku wa Kuchi wauzwe laki Tano, wanunuzi hawakujitokeza, watu wakapata hasara
 

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,343
2,000
Utapeli mwingine huu.
Namaingo mlituaminisha biashara ya kware inalipa na tiba, kumbe uwongo mtupu.
Sungura na wenyewe ni muendelezo wa utapeli wenu.
Ni Wapi sungura wa kuchoma wanauzwa DSM?
Namaingo mlisababisha kuku wa Kuchi wauzwe laki Tano, wanunuzi hawakujitokeza, watu wakapata hasara
Sungura wanapigiwa upatu sana na kampuni ya tbcc - tanzania business creation company- Ndio hao Namaingo?
 

G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,290
2,000
Kama walivo kuku choma kila mahali unapata, ndivo na mfugaji solo lake lilivyo, popote atauza' Hawa sungura choma sijawai on a mahali wanauzwa"
 

adolf440

JF-Expert Member
Sep 19, 2015
251
250
Haya mambo bana, hatari sana, tuna tatizo kubwa sana la uelewa hapa Tanzania, kitu kinaanzishwa kwa kauli za kuvutia na watu kwa akili ya kupata fedha za haraka haraka basi wanaingiza mitaji yao midogo walioisotea kwa muda mrefu, ghafla inapotea. Walianza na kuku wa Malawi, mayai ya Kware hapa jaribuni kukumbuka promo iliyokuwa inapigwa usiku na mchana ilivyopotea hata sijui ilipoteaje. Biashara zipo nyingi ambazo ukiianzisha na kuisimamia itakusogeza tuu kidogo kidogo.
Usitake tuu kuwa kama Aliko Dangote over night kesho na wewe uagize hiace 600/-
 

Mtu mdogo

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
526
1,000
Hao sungura wa aina mbona huku kwetu kijijini wapo wengi inaweza kuwa fursa hii eeh ?
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,254
2,000
Utapeli mwingine huu.
Namaingo mlituaminisha biashara ya kware inalipa na tiba, kumbe uwongo mtupu.
Sungura na wenyewe ni muendelezo wa utapeli wenu.
Ni Wapi sungura wa kuchoma wanauzwa DSM?
Namaingo mlisababisha kuku wa Kuchi wauzwe laki Tano, wanunuzi hawakujitokeza, watu wakapata hasara
Duh kuchi laki 5?

Hii fursa ilinipotaje??? Ningewauzia majongoo wangu wana jf

Hivi hii biashara ya sungura watu wanaamini????
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom