Wajane milion 115 wanapitia Unyanyasaji

Wajane milion 115 wanapitia Unyanyasaji

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,581
Reaction score
10,111
Takwimu za kidunia zinaonesha kuwa idadi ya Wajane ni takriban millioni 258 kati ya hao, Wajane 115 millioni wanadhulumiwa, wanafanyiwa ukatili, wanakabiliwa na umaskini na kutengwa na jamii.

Tanzania ina idadi ya Wajane 1,396,262 sawa na 4.4% ya Wanawake wote nchini (Sensa ya Watu na makazi mwaka 2022).

Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa
ya Wajane ambayo huadhimishwa tarehe 23 Juni kila mwaka yenye lengo la kuikumbusha jamii kudai haki za Wajane.

Maadhimisho ya Wajane hulenga kutafakari hali zao baada ya kufiwa na wenza wao, kuwaunganisha katika mitandao ya kupata taarifa za fursa za kiuchumi, kijamii na uongozi.

Aidha siku hii hutumika kuelimisha kuhusu haki zao, kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu, kama vile kunyimwa urithi, kufukuzwa nyumbani, kulazimishwa kuolewa, kutengwa na kukosa msaada wa kisheria.
 
Hao wajane sio wa kuwaonea huruma,ukifatilia kwa undani asilimia kubwa wao ndio sababu ya waume zao kufa.
Ex wife ilikuwa kidogo kuniwekea sumu
 
Hao wajane wengi watakuwa Christian na sera yao ya mke mmoja ila jinsia moja kuoawana ruhsa waislamu wana wake wawili wawili kuendelea.
 
Umeongea kwa utafiti gani mkuu au umetoa kichwani
 
Takwimu za kidunia zinaonesha kuwa idadi ya Wajane ni takriban millioni 258 kati ya hao, Wajane 115 millioni wanadhulumiwa, wanafanyiwa ukatili, wanakabiliwa na umaskini na kutengwa na jamii.

Tanzania ina idadi ya Wajane 1,396,262 sawa na 4.4% ya Wanawake wote nchini (Sensa ya Watu na makazi mwaka 2022).

Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa
ya Wajane ambayo huadhimishwa tarehe 23 Juni kila mwaka yenye lengo la kuikumbusha jamii kudai haki za Wajane.

Maadhimisho ya Wajane hulenga kutafakari hali zao baada ya kufiwa na wenza wao, kuwaunganisha katika mitandao ya kupata taarifa za fursa za kiuchumi, kijamii na uongozi.

Aidha siku hii hutumika kuelimisha kuhusu haki zao, kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu, kama vile kunyimwa urithi, kufukuzwa nyumbani, kulazimishwa kuolewa, kutengwa na kukosa msaada wa kisheria.
Tupate idadi ya walioko Tanganyika
 
Back
Top Bottom